Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 16,559
- 41,078
Katikati ya majonzi na masikitiko makubwa kutokana na baadhi ya watu wanafiki, waongo, wenye upeo na uwezo duni, wanaopigania matumbo yao; kuna faraja kubwa.
Sote tunajua wazi kuwa baadhi ya watu, ama kwa kusukumwa na tamaa ya kujinufaisha wao binafsi, au kwa kukosa maarifa na weledi, wameamua kuliangamiza Taifa.
Wataalam mbalimbali, wenye weledi na uelewa mkubwa lakini ambao hawajapungukiwa ukweli wa nafsi na mapenzi makubwa, wamechambua kwa kina, na kwa uwazi kabisa mkataba wa bandari, wakaainisha namna wenzetu wachache kutokana na tamaa zao, walivyolidhalilisha Taifa, kwanza kwa kukubali wageni ndio waliamlie Taifa. Watu hawa waovu, maadui wa Taifa letu, wamefanya yafuatayo (nayataja yale ya msingi tu, lakini TLS na wazazuoni wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam wameainisha yote kwa kina):
1) Wamekula njama na kukubaliana na DP kuwa DP iwe juu ya sheria na katiba ya nchi. Kwenye hili, wakati katiba yetu ya nchi inatamka wazi kuwa ardhi yote ya nchi ni mali ya umma wa Watanzania, na msimamizi wake ni Rais, wao wamekubaliana na DP kuwa sehemu yoyote ya ardhi maeneo ya bandari, na sehemu nyingine yoyote atakayoitaka DP, Serikali italazimika kuwaondoa wananchi, taasisi au makampuni, kutoka kwenye hiyo ardhi anayoitaka DP, na ardhi hiyo itamilikishwa kwa DP.
2) Wamekula njama na kukubaliana na DP kuwa DP atamilikishwa ardhi, kinyume na sheria za nchi. Sheria yetu ya ardhi hairuhusu mgeni kumiliki ardhi. Yeye anaruhusiwa kuitumia tu lakini siyo kumiliki. DP kwa kadiri ya IGA, ambayo haturuhusiwi kujitoa, atamilikishwa ardhi.
3) Wamekula njama na kukubaliana na DP kuwa watu watakaoondoshwa kwenye ardhi anayoitaka DP, serikali ndiyo iwalipe fidia. Hii ni kinyume kabisa na sheria yetu ya ardhi kuhusiana na fidia ya ardhi, ambayo inatamka wazi kabisa kuwa mtu, taasisi au kampuni yoyote itakayohitaji ardhi kwa matumizi yoyote yale, ndiyo itakayolazimika kulipa fidia. Lakini kwa DP, serikali itawaondosha watu na taasisi zake, halafu yenyewe ndiyo iwalipe fidia.
4) Wamekula njama na DP kuiondolea nchi heshima yake ya kuwa Taifa huru linaloweza kufanya maamuzi yoyote wakati wowote kwa maslahi ya Taifa kwa kuzingatia katiba na sheria ambazo imeziweka. Kwenye mkataba wa DP, hata kama tukiwapata wawekezaji wengine ambao labda tunaona wana tija kwa Taifa letu, hata kwenye bandari ambazo DP watakuwa hawajawekeza chochote, hatutaruhusiwa mpaka DP aridhie.
5) Wamekula njama na DP kuwezesha uporaji wa bandari ya Dar es Salaam. Sheria zetu za nchi zinatoa haki ya mtu kutambulika kwa mali yake. Na hiyo ndiyo inakupa haki ya kuiuza mali hiyo au hata kuitumia mali yako hiyo kuingia kwenye ubia. Wenzetu hawa, kwa ujambazi wa ajabu, licha ya matrilioni ambayo tumewekeza bandari ya Dar es Salaam na bandari nyingine, wameamua DP apewe bure. Hatutapewa fidia ya uwekezaji tuliofanya, wala uwekezaji tulioufanya hautupi hata ile haki ya kuwa wabia ili nasi tufaidike na faida itakayopatikana, kama ambavyo hawa hawa DP wamefanya huko Uingereza.
6) Wamekula njama na DP, kudharau kabisa sheria yetu ya kodi, na kukubaliana kuwa hizi kodi zetu ambazo zipo kwenye sheria yetu ya kodi, hazitamhusu DP. Yeye atapewa msamaha au kupunguziwa kiwango.
