GE2025 Rais Samia amuondolea hadhi ya Ubalozi Ndg Humphrey Polepole

GE2025 Rais Samia amuondolea hadhi ya Ubalozi Ndg Humphrey Polepole

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Ndo hapo sasa, polepole hakuomba kujiuzulu Bali alitoa statement kua kajiuzulu


Unaweza kuomba ku resign boss akakusihi uendelee, naskia Mzee wetu lowassa ndo aliingizwa kingi hivi kua aombe ku resign then mkwere amsihi kuendelea, iwe kama political move kuonyesha uwajibikaji, wajanja wa mjini wakamseti then wakamla kichwa
EL amepitia mengi, apumzike salama yule mzee.
Nilikua nampenda mie, daaah
 
Hiyo hadhi ya ubalozi ukiwa nayo unapata faida gani na ukiikosa unapata faida gani ?


Au na mabolozi hulipwa marupurupu mpaka wanakufa ?
1. Upatikanaji wa huduma za kipekee kwenye viwanja vya ndege (kama chumba cha VIP)

2. Uwezo wa kuhudhuria hafla za kimataifa bila vizuizi

3. Uungwaji mkono wa kisheria na ulinzi wa kimataifa

4. Fursa za mitandao ya kijamii na kitaaluma na viongozi wengine

5. Uwezo wa kuwakilisha maslahi ya taifa au taasisi kimataifa

6. Upatikanaji wa taarifa za siri au za kipekee (kulingana na makubaliano)

7. Uzoefu wa kujadili na kusuluhisha migogoro ya kimataifa

8. Kuimarisha uhusiano wa kibinafsi na kitaaluma na wawakilishi wa nchi zingine

9. Kinga ya kidiplomasia

10. Msamaha wa kodi na ushuru

11. Ustawi wa kifedha

12. Uwezo wa kushawishi kimataifa

13. Fursa za ushauri na kazi za kujitegemea

14. Heshima na hadhi ya kijamii

15. Uwezo wa kufanya kazi katika mazingira ya kimataifa

16. Uzoefu wa kuongoza na kushirikiana na mataifa
 
Ndo hapo sasa, polepole hakuomba kujiuzulu Bali alitoa statement kua kajiuzulu


Unaweza kuomba ku resign boss akakusihi uendelee, naskia Mzee wetu lowassa ndo aliingizwa kingi hivi kua aombe ku resign then mkwere amsihi kuendelea, iwe kama political move kuonyesha uwajibikaji, wajanja wa mjini wakamseti then wakamla kichwa
Mkuu ni procedure tu hizo; kujiuzulu ubalozi haiondoi haki na hadhi za kibalozi hadi pale unapoondolewa hadhi hiyo na aliyekuteua.
 
Not pathetic ni kawaida kwani asipofanya hivyo ataidai hiyo status popote atakapoenda,kwa sasa hataweza kuitimia diplomatic passport aliyonayo na privileges zake zote
Sahihi kabisa, wabongo hatuna tabia ya kujifunza kanuni mbalimbali. Tunajua kushambulia tu. Hata kwenye mechi kuna muda udefend au uchezee mpira ili kusoma mchezo
 
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki imethibitisha kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, ametengua uteuzi wa Balozi Hamphrey Polepole, aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Cuba, na kumwondolea rasmi hadhi ya ubalozi.

Taarifa hiyo imetolewa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dk. Samwel Shelukindo, kufuatia barua rasmi iliyopokelewa kutoka kwa Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Dk. Moses Kusiluka.

Kwa mujibu wa barua hiyo, Rais Samia, kwa kutumia mamlaka aliyopewa chini ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kwa mujibu wa sheria ya utumishi wa umma, amechukua hatua mbili kuu dhidi ya Polepole Kutengua uteuzi wake kama Balozi wa Tanzania nchini Cuba, Kumuachisha kazi rasmi kwa manufaa ya umma

Taarifa hiyo imeeleza kwamba, hatua hizo zimeanza kutekelezwa rasmi kuanzia tarehe 16 Julai 2025.

Hamphrey Polepole, ambaye aliwahi kushika nyadhifa mbalimbali za juu serikalini na ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), alikuwa amepelekwa kuiwakilisha Tanzania nchini Cuba kama balozi, nafasi aliyoshika hadi uteuzi wake ulipotenguliwa.

Wizara ya Mambo ya Nje imeeleza kuwa hatua nyingine za kiutumishi na kidiplomasia kuhusu nafasi hiyo zitatolewa kwa wakati muafaka, kadri taratibu za uteuzi mpya zitakavyokamilika.
 
Mkuu ni procedure tu hizo; kujiuzulu ubalozi haiondoi haki na hadhi za kibalozi hadi pale unapoondolewa hadhi hiyo na aliyekuteua.
Kwaiyo Polepole alikuwa anamuakilisha Sir mia binafsi au Taifa?

Kuuliza swali hili lengo langu kuona jinsi gani yule namba 1 moja anatumia vibaya madaraka.
 
Back
Top Bottom