Detective J
JF-Expert Member
- Oct 17, 2016
- 18,730
- 29,265
Huyu akujua kama ana mu address raisEti mabango ya KUMTUSI mama RUKHSA!!!
Huyu akujua kama ana mu address raisEti mabango ya KUMTUSI mama RUKHSA!!!
100% hii ndio imemponza
Ataendaje ofisini wakati akiamka hakuna gari ya kwendea ofisini na hata dereva atakuwa hapokei simu yake. Huku walinzi wanamwambia toa kilicho chako mwenye nyumba yuko njiani?Halafu muhusika kalala hana habari, akiamka asubuhi anabeba makabrsha anaenda ofisini, akifika atashangaa watu wakimpa pole.
Sent from my SM-A125F using JamiiForums mobile app
Nafasi yoyote ya kuteuliwa ni high risk. haina dhamana.Kazi za kuteuliwa mbaya kweli
Bado yule DC wa Iringa Kasesela video yake ya matusi ilisambaa sanaIla kwa maneno aliyoyaongea huyo jamaa, kama hiyo ndo sababu ya kutenguliwa, basi naiafiki kabisa.
Mama alisema ataki mabango,akiyakuta,ata wafyeka viongozi.chala anaamka na hangover anawambia waje na mabango hajaishia apo,anakuambia ata kama ya matusiChalamila kilichomponza NI ile ya kusema wezi wawajibishwe
Wengi walioteuliwa ijumaa ni siku yao ya kumcha mungu
Hapi anaenda ku-fail big time Mara, Mama kamsukumia kule ili kumpa nafasi ya kumtimua.Chalamilla hafai kabisa, lakini mama namshangaa bado anaona Hapi anafanyaa kweli? Lakini muda utaongea
Mama kaondoka na kichwa, asubuhi ataamka atashangaa mbona Viete haliji wakati mda wa ofisi tayari?!
Ila Chalamila ameniuma sana, alikuwa ameanza kuchangamsha jiji.Post #63 ukiingia you tube pia utakuta hotuba nzima aliongea vizuri tu nahisi jamaa analazimishaga utani halafu hauwezi siyo mara ya kwanza kuongeaongea vitu vya kipuuzi.
Ila hiyo siyo hapo naona alikuwa anafafanua kauli yake ngoja nitafute ile clip iko somewhere nitaituma hapa soon
Kuteua ni moja ya majukumu ya raisHmm…huyu mama naye kama Magufuli tu sasa.
Anateua leo, jioni anatengua.
Kesho anateua, keshokutwa anatengua!
Hivi hao wateuliwa huwa hawafanyiwi vetting??
NB: Hizi press releases huwa zinatolewa saa ngapi usiku?
Batilda Salha Buriani kutoka uraiani Hadi kuwa RAS mama alichemsha. Hivyo amebuni kumpa ukuu wa mkoa cheo Cha kusiasaRais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo tarehe 11 Juni 2021 amefanya mabadiliko madogo ya wakuu wa Mikoa na kuteua viongozi wengine kama ifuatavyo:-
=====
Rais Samia Suluhu Hassan, ametengua uteuzi wa Mkuu wa mkoa wa Mwanza Albert Chalamila, na kumhamishia mkoa huo Mhandisi Robert Gabriel ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Mara.
Hatua hiyo imetokana na Rais Samia Suluhu Hassan kufanya mabadiliko madogo ya wakuu wa Mikoa na kuteua viongozi wengine.
Taarifa iliyotolewa usiku huu wa Juni 11, 2021 na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Jaffar Haniu imesema katika mabadiliko hayo aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora Ally Salum Hapi anahamia Mkoa wa Mara.
Kwa mujibu wa Taarifa hiyo, Rais Samia amemteua Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga Batilda Salha Buriani kuwa mkuu wa Mkoa wa Tabora kuchukua nafasi ya Ally Salum Hapi.
Aidha Katibu Twala Wilaya ya Simanjoro Zuwena Omari Jiri ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga kuchukua nafasi ya Batilda Salha Buriani.
Taarifa hiyo imesema tarehe ya uapisho wa viongozi wapya itatangazwa baadae
View attachment 1814796