7) Wamekula njama na DP kuhakikisha uhuru wa Taifa unafungwa. Wamekubaliana na DP kuwa kwa mazingira yoyote yale, hata kama DP atakuwa amekiuka mkataba wowote ule kati ya hiyo mikataba midogo itakayofungwa, ni marufuku sisi kama Taifa, kuuvunja mkataba huu, mpaka yeye aridhie (kwa kutufanya wajinga, wameandika kuwa mpaka pande zote zikubaliane. Yaani hata ikitokea DP amefanya makosa, hatuwezi kumfukuza mpaka yeye akubali).
Haya ni machache, wenzetu hawa wasiolitakia mema Taifa letu, wameyafanya. Na vinara kwenye uovu huu, yupo:
Waziri Mbarawa
Majaliwa Majaliwa
Eliezer Feleshi
Tulia Ackson
Wabunge wa bunge batili, wakiongozwa na Musukuma
Mzee Malechela
Wziri Nape
Kwa upande mwingine, unaotia faraja, ni upande wa watu wenye hekima, wenye weledi na upeo, wakweli wa nafsi, wanaolipigania Taifa lao la leo na kesho, wanaoamini kuwa katiba, sheria, mamlaka na uhuru wa Taifa ni lazima vilindwe, vidumishwe na kupiganiwa wakati wote. Zipo taasisi imara, kama vile viongozi wa dini, chama cha wanasheria na wanasheria mbalimbali, wanazuoni wa chuo kikuu cha Dar es Salaam na watu mbalimbali, wamepaza sauti zao, na kuweka mwongozo wa wapi twende.
Wote wote wenye akili timamu, wanaoelewa, wenye uwezo wa kufundishika hata kama hawana elimu, wanatambua wazi jinsi mkataba kati ya Tanzania na DP World ulivyo wa hovyo na wa kishenzi, na jinsi unavyotweza utu wetu, utaifa wetu na Taifa letu kwa ujumla.
TLS imeuchambua kwa kina mkataba huo. Professor Shivji na wasomi wenzake wa UDSM, wameuchambua kwa kina mkataba huo. Wote wameorodhesha na kubainisha vifungu vyote vya hovyo, jinsi vinavyotubana, jinsi vinavyofuta haki za kikataba na za kisheria tulizoziweka, na namna mkataba huo ulivyo wa kinyonyaji na kutufanya kuwa ni watu tusiokuwa na akili hata ile ya kawaida. Wataalam hawa hawajaishia kuorodhesha tu vipengere vya hovyo, bali wameelezea madhara ya vipengere hivyo, na wametoa mapendekezo ya namna ya kuondoka mahali hapo.
Sasa ni maamuzi ya Rais Samia kuendelea na watu waovu, wanafiki, wanaompamba kwa rushwa ya sifa za kipuuzi, watu wanaopigania matumbo yao kufa na kupona, AU asimame na kuubali ushauri wa watu wenye mapenzi mema na Taifa letu, wenye upeo na uelewa mkubwa na walio wakweli wa nafsi.
Kwa upande mwingine, tunawaomba wote waliosimama kidete kutetea hadhi na rasilimali za Taifa letu, waandae mkutano wa pamoja, ili tutoke na azimio moja. Lakini kikubwa zaidi ni kukubaliana, nini kifanyike, kama waovu hawa wakaendelea na mipango yao ya uovu.
Taasisi hizi, na watu hawa hapa chini, mzidi kubarikiwa kwa dhamira yenu njema kwaajili ya kizazi hiki na wale watakaokuja huko mbeleni. Mungu wetu azidi kuwajalia ujasiri, kuwapeni ulinzi wa kutosha katika kazi hii takatifu mnayoitenda. Hawa hapa chini ni wachache niliowakumbuka. Ongezeni orodha yao.
Viongozi wa dini
Chama cha Wanasheria Nchini
Wanazuoni wa Chuo Kikuu Dare es Salaam
Jaji Stela Augustine
Dr. Wilbroad Slaa
Prof. Lipumba
Prof. Shivji
Prof. Tibaijuka
Wakili Alphonce Lusako
Mwanasheria Dr. Rugemeleza
Tundu Lisu
Freeman Mbowe
Na wengine wengi.