Rais Samia “amzawadia” Millioni 10 Askofu Ruwa’ichi Kwa kutambua mchango wake kwa Kanisa na Taifa

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Jul 28, 2022
17,757
11,996
Ndugu zangu Watanzania,

Rais wetu mpendwa na Jemedari wetu kipenzi cha watanzania Mheshimiwa Daktari Mama Samia Suluhu Hasssan mama wa shoka, chuma cha Reli, shujaa wa Afrika, jasiri muongoza njia, simba wa nyika, komandoo wa vita, nyota ya matumaini na nuru ya wanyonge amemzawadia kiasi cha shilingi Milioni 10 Askofu Ruwaichi wa kanisa katoliki Jimbo kuu la Dar es salaam.

Zawadi hiyo ni katika kutambua mchango wake kwa kanisa na Taifa letu kwa ujumla kupitia huduma na uongozi wake.ambapo ni yeye pia aliyeanzisha chuo kikuu cha Mtakatifu Agustino Mwanza pamoja na matawi yake mbalimbali kama vile Mtwara,moshi n.k.lakini pia katika utumishi wake akiwa askofu jimbo kuu la Dar ameweza kuanzisha parokia mbalimbali takribani 100.

Hayo yameelezwa na makamu wa Rais Mheshimiwa Dkt Philipo Isdori Mpango alipomwakilisha Mh Rais wetu kipenzi katika Misa ya Jubilee ya miaka 25 ya uaskofu wa Ruwaichi. Ambapo pamoja na mambo mengine makamu wa Rais amesisitiza Watanzania kuwa na mioyo ya shukurani na kusema asante. kumshukuru Mungu kwa kutupatia uhai na afya njema na hii pumzi tuliyonayo.

Rais wetu kipenzi Anaendelea kuonyesha namna alivyo Rais wa watu wote ,mwenye upendo kwa wote na mwenye kushirikiana vyema na viongozi wetu wa Dini na madhehebu yote. Rais wetu anatambua mchango wa viongozi wa Dini na nafasi yao katika Ustawi wa Taifa letu . ndio maana ya kuamua kumtuma kiongozi namba mbili baada yake kwenda kumuwakilisha.hii yote ni katika kuonyesha heshima na upendo wake mkubwa alio nao katika moyo na kifua chake kwa viongozi wetu wa Dini.

Ndio mama Mama yetu mpendwa amekuwa akishirikiana vyema sana na viongozi wetu hawa wakiroho katika masuala mbalimbali na kuwapa nafasi ya kuwasikiliza pale wanapokuwa na jambo ambalo wangependa kutoa maoni au mawazo yao, kama alivyofanya kwenye suala la uwekezaji bandarini jambo ambalo viongozi wetu walimuelewa vyema na kuondoa hofu waliyokuwa nayo awali na kuamua kumuunga mkono Rais wetu na serikali yake na dhamira yao njema iliyozingatia maslahi mapana kwa Taifa letu. Ambapo ndio maana Tunaendelea kuona amani na utulivu vikiendelea kutamalaki hapa nchini .

Huku umoja na mshikamano ukiendelea kuwa imara miongoni mwa Watanzania ,tukiishi kwa pamoja na kuzungumza lugha moja pasipo kubaguana kwa misingi ya Dini zetu au makabila yetu au jinsia zetu au ukanda tunaotokea.tumebakia kama Taifa moja lililoungana vyema na kushikamana.

Naweka kalamu yangu chini na kuishia hapa. Chanzo cha habari yangu ni Gazeti la Mwananchi la kiswahili. Kama unataka kupata na mengine mengi juu ya habari hii basi nenda kwenye chanzo hicho cha habari hii.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa. Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
 
Mama anahangaika kugawa hela na Kuna wanafunzi wamezuiliwa kufanya mtihani kisa ada.. wanategemea boom muda huo huo mama anamwaga hela
Kama unawafahamu hao wanafunzi kwanini hujawasaidia? Au wewe kazi yako ni kupiga umbea na kuzusha uongo na fitina? Kwa hiyo ulitaka asitoe? Kwani wewe umesaidia wangapi hapo ulipo?
 
Kama unawafahamu hao wanafunzi kwanini hujawasaidia? Au wewe kazi yao ni kupiga umbea na kuzusha uongo na fitina? Kwa hiyo ulitaka asitoe? Kwani wewe umesaidia wangapi hapo ulipo?
Uongo na fitina kwenye dunia ya uwazi? Ningewasaidia ila Kuna taasisi maalum imewekwa kwaajili yao (HESLB). Mpunguze sifa za kijinga
 
Back
Top Bottom