Rais Samia ataka mazungumzo ujenzi wa Hospitali ya Apollo nchini

benzemah

JF-Expert Member
Nov 19, 2014
1,504
3,034
Screenshot 2023-11-06 163423.png

Rais Samia Suluhu Hassan ameitaka Wizara ya Afya kukufua mazungumzo ili kuhakikisha kituo cha umahiri na ubobezi wa kimatibabu 'Apollo Hospital' kinajenga jijini Dar es Salaam na kukamilika ifikapo mwaka 2026.

Hayo yamesemwa leo Novemba 6, 2023 wakati ujumbe wa Rais wa Apollo Group Hospitals, Dk Hari Prasad ulipomtembelea na kuwa na mazungumzo juu ya mchakato unaoendelea baada ya kikao cha siku tatu kati ya hospitali hiyo na Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Afya.

Uwekezaji huo utaokoa fedha nyingi za kigeni ambazo Serikali imekuwa ikitumia kutibu Watanzania nje ya nchi, pia utaleta chachu katika uchumi wa nchi, kuongeza fedha za kigeni na utaambatana na teknolojia za kisasa.

"Tumekuja Tanzania kuanzisha kituo cha matibabu bobezi, sisi tunaziba pengo lililopo na hatuji kwa sababu ya mashindano na watoa huduma wengine, tunaamini katika hili ujio wa bima ya afya kwa wote pia utasaidia watu kupata huduma bora zaidi Tanzania na Baraza la Afrika," amesema.

Amesema katika mazungumzo na Rais Samia alisisitiza namna watakavyosaidia kuleta huduma za kibingwa nchini ikiwemo matibabu kwa watoto wenye matatizo ya moyo na hasa Yale magonjwa ambayo bado Watanzania wanafuata huduma India.

"Tulisaini makubaliano kati ya Tanzania na India, tumekaa hapa kwa siku tatu, tumeangalia sera zilizopo na kuona eneo ambalo tutawekeza tumefurahi sana na tunaamini miaka miwili ijayo tutaweza kuanzisha huduma kwani tunashauku na hatuna wasiwasi kuwekeza Tanzania," amesema Dk Prasad.R

Mwananchi
 
Back
Top Bottom