Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 2,814
- 11,991
Mkutano wa kilele wa BRICS umeingia siku ya 3 huko Johanesburg, Afrika Kusini. Nchi wanachama zinapania kuimarisha ushawishi kuukabili muundo wa uchumi wa dunia unaoongozwa na nchi za Magharibi.
Viongozi wa muungano wa BRICSwamegeukia ajenda kuu ya mkutano wao, siku moja baada ya Rais wa Urusi Vladimir Putin kuzikosoa nchi za magharibi. Muungano huo unajadili uwezekano wa utanuzi na kuruhusu wanachama wapya wajiunge, ikiwa ni zaidi ya muongo mmoja tangu ulipoasisiwa.
Zaidi ya nchi 20 zimewasilisha rasmi maombi ya kutaka uanachama ikiwemo Saudi Arabia.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye mazungumzo na Rais wa China Mhe. Xi Jinping kando ya Mkutano wa BRICS unaofanyika Jijini Johannesburg nchini Afrika Kusini tarehe 24 Agosti, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akiwa pamoja na Wakuu wa nchi na Serikali kwenye Mkutano wa 15 wa BRICS unaofanyika Jijini Johannesburg nchini Afrika Kusini tarehe 24 Agosti, 2023.