Rais Samia atakumbukwa kwa kujenga uchumi unaowagusa Watanzania

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Jul 28, 2022
15,262
9,713
Ndugu zangu, wanasema uchumi mzuri ni ule unao gusa maisha ya watu wengi. Ukimfuatilia vizuri Mh. Rais wetu utagundua kuwa anajenga uchumi wenye kumgusa kila Mtanzania.

Kwanza Mh. Rais ametambua kuwa kilimo ndio sekta iliyo ajiri watanzania wengi wa makundi tofauti tofauti. Hivyo juhudi zozote za kuujenga uchumi wetu ni sharti ukipe kipaumbele kilimo.

Ndio maana unaona ongezeko la bajeti katika wizara ya kilimo na hata utoaji wa ruzuku takribani billioni 150. Hii inakwenda kuchochea uzalishaji, lakini pia kundi kubwa linakwenda kuguswa kupitia mipango hii ya Rais wetu mpendwa.

Mh. Rais wetu smedhamilia kuhakikisha kuwa, katika kujenga uchumi wetu hakuna mtu au kundi lolote linaloachwa nyuma au kusahaulika. Hali hii inajidhihilisha kwa namna anavyojenga miradi mbalimbali inayogusa maisha ya watu hasa wanyonge.

Ndio maana unaona miradi kama shule, vituo vya afya, zahanati, huduma za maji na umeme vikitamalaki kila Kona ya nchi hii.

Rais wetu pia anajitahidi kuhakikisha kuwa mfumuko wa bei unaoikumba dunia unapunguzwa kwa kuweka ruzuku kwenye mafuta ambayo ni injini ya uchumi wetu. Ndiyo maana unaona akitoa karibu billioni mia moja kila mwezi.

Rais Samia mama yetu Atakumbukwa sana akimaliza uongozi wake 2030, kwa kujenga uchumi unaogusa watanzania hasa wakipato cha chini. Kazi ya serikali ni kusaidia watu kunyanyuka kiuchumi, kazi ambayo Mh. Rais wetu anaifanya vyema sana.

Mama hakika yupo kazini, tunamuhitaji mama aendelee kututumikia hadi 2030. Ndio tutajuwa tufanye nini akitufikisha hapo, kikubwa tunaendelea kumuombea uzima na afya njema.
 
Umetumia muda mrefu kuandika hii yote ni kwa sababu hukujielewa vzr nn unafanya yawezekana sio kosa lako, Ninyi ndio wale ambao wanasema wanamasikio lkn hawasikii na mna macho na mmeyatumbua watu wanadhani mnaona kumbe ninyi ni vipofu.kuna mambo kwa jinsi yalivyo huitaji kumuelekeza mtu.
 
48f77601f422d2e99baec29c6e2b7492.jpeg
 
Ndugu zangu wana JF tuungane kwa pamoja kuacha kuchangia nyuzi za aina hii.
Hata usipochangia bado kazi za mh Rais wetu zitaendelea kukumbukwa na Watanzania ,maana mh Rais anafanya kazi za kuacha Alama ya kukumbukwa katika mioyo ya Watanzania.

Ni Rais mwenye upendo na nchi hii, Ni kiongozi mnyenyekevu na msikivu Sana, Ni jemedari aliye mstari wa mbele kuipigania nchi yake, NI Dereva anayeendesha nchi hii kwa umakini kwa kuhakikisha kuwa tuna fika salama,

Tumuunge mkono Rais wetu na Tumpe ushirikiano wetu, Juhudi zake za kuijenga nchi hii Ni kubwa Sana, Ndio maana unaona ameanza kwa kutuunganisha watanzania ili Tuwe kitu kimoja na tusonge mbele kwa paamoja
 
Umetumia muda mrefu kuandika hii yote ni kwa sababu hukujielewa vzr nn unafanya yawezekana sio kosa lako,Ninyi ndio wale ambao wanasema wanamasikio lkn hawasikii na mna macho na mmeyatumbua watu wanadhani mnaona kumbe ninyi ni vipofu.kuna mambo kwa jinsi yalivyo huitaji kumuelekeza mtu.
Mpe pongezi mh Rais wetu kwa kazi kubwa anayoifanya, husikii wenzetu wanavyolia Hali ngumu,
 
Huyu mama ataendelea kujua rangi za Watanzania,akitoka madarakani,nadhani hakujifunza kwa Magu.Kama JPM alipondwa vile na alikua vile,huyu mama itakuaje?Aisee.
Kazi za mh Rais zitasimama kumtetea na kumsemea hata Kama tusipomsemea, lakini Mimi nitaendelea kumsemea Rais wangu popote pale
 
Mpumbavu Mmoja wee,

Maisha yalivyopanda Ghari, uchumi wa mtu Mmoja Mmoja unazidi kushuka, Masikini wanakua wengi,

Unapata muda wa kufungua Nyuzi JF kusifia kisichokuwepo?

Mjinga mmoja wee, mijitu kama nyie hutafuta nafasi za teuzi ,na mnapopata Huwa hamna Impact chanya yoyote sababu Vichwa vyenu vimejaa kujipendekeza na ujinga

Hivi mbona JPM Mwamba, alisema "Nitabomoaa,"... Anabomoa kweli ,

Lkn bado akapewa URAIS wa Nchi hii?

Achen kutafuta Teuzi Kwa kupiga Domo .. nahili jambo ndo linaloumiza Taifa hili, hatuwi na viongozi wenye uwezo Bali tuna maviongozi sababu ya midomo Yao

Shame on you!
 
Mpumbavu Mmoja wee,

Maisha yalivyopanda Ghari, uchumi wa mtu Mmoja Mmoja unazidi kushuka, Masikini wanakua wengi,

Unapata muda wa kufungua Nyuzi JF kusifia kisichokuwepo??


Mjinga mmoja wee, mijitu kama nyie hutafuta nafasi za teuzi ,na mnapopata Huwa hamna Impact chanya yoyote sababu Vichwa vyenu vimejaa kujipendekeza na ujinga


Hivi mbona JPM Mwamba, alisema "Nitabomoaa,"... Anabomoa kweli ,

Lkn bado akapewa URAIS wa Nchi hii??

Achen kutafuta Teuzi Kwa kupiga Domo .. nahili jambo ndo linaloumiza Taifa hili, hatuwi na viongozi wenye uwezo Bali tuna maviongozi sababu ya midomo Yao


Shame on you!!!
Mfumuko wa Bei mh Rais anaendelea kuweka juhudi za ziada kulikabili, mfano ametoa billioni Mia moja hamsini kwenye kilimo na Sasa mbolea itauzwa Elfu 70 kutoka huko ilikokuwa kwa laki na nusu, hapa amemsaidia mwananchi mnyonge kuokoa pesa zake kwa ajili ya matumizi mengine ya kimaisha

Katika mafuta nako anatoa Ruzuku ya billion Mia moja kila mwezi, bila kufanya hivyo Hali ingekuwa mbaya zaidi

Mh Rais anaendelea pia kusogezs huduma za kijamii karibu na wananchi, ili kumpunguzia mzigo wa kusafiri umbali mrefu kutafuta huduma
 
Labda uchmi wa kwako binafsi, usiwataje wananchi kabisa hapo
Uchumi wa watanzania wengi unategemea secta ya kilimo ambako huko utakuta mh Rais ameweka mkono wake wa Ruzuku ya billion Mia moja hamsini ili mkulima amudu Bei za mbolea, hii itamsaidia mkulima kukuza kipato chake na uchumi wake kwa kuwa uzalishaji utaongezeka

Hapo Kama ana mtoto akienda shule anakuta Elimu bure kwa kuwa mh Rais ni Rais mwenye huruma anayetaka kuona watoto wa wananchi wanyonge nao wanapata fursa ya Elimu bila shida,sasa hapo hajasaidia au unataka Rais wetu afanye Nini ndio ulizike wewe.
 
Mfumuko wa Bei mh Rais anaendelea kuweka juhudi za ziada kulikabili, mfano ametoa billioni Mia moja hamsini kwenye kilimo na Sasa mbolea itauzwa Elfu 70 kutoka huko ilikokuwa kwa laki na nusu, hapa amemsaidia mwananchi mnyonge kuokoa pesa zake kwa ajili ya matumizi mengine ya kimaisha

Katika mafuta nako anatoa Ruzuku ya billion Mia moja kila mwezi, bila kufanya hivyo Hali ingekuwa mbaya zaidi

Mh Rais anaendelea pia kusogezs huduma za kijamii karibu na wananchi, ili kumpunguzia mzigo wa kusafiri umbali mrefu kutafuta huduma
Unaona ulivyo mpumbavu, unasifia mbolea 70000 wakati tulikuwa tunanunua 45000 kipindi cha mwendazake,
 
Unaona ulivyo mpumbavu, unasifia mbolea 70000 wakati tulikuwa tunanunua 45000 kipindi cha mwendazake,
Lazima ujuwe Mambo yanabadilika, acha kukalili, wewe unafikiri Bei zimepanda Tanzania pekee, mh Rais wetu amejitahidi Sana ukiangalia Hali Ilivyo kwa Sasa duniani kwote, lakini pia mh Rais amefanya juhudi kubwa kuvuta wawekezaji wa viwanda vya mbolea ili waje kuwekeza hapa nchini.
 
Ndugu zangu, wanasema uchumi mzuri Ni ule unao gusa maisha ya watu wengi, ukimfuatilia vizuri mh Rais wetu utagundua kuwa Anajenga uchumi wenye kumgusa kila mtanzania.

Kwanza mh Rais ametambua kuwa kilimo ndio secta iliyo ajiri watanzania wengi wa makundi tofauti tofauti, Hivyo juhudi zozote za kuujenga uchumi wetu Ni sharti ukipe kipaombele kilimo, Ndio maana unaona ongezeko la bajeti katika wizara ya kilimo Na hata utoaji wa Ruzuku takribani billioni 150, hii inakwenda kuchochea uzalishaji, lakini pia kundi kubwa linakwenda kuguswa kupitia mipango hii ya Rais wetu mpendwa.

Mh Rais wetu Amedhamilia kuhakikisha kuwa katika kujenga uchumi wetu Hakuna mtu au kundi lolote linaloachwa nyuma au kusahaulika, Hali hii inajidhihilisha kwa namna anavyojenga miradi mbalimbali inayogusa maisha ya watu hasa wanyonge, ndio maana unaona miradi Kama shule, vituo vya Afya,zahanati,huduma za maji na umeme vikitamalaki kila Kona ya nchi hii.

Rais wetu pia anajitahidi kuhakikisha kuwa mfumuko wa Bei unaoikumba Dunia unapunguzwa kwa kuweka Ruzuku kwenye mafuta ambayo Ni injini ya uchumi wetu, ndio maana unaona akitoa karibu billioni Mia moja kila mwezi.

Rais Samia mama yetu Atakumbukwa Sana akimaliza uongozi wake 2030 kwa kujenga uchumi unaogusa watanzania hasa wakipato Cha chini, kazi ya serikali Ni kusaidia watu kunyanyuka kiuchumi, kazi ambayo mh Rais wetu anaifanya vyema Sana.

Mama hakika yupo kazini, Tunamuhitaji mama aendelee kututumikia Hadi 2030, ndio tutajuwa tufanye Nini akitufikisha hapo, kikubwa tunaendelea kumuombea uzima na Afya njema.
Hawezi kamwe kumfikia Magufuli!
Hizo Fedha nyingi zinaishia mifukoni mwa wachache
 
Back
Top Bottom