Rais Samia ataziweza 'fitina za Watanganyika'?

Rais Samia ataziweza 'fitina za Watanganyika'?

Usimsikilize huyu muongo Kabisa
Apson hakuwahi kufanya kazi Kwa pamoja na Anna Tibaijuka...

Acha kujitoa ufahamu.
Labda wadanganye watoto wa chekechea.
Apson kama "DG wa TISS" alikuwa anafanyakazi na mawaziri wote, including Prof Tibaijuka!
Ushahidi huu hapa kwenye ibara ya 5(1)(b) ya sheria ya TISS (1996).
1688311232607.png
 
Usimsikilize huyu muongo Kabisa
Apson hakuwahi kufanya kazi Kwa pamoja na Anna Tibaijuka...
Kikwete alipoingia alimteua Othman Rashid miezi mitatu ya kwanza Tu..
Tibaijuka alikuja kuteuliwa baadae hapo wizara ya ardhi...
Huyu anaongea uwongo alio tunga kichwani mwake...
Tibaijuka aliingia kwenye politics nadhani kwenye uchaguzi wa 2010.
 
unapoint ila waislamu umeshindwa kuwaweka sababu ni dini ingekuwa katoka kigoma raisi na dini muislamu ungekalia ukabila
 
Mkataba wa Barrick umewezesha kuanzishwa Kampuni ya Madini ya Twiga ambapo Watz tuna 16% toka zero %!! Unajitambua kweli wewe? Pia tumeshapata 600B. Nafikiri utakuwa taahira wewe!
Hapo umesema uwongo au tuseme ulikuwa hujui.

Free carried shares ya Serikali kwenye makampuni ya madini, kabka ya Magufuli ilikuwa 10%, haikuwa 0%. Magufuli aliongeza toka 10% hadi 16%. Mrabaha ulikuwa 4%, aliongeza mpaka 6%.
 
Mna hofu isiyo na msingi.

Nguvu ya nchi ni Rais ( Jeshi + Hazina )

Ukiona Rais amekuwa mstaarabu ujue ni maamuzi yake. Usifikiri Kikwete au Mkapa hawakuwa na uwezo wa kusema chukua bunduki kammalize Lissu au poreni chaguzi zote!!

Tatizo lenu mnataka Samia na yeye awe Magufuli No. 2 wakati Magu was a total mess.

Hao Team MAGU hawana mizizi, nguvu yao ilikuwa ni Dola na haipo tena. Wengi wao hata siasa za CCM majimboni hawataziweza.

Halafu unaposema eti maaskofu watamfanyia figisu, ni lini maaskofu walishawahi kunyamaza. Hukuwahi kuona mfulululizo wa nyaraka na ukosoaji mkubwa kutoka kwa maaskofu. Au wewe unadhani Askofu mkuu wa Jimbo DSM ndio maaskofu wote, au wakristo wote ukiachana na wachache. Hivi kuna watu walitulia tuli kama waislamu enzi za kwa Magu?

Tena hadi Makonda, maana kawahonga mnoo pesa.

Hao waliokuwa wananyenyekea Magu haikuwa sababu ya Ukatoliki wake baki nguvu ya mamlaka yake.

Kina warioba mnawaonea tu maana mtu kama Warioba sijawahi kuona akifanya figisu yoyote.

Ninachokiona labda mnatafuta defensive mechanism, akiboronga ionekane anafanyiwa figisu kwasababu ya Uzanzibar wake, Dini au mwanamke.

Kwasasa ngoja apange timu yake amalize ili asimlaumu mtu yeyote.

Urais hauko hivyo, kwamba unyamazishe kila mtu na akubali kunyamaza tuliii. Noooo.

Kama unajijua kuwa hupendwi kusemwa, kukosolewa, wala kuambiwa chochote ni bora usiwe Rais maana siyo lazima.

Watu wataongea tu hata nje ya nchi.
Usifananishe Magufuli na upuuzi
 
Porojo tu ooh umaarufu wa JPM umepungua! Nani kakudanganya? Sasa mmemhonga Lissu kala kamaliza anataka mumhonge tena,kazi mnayo,atawaharibia na kumvua nguo Mama yenu.
 
Hizo nyingine 84% zinamilikiwa na nani? Acha hasira twende taratibu
84% zinamilikiwa na mwekezaji. Mwekezaji amegharamia utafiti, mine development, na anagharamia uchimbaji na processing. Sisi tunapewa hisa za bure 16% kwa sababu ni mali ya asili ya kwetu. Hii ni tofauti kabisa na ule ushenzi wa DP. Kwene bandari, maji na ardhi ni vyetu, bandari tumeijenga wenyewe, miundombinu mingi tumeigharamia wenyewe, wao wanakuja tu kuongezea vifaa na kusimamia uendeshaji.

Kwenye madini ambako hatujawekeza chochote tuna 16%. Kwenye bandari ambako tumwekeza matrilioni ya pesa, tukiukubali ushenzi wa DP, tutakuwa na 0%.
 
Fatma Karume now kajiunga na kundi la kumpinga Rais Samia baada ya Ally Karume kufukuzwa Ccm...

Nilisema wastaafu Wana watoto wao...Mama awe Makini..
 
Ni wakupuuzwa tu mana hata uhulu hawajaunga mkono.

Kuna wanaosifia tawala za wanaowaita waswahili kwa siri twende nao sinia likiwekwa kati wao watakimbilia nyama kama kawaida yao
 
Ni wakupuuzwa tu mana hata uhulu hawajaunga mkono.

Kuna wanaosifia tawala za wanaowaita waswahili kwa siri twende nao sinia likiwekwa kati wao watakimbilia nyama kama kawaida yao
"Uhuru"
 
The Boss uzi wako nimeukumbuka. Nadhani uliona mbali sana.

Mama hatoboi 2025, kwasabb HAWEZI, HAFAI na ni WAKUJA
 
Back
Top Bottom