Rais Samia atengua uteuzi wa Albert Chalamila RC Mwanza, Dkt. Batilda ateuliwa kuwa RC Tabora

Halafu muhusika kalala hana habari, akiamka asubuhi anabeba makabrsha anaenda ofisini, akifika atashangaa watu wakimpa pole.

Sent from my SM-A125F using JamiiForums mobile app
Ataendaje ofisini wakati akiamka hakuna gari ya kwendea ofisini na hata dereva atakuwa hapokei simu yake. Huku walinzi wanamwambia toa kilicho chako mwenye nyumba yuko njiani?
 
Huyu mwamba sijawahi kumwelewa kabisa wakati wa uongozi wake.... Either way, huu utenguzi ni "technical" kuwafanya watu waache kujadili budget na kuhamia kwa chalamila
 
Post #63 ukiingia you tube pia utakuta hotuba nzima aliongea vizuri tu nahisi jamaa analazimishaga utani halafu hauwezi siyo mara ya kwanza kuongeaongea vitu vya kipuuzi.

Ila hiyo siyo hapo naona alikuwa anafafanua kauli yake ngoja nitafute ile clip iko somewhere nitaituma hapa soon
Ila Chalamila ameniuma sana, alikuwa ameanza kuchangamsha jiji.
 
dah chalamila naona mdomo umemponza amesifiwa juzi kuwa ni mlipukaji ameenda kuropoka anataka wananchi wamtukane raisi.
juzi alikuwa anawaambia ma Dc hawaelewi hatima yao nakujiona yy amemaliza.
achukue pension yake akajiajiri kama vijana wengine.
uongozi ni zamana tu
kazi iendele
 
Hmm…huyu mama naye kama Magufuli tu sasa.

Anateua leo, jioni anatengua.

Kesho anateua, keshokutwa anatengua!

Hivi hao wateuliwa huwa hawafanyiwi vetting??

NB: Hizi press releases huwa zinatolewa saa ngapi usiku?
Kuteua ni moja ya majukumu ya rais
Rais asipo teua mtaanza pia kulalamika

Ova
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo tarehe 11 Juni 2021 amefanya mabadiliko madogo ya wakuu wa Mikoa na kuteua viongozi wengine kama ifuatavyo:-

=====

Rais Samia Suluhu Hassan, ametengua uteuzi wa Mkuu wa mkoa wa Mwanza Albert Chalamila, na kumhamishia mkoa huo Mhandisi Robert Gabriel ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Mara.

Hatua hiyo imetokana na Rais Samia Suluhu Hassan kufanya mabadiliko madogo ya wakuu wa Mikoa na kuteua viongozi wengine.

Taarifa iliyotolewa usiku huu wa Juni 11, 2021 na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Jaffar Haniu imesema katika mabadiliko hayo aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora Ally Salum Hapi anahamia Mkoa wa Mara.

Kwa mujibu wa Taarifa hiyo, Rais Samia amemteua Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga Batilda Salha Buriani kuwa mkuu wa Mkoa wa Tabora kuchukua nafasi ya Ally Salum Hapi.

Aidha Katibu Twala Wilaya ya Simanjoro Zuwena Omari Jiri ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga kuchukua nafasi ya Batilda Salha Buriani.

Taarifa hiyo imesema tarehe ya uapisho wa viongozi wapya itatangazwa baadae
View attachment 1814796
Batilda Salha Buriani kutoka uraiani Hadi kuwa RAS mama alichemsha. Hivyo amebuni kumpa ukuu wa mkoa cheo Cha kusiasa
 
Viongozi wengi walioteuliwa kutokea upinzani wanafanya vizuri hii inaonesha upinzani unapika viongozi vizuri mf. Juliasi mtatiro, machari hawa vijana mpaka sasa hamjasikia skendo zao japo kuna kipindi mtatiro alitaka kuiga mkumbo wa mwenda zake kwa kuchapa viboko wanafunzi watoro huku akiwa live mainstream nadhani alijirekebisha.

Wengine ni mgwira ambaye amestahafu bila doa na sasa kafulila amepewa mkoa tangu apewe mkoa hatujaskia madoido yoyote, lkn nina mashaka na huyu mlevi mwita waitara naona hana muda mrefu sana kwenye baraza


Sent from my HUAWEI LUA-U22 using JamiiForums mobile app
 
Chalamila hakujua kuchuja maneno. Hana wa kumlaumu isipokuwa mwenyewe.
Sidhani kama alikuwa mtendaji super kiasi hicho
 
Back
Top Bottom