Rais Samia asizibe masikio dhidi ya kelele za watanzania kupinga kifungu cha 23(4) cha Mkataba wa awali wa DP World ambacho ni cha kitumwa

Mama Amon

JF-Expert Member
Mar 30, 2018
2,021
2,479
1687676550312.png


Waziri Mkuu, Cassim Majaliwa, alitoa hotuba zuri kuwaalika watanzania kutoa mawazo kuhusu mkataba wa DP World ili serikali iyapokee na kuyachambua. Lakini sasa ni kama bosi wake anamkana.

Jana, Rais Samia akiwa anazungumza baada ya wananchi waliokuwa wamejitokeza kumpokea katika eneo la Tengeru kuanza kuimba nyimbo zenye maneno "Samia Sema, Sema usiogope sema" aliwajibu kwa kusema:

"Nimeshasema wanangu, mimi sina maneno mengi, mimi vitendo tu ndio vingi. Wakisema mimi [naziba] masikio hivi (huku akitumia mkono wake kuziba sikio la kushoto) naangalia wapi ninakwenda, kwa hiyo waseme sisi tunafanya” (Sikiliza na kutazama video hapa)

Ni vizuri kwa viongozi kuwa na fokasi. Lakini, napenda kumkumbusha Rais Samia kwamba ni vizuri zaidi kiongozi kuwa na fokasi inayofukuziwa kwa msaada wa matendo halali, yanayotekelezwa katika mazingira halali.

Kinachohitajika ni fokasi halali, matendo halali na mazingira halali. Hii ni kanuni ya utatu wa utawala bora. Mkataba wa awali kati ya Tanzania na DP World unavunja kanuni hii.

Katika hili, bado watanzania wanataka kusikia kauli ya Rais Samia kuhusu kifungu cha 23(4) katika Mkataba wa awali wa DP World. Watu wanasema bila kumung'unya maneno, kwamba hiki ni kifungu cha kitumwa. KInasomeka hivi:

1687676033966.png


Ukisoma ibara ya 20 inayotajwa hapo juu ndio unaona vizuri utata wa mkataba wenyewe. Inasomeka hivi:

1687677509134.png


1687677537572.png


1687677561714.png


Uchambuzi wa ibara hii ya 20, unaonyesha kuwa, hakuna sehemu ambapo Jukwaa la Usuluhishi (Tribunal) linalotajwa linapewa mamlaka ya kuvunja mkataba huu, na hivyo kupindua dhamira ya urafiki wa milele iliyotajwa kwenye kifungu cha 23(4).

Nataka niweke mtazamo wa kisheria kuhusu mipaka ya mamlaka ya kimahakama katika kusuluhisha migogoro ya kimkataba kama ifuatavyo: Mahakama Kuu ya Nigeria, katika kesi ya, Osun State Government v. Daiami Nigeria Limited, Senior case no. 277/2002, ilisema yafuatayo katika jambo hili:

“Strictly speaking, under our [common] laws, once parties have freely agreed on their contractual clauses, it would not be open for the courts to change those clauses which parties have agreed between themselves, it was up to the parties concerned to negotiate and to freely rectify clauses which they find to be onerous. It is not the role of the courts to re-draft clauses in agreements but to enforce those clauses where parties are in dispute."

Habari ndio hiyo. Na itikadi ya utumwa ni mtoto wa itikadi ya mfumo mbari (racial superiority ideology). Wabantu ni mbari iliyoonja machungu ya utumwa mikononi mwa mbari ya Waarabu. Kwa hiyo, mkataba wa DP World wenye kifungu cha kitumwa hauwezi kukubalika kwa Wabantu. Utalipasua Taifa kwa kuzalisha kanda za masetla wa Kiarabu (Arabic Sttlers Zones).

Kwa hiyo, namsihi Rais Samia asizibe masikio dhidi ya kelele za watanzania kuhusu kifungu hiki cha 23(4) ambacho ni kifungu cha kitumwa katika Mkataba wa awali wa DP World.

Utumwa ni itikadi inayofuta sifa ya utu aliyo nano binadamu na badala yake kumvisha sifa ya ukitu. Ni itikadi inayotukuza "ukituaji wa binadamu," yaani "objectification of human persons."

Kwa mujibu wa Martha Nussbaum(1995), katika makala yake, "Objectification," pamoja na Rae Langton(2001), katika makala yake, "Autonomy Denial in Objectification," "ukituaji wa binadamu" ni kitendo cha kumtumia mtu kama mwili ambao ni nyezo ya kufanikisha malengo binafsi bila kujali sifa zingine za kibinadamu alizo nazo (instrumentality). Kwa mfano:
  1. kumwondolea mtu uhuru wa kufikiri kwa kumnyima taarifa sahihi (inertness);
  2. kumwondolea mtu uhuru wa kuamua atakavyo kwa kumnyima taarifa sahihi (denial of autonomy);
  3. kumchukulia mtu kama kitu kinachoweza kutumiwa na kisha kuwekwa pembeni baada ya kupoteza thamani halafu nafasi yake ikachukuliwa na kitu ambacho bado kina thamani, kama inavyotokea kwa ganda la muwa (fungibility);
  4. kumchukulia mtu kama kitu kinachoweza kuteketezwa (violability);
  5. kumchukulia mtu kama kitu kinachoweza kununuliwa, kuuzwa na kumilikiwa (comodification);
  6. kumchukulia mtu kama kitu kisicho na hisia (denial of subjectivity);
  7. kumchukulia mtu kama kitu kisicho na haki ya kusema fikra zake (silencing).

Yote haya Waarabu waliwafanyia Wabantu, na bado baadhi ya makovu hayajapona.

Kwa ujumla, utumwa ni itikadi inayopingana na ibara ya 12(1) ya Katiba ya Tanzania, ambayo Rais Samia ameapa kuilinda. Na kuwaingiza watanzania katika utumwa ni kuwauza. Pia, kutoa rasilimali za Tanzania kwa kwa "mfuga watumwa" ni kuuza nchi kwake. Kunahitajika mantiki ndogo kufikia mahitimisho haya.

Kwa vile, ushahidi wa kimazingira unaonyesha kuwa Rais Mstaafu wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete, pia alishiriki kwenye ziara ya juzi huko Dubai, basi naye tunamwomba amsaidie Rais Samia kuondokana na aibu hii.

Kifungu hiki katika Mkatana huu ni kashfa ya MIlenia. Ni kifungu kinachoweza kumwondoa Rais Madarakani kwa kuwa utumwa unavunja ibara ya 12(1) ya Katiba ya Tanzania (1977), ambayo ameapa kuilinda.

Kuhusu uvunjwaji wa Katiba hoja yangu iko hivi: Huwa tunapima utiifu na ukiukaji wa katiba kwa kutumia chujio la kimantiki lifuatalo:
  1. Dokezo kuu: Kama kuna ibara X iliyovunjwa, basi, kuna ukaidi wa Katiba umefanyika.
  2. Dokezo dogo: Kwa mujibu wa seti ya ushahidi Y, ibara X imevunjwa.
  3. Hitimisho: Kwa hiyo kuna ukaidi dhidi ya Kanuni X umefanyika.
Kwa kutumia chujio hili nimeridhika kwamba, hoja ifuatayo ni sahihi:
  1. Dokezo kuu: Kama ibara ya 12(1) ya Katiba ya Tanzania (1977) inayotetea usawa wa binadamu wote bila kujali tofauti za kijinsia imevunjwa, basi kuna ukaidi wa kikatibaunatokea.
  2. Dokezo dogo: Ni ukweli kwamba, utumwa unakiuka kanuni ya usawa wa binadamu, na kwamba ibara ya 23(4) katika Mkataba wa DP World inahalalisha utumwa wa Wabantu wa Tanzania chini ya Waarabu wa Dubai.
  3. Hitimisho: Kwa hiyo, kuna ukiukaji wa Katiba unafanyika dhidi ya ibara ya 12(1) ya Katiba ya Tanzania (1977).
Changamoto hii ya ukiukwaji wa Katiba ya nchi kutokana na mkataba kati ya Tanzania na Taifa la Kiarabu imeimarisha tetesi na minongono iliyokuwepo huku mitaani.

Watu wamekuwa wanahoji: Kwa kuzingatia historia tata kati ya waarabu na wabantu, Idara ya Usalama wa Taifa ilikuwa wapi kuikabidhi Tanganyika na Zanzibar kwa watu amba wana nasaba ya Kiaarabu?

Hussein Mwinyi wa Zanzibar ni Mwarabu kwa asili, na utaratibu wa kukodisha visiwa unaoendelea huko Zanzibar unatafsiriwa kama kuviuza visiwa hivyo kwa Waarabu, ambapo tayari visiwa 16 vimekodishwa.

Samia wa Tanzania Bara ni Mwarabu kwa asili. Mkataba wa awali wa DP World unazo dalili za kuuza bandari zetu. Umeziibua tetesi zinazohusu kutoaminika kwa viongozi wenye nasaba ya Kiarabu na kuzipa uhalali.

Kwa kauli yake ya sasa, ni wazi kwamba, Rais Samia ameshindwa kujifunza kusoma saikolojia ya kisiasa (political psychology) na kuchukua hatua stahiki. Joto la homa ya kisiasa liko juu hadi nyuzi sentigredi arobaini. LInahitaji kushushwa. Lakini bado anaweza kujisahihisha.

Wito: Watu wote tuliokula kiapo cha kuheshimu na kutetea utakatifu wa Katiba ya nchi tunapaswa kufanya hivyo kila mahali na kila wakati bila kuchoka ili tusije kupoteza sifa ya kuendelea kukalia viti tunavyovikalia leo.

Naambatanisha mkataba mzima wa DP World.

1687676118377.png
 

Attachments

  • MKATABA KATI YA TANZANIA NA DUBAI KUHUSU UENDESHAJI WA BANDARI ZA TANZANIA.pdf
    2.3 MB · Views: 6
mkataba wa ulaghai
watoto watasoma huu mkataba kwenye maarifa ya jamii darasa la tano 2100 nimekaa pale
(hautakuwa tu ule wa Mangungo)
 
Haya majitu mengine ndio Marehemu Prof Seith Chachage aliyaeleza kwenye kitabu chake cha Makuwadi wa Soko Huria kupitia mhusika anayeitwa Japhet lupocho .ambaye baada ya kuwa kuwadi wa Mooney aliporwa busara na Hekima yake na kumwachia bepari Mooney kuwa na kauli na uamuzi wa mwisho
 
Kauli aliyoitoa Samia ni ya kijinga sana.

Haiwezekani mtawala mwenye akili zako timamu, uambiwe mahali fulani kuna tatizo, halafu wewe badala ya kutazama uone kama kweli tatizo lipo, unajibu kwa ufupi tu, siwaskii/nimeziba masikio, hii ni dharau kwa watanganyika, lakini pia, ni ujinga uliopitiliza wa kiongozi husika.

Hivi huyu msaliti yupo accountable kwa nani kama sio kwetu anaotuongoza?

Kama mtawala huwezi kuyajibu yale unayoulizwa yanayohusu mamlaka yako, badala yake unajidai uko busy kuwafanyia kazi wanaokuuliza, kazi ambazo matokeo yake ndio yanazua maswali kwako, wewe ni kiongozi usiyejielewa, usiyejua muelekeo wako, wala usiyejua muelekeo wa wale unaowaongoza.

Haya ni matokeo ya kufuata ushauri/mawazo ya mjinga aliyefeli, kinachotokea sasa ni ule ujinga wa yule aliyefeli mwanzo uliobaki kichwani mwake, sasa ndio umepata muda wa kufanyiwa kazi kwa vitendo na mtawala mjinga asiyejielewa, wala asiyejua kuchambua mambo nyetu kwa akili zake.

Alichokifanya Samia ni sawa na kuambiwa amekanyaga uchafu unaotoa harufu mbaya, halafu anajibu nimeziba masikio siwasikii!.
 
Unajua ccm wanaspin kuwa watu hatutaki mkataba na dp, lakini ukiwauliza kuusu terms za mkataba ,wanakwambia dp Wana watoto wadogo wanabeba kontena kwa computer, ila terms za mkataba hawagusi

Ukiwambia mkataba huu Ni wa milele hauna ukomo , watakujibu bandarini Kuna wapigaji sana ,Kuna wezi kichizi,..wakati ccm ndio wamilki, wao ccm ndio wanapitisha vitu bila kulipa Kodi, pia wao ndio wezi wenyewe

Ukiwambia mkataba huu umeuza bandari zetu zote ,kuanzia za baharini, maziwani, mitoni, mabwawa mpaka kwenye vidimbwi ,watakujibu ticts imekaa miaka 20 lakini hawakufanya lolote, hao ticts walipewa bandari na chadema?

Ukiwambia mkataba huu umesainiwa na wazanzabar watatu , wanasheria mkuu hakuwepo, watakujibu nyie wabaguzi wa rangi, mnataka kuua muungano

Ukiwaambia mkataba wa IGA Ni wa nchi na nchi na sio wa nchi na Jimbo la Dubai au na kikampuni Cha dp, watakwambia nyie ndio wapigaji wenyewe pale bandarini ,sa watanganyika million 60 wote wameajiliwa bandarini?

Ifike mahali watanganyika tumkatae huyu mama
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom