Rais Samia ataziweza 'fitina za Watanganyika'?

Lissu aombwe arejee nchini aendelee na maisha kama zamani.Alipwe pesa za matibabu,marupurupu na mishahara yake alizozulumiwa na Ndugai.
Alipwe fidia kwa usumbufu uliojitokeza.
Kesi ya kushambuliwa kwake ifutwe kwakuwa mhusika mkuu ameshatangulia kwenye hukumu,washirika wake wasamehewe bure.
Hapo Tundu Lissu atakuwa wa msaada sana eneo atakalo tumika.
Thubutu Mbona jiwe litarudi.
 
Hapa haupo sahihi na huo utakatifu atapewa na nani mkuu na swahiba wake Pengo au maana hata Mwalimu hajawa na hatokuwa daima
subiri
20210326_181644.jpg
 
FITINA dawa yake ni JEURI.

Hayati JPM hakusikiliza wala kutetereshwa na FITINA

naamini pia Rais wetu Samia Suluhu atakuwa MADHUBUTI zaidi kuliko hata JPM.

Kamwe Rais wetu usikubali kuyumbishwa kwa Maneno ya; MAJUNGU, FITINA NA UNAFIKI. Maana mambo haya yameota mizizi miongoni mwa watanzania.

kuna Maprofessional wa kuwafiti wenzao, wapiga majungu na wanafiki, watu wenye tabia hizo wapo wengi sana tena cha kushangaza baadhi yao ni viongozi ktk idara mbali mbali,

Ogopa sana watu wenye tabia ya UNAFIKI ni watu hatari zaidi kuliko silaha za nuclear au ugonjwa wa ukimwi na Corona.

watu wenye tabia hiyo ya UNAFIKI tuwe nao makini sana;
njia pekee ni kuwabaini/kuwatambua na kuwaepuka, lkn kubwa zaidi ni kuwapuuza.
Halafu walio wengi ni wabunge wa chama fulani
 
Ukiwa Rais wa Tanzania hasa kama umetokea Zanzibar..kuna changamoto kubwa mno ya kuyajua makundi ya fitina ya watanganyika na namna ya kupambana na fitna zao..

Rais Mwinyi alikuwa 'victim' 'mkubwa Sana wa makundi haya. Ilifikia wakati alikuwa anaona kama mda wa kumaliza urais unachelewa. Rais akiwa mpole na muungwana na mstaarabu kama walivyo Wazanzibari wengi anaweza kujikuta anachezeshwa ngoma na asijue nani mpigaji wa ngoma hiyo.

Yafuatayo ni makundi ya fitina hatari mno kwa Rais yeyote anapaswa kuyajua na kujua namna ya ku-deal nao:

1. Viongozi wastaafu

Hapa Mama Samia ana changamoto kubwa. Hata kama ana support ya Kikwete bado kuna Kina Mzee Warioba
Mzee Butiku Lowassa .Sumaye ..mizengo Pinda n.k. Hawa Wana makundi Yao na watoto wao. Na wana maslahi yao.

2. Team JPM
Hawa wanajulikana. Advantage ni kuwa ushawishi wao utazidi kupungua lakini wana pose threat bado, hasa kama wataunganisha nguvu na makundi mengine.

3. Maaskofu na Baraza la Maaskofu
Hawa Wana uchungu. Mtoto wao hakumaliza miaka 10 na inafahamika alivyowadekeza Samia ategemee waraka na matamko. Sasa wanaona haya tu kum-attack waziwazi Kwa sababu ya ukimya waliompa mtoto wao ambae sitashangaa wakimtangaza 'Mtakatifu'

4. Wana CCM before JPM
Hawa ni wale waliozoea ule msemo CCM ina wenyewe. Hawa hasa hasa wanataka tu 'nafasi za kula' baada ya JPM kuwaweka pembeni mda mrefu.

5. Wanasiasa wa upinzani hasa wale wanafiki
Hapa kuna wanasiasa aina zote. Wenye maslahi yao binafsi hadi wale wa kutumika na makundi mengine hapo juu
Usishangae kuona mwanasiasa wa upinzani akibeba ajenda za Lowasa au Sumaye kuzipigania.

6. Asasi za kiraia (NGOs)
Hapa napo kuna watumikiao makundi mengine hapo juu. Kuna wanaotumikia taasisi za dini zao au hata taasisi za nje na kibano cha JPM ndo kitawafanya now waamke Kwa nguvu kufidia hasara za miaka ya JPM. Wengine ni matumbo yao tu ndo wanahangaikia.

7. Wasiotaka Muungano
Hawa Kwa upande wa Zanzibar watakuwa kimyaa..now wataamka WA upande wa Tanganyika. Rais Mwinyi alikumbana na G-55, nusura wamgeuze Gorbachev. Ili mradi Rais ni mzanzibari sasa utasikia kelele zao na fitina zao.

8. Wenye ndoto za Urais
Hili kundi nalo limepigika vibaya. Litajitahidi mno kuchafuana na hata kumchafua Rais, mradi waweke mazingira
ya wao kuja kuchukua kiti.

9. Makahaba wa siasa
Siku hizi hili kundi linazidi kukua hawana agenda maalum. Wao popote upepo unapoelekea wapo. Kimbelembele ndo sifa yao.

10. Wabunge wenye 'mabwana wengine' wa kuwatumikia.
Hawa wanafahamika. Mama kazi anayo.

12. Waandishi wa habari walionunuliwa
Katika hayo makundi baadhi yana waandishi wao na vyombo vyao vya habari.

13. 'Manipulated crowds'
Hayo makundi baadhi hufanikiwa kuzalisha makundi ya watu wengi kusemea agenda zao. Kupitia media
au matamasha ya kiimani. Tegemea migomo, maandamano na makelele ya kila aina baada ya mda mfupi tu hata mwaka usipite.
Hii ndiyo tunaita hofu ya kitu kisichojulikana.
 
Umeandika upuuzi wa ajabu sana, tatizo la inferiority complex linawatesa sana, Magufuli atafanywa na nani kuwa mtakatifu? hivi mkiwa mnaandika huu upuuzi wenu huwa mnajipa muda kidogo wa kufikiri au mnakurupuka tu? unadhani mtu kuitwa mtakatifu ni suala la kuamka asubuhi na kumpachika hilo jina? huo ni mchakato ambao hata hivyo kwa Magufuli sijawahi kusikia kama upo zaidi ya kelele za mtaani tu ulizoandika hapa.

TEC hawajawahi kusema wanaanzisha huo mchakato, kama una ushahidi weka hapa, kwa haya mawazo yako hutaki Rais akosolewe hata akikosea, kwani wakifanya hivyo utasema wanamu-attack kwasababu ya dini yake, mambo ya imani unayachanganya na siasa kwa maneno ya kuokoteza mtaani, very small mind, halafu wanakuita great thinker!
 
TEC siyo mtu mmoja, ni umoja wa maaskofu huru nchi nzima. Kwahiyo usitegemee watakuwa wanaobgea kila wiki.

Unasema walikuwa wanaunga mkono kila kitu, kipi !??

Leta hapa tamko la TEC linakomuunga mkono Magufuli.




Kuhusu haki za binadamu,


Utawala wa kisiasa, uwe unatekelezwa na jumuiya yenyewe au na vyombo vinavyowakilisha dola, ni lazima daima ufanyike ndani ya mipaka ya sheria ya kimaadili. Lengo lake ni kuyafikia manufaa ya wote, tena manufaa yenye maendeleo yake, kadiri ya kanuni za utaratibu wa kisheria uliokwisha kuwekwa, au wa kuwekwa

Kuhusu KKKT


Hao miaka yote wanasumbuliwa na inferiority complex, hawana hoja za maana zaidi ya kulia lia tu na hisia zao.
 
Mna hofu isiyo na msingi.

Nguvu ya nchi ni Rais ( Jeshi + Hazina )

Ukiona Rais amekuwa mstaarabu ujue ni maamuzi yake. Usifikiri Kikwete au Mkapa hawakuwa na uwezo wa kusema chukua bunduki kammalize Lissu au poreni chaguzi zote!!

Tatizo lenu mnataka Samia na yeye awe Magufuli No. 2 wakati Magu was a total mess.

Hao Team MAGU hawana mizizi, nguvu yao ilikuwa ni Dola na haipo tena. Wengi wao hata siasa za CCM majimboni hawataziweza.

Halafu unaposema eti maaskofu watamfanyia figisu, ni lini maaskofu walishawahi kunyamaza. Hukuwahi kuona mfulululizo wa nyaraka na ukosoaji mkubwa kutoka kwa maaskofu. Au wewe unadhani Askofu mkuu wa Jimbo DSM ndio maaskofu wote, au wakristo wote ukiachana na wachache. Hivi kuna watu walitulia tuli kama waislamu enzi za kwa Magu?

Tena hadi Makonda, maana kawahonga mnoo pesa.

Hao waliokuwa wananyenyekea Magu haikuwa sababu ya Ukatoliki wake baki nguvu ya mamlaka yake.

Kina warioba mnawaonea tu maana mtu kama Warioba sijawahi kuona akifanya figisu yoyote.

Ninachokiona labda mnatafuta defensive mechanism, akiboronga ionekane anafanyiwa figisu kwasababu ya Uzanzibar wake, Dini au mwanamke.

Kwasasa ngoja apange timu yake amalize ili asimlaumu mtu yeyote.

Urais hauko hivyo, kwamba unyamazishe kila mtu na akubali kunyamaza tuliii. Noooo.

Kama unajijua kuwa hupendwi kusemwa, kukosolewa, wala kuambiwa chochote ni bora usiwe Rais maana siyo lazima.

Watu wataongea tu hata nje ya nchi.

tofautisha kuongea,kutoa maoni,wazo
na kupinga.

hivyo ni vitu tofauti,ukiwa na hoja ama maoni hakuna ambaye hatakuwa tayari kukusikiliza,shida ni pale unapofanya moja kati ya hayo kwa maslahi yako lazima utavuruga mambo.
 
Rais mwinyi anasema Zanzibar imeoza kwa ufisadi na kila leo anatumbua juzi kawakimbiza viongozi wa vikosi vya kmkm
Sio KMKM pekee, wengine ni JKU na Chuo Cha Mafunzo kwa kadhia ya watumishi hewa.
 
tofautisha kuongea,kutoa maoni,wazo
na kupinga.

hivyo ni vitu tofauti,ukiwa na hoja ama maoni hakuna ambaye hatakuwa tayari kukusikiliza,shida ni pale unapofanya moja kati ya hayo kwa maslahi yako lazima utavuruga mambo.
Kupinga nini ??
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom