Rais Samia afunga mjadala wa machinga; ataka wapangwe vyema bila uonevu

Ila mbona makusanyo yameongezeka? Mwezi uliopita makusanyo yalikuwa trillion 1.6.

Kipindi Cha kikwete ambapo machinga hao unaowasema hawakuwepo lakini makusanyo kwa mwezi ilikuwa bil 800
Unalinganisha billion 800 ya mwaka 2012 ?

Na kuilinganisha na uchumi wa Sasa

Angalia Kwanza exchange ya dollar kipindi kile na sasa
 
Hujamuelewa Mh Rais.

Kasema waondolewe kwa utaratibu bila kelele na vurugu.

Hiyo ni Go ahead ya Wamachinha kuondolewa. Hiyo kinga hakuna tena ya kutoguswa.
Na wewe hujaelewa, maana yake machinga wabaki lakini wasizibe maduka lakini pia watoe mwanya basi waenda kwa miguu nao weweze kupita yaani wapangwe vizuri sio kufunga njia kabisa kabisa., machinga hawezi ondoka mjini pigaua
 
Na wewe hujaelewa, maana yake machinga wabaki lakini wasizibe maduka lakini pia watoe mwanya basi waenda kwa miguu nao weweze kupita yaani wapangwe vizuri sio kufunga njia kabisa kabisa., machinga hawezi ondoka mjini pigaua

Mama yuko njema,,,anasitahili tuzo ya
 
Kama kweli tuko makini na kwa dhati kabisa katika kuweka miji na majiji yetu yawe Safi na kuongeza mapato inabidi uamuzi mgumu tu, machinga na biashara holela zitolewe mijini yaani kila kitu kiwe Kama kilivyopangiliwa ie maeneo ya barabara,maeneo ya wazi, kuondoa vibanda vilivyowekwa kiholela maana kuruhusu biashara/machinga katikati ya mjini ni sawa na kutema banzoka kwa tukaranga twakuonja Tanzania uchumi wetu unajengwa na wakulima sio wamachinga na wachuuzi wa bidhaa toka China kwanza ndio wanaodhoofisha viwanda vidogovidogo vya ndani
 
Walipewa masoko yaliyojengwa na mradi wa kuboresha manispaa DMP na wameyatelekeza. Mbagala waliambiwa wawapishe wajenzi wa barabara, wamegoma kuondoka na kusababisha usumbufu kwa wajenzi kwa kutupa taka wanamojenga na kukanyaga lami mbichi. Mmachina ni sawa na wale ndege wanaokaa migongoni mwa wanyama mbugani.
Jamaa wanapenda mchekea wafanye biashara sehemu zinazolipa lakini hawataki kutozwa gharama zinazoendana na eneo husika wakiguswa wanasema wanaonewa.
 
Wanaondolewa wanapelekwa wapi?
Watu hawana ajira wala kipato cha ziada. Waache wafunge barabara ndio tuelewane.
Nafikiri serikali sasa ijikite kuanzisha miradi yenye tija ili kiongezea ajira.
Gas na madini ni eneo pana litakalosaidia sana. Mbona kama hatuoni haja ya kufanya hivyo haraka?
 
Niliandika tarehe 13/09/2021 nayo itapita wamachinga watakuwapo, Leo tarehe 13/09/2021 Rais akiongelea kuhusu wamachinga alisema hataki kuona nguvu yoyote ikitumika kuwaondoa wamachinga, kauri hii ya Rais ni muendelezo wa kuwajengea kiburi wamachinga.

Nilisema jukumu la kuwaondoa ni la Rais tu mkuu wa mkoa hana ubavu wa kuwaondoa wanyonge wapigakura wa Rais.

Je, viongozi wengine wanasababu ya kuwapa muda wa kuondoka sehemu wasizositahili?

Hapa, wawaache tu.


----Zaidi soma--

Rais Samia Suluhu amesema haya...

Najua kwamba Serikali tumetoa fursa kubwa kwa machinga kufanya biashara zao ili kujiingizia vipato vyao. Wakuu wa Mikoa na Wilaya wanawapanga lakini imefika wakati wameenea kila mahali, mpaka kwenye maduka wao wanaziba na wenye maduka hawauzi wanauza wao mbele.

Sasa baadhi ya wenye maduka wamepata mtindo wa kutoa bidhaa ndani na kuwapa wamachinga kuuza, tendo hili linatukosesha kodi kwa sababu machinga halipi kodi. Nitoe wito kwa wakuu wa mikoa, muwapange vyema machinga bila kuleta vurugu, fujo na uonevu

Niwaombe ndugu zangu machinga nanyi mkafuate sheria. Ndugu zangu mlioapa leo na wengine mliopo na kwingine, mwende mkachape kazi, nami nikitoka hapa nakwenda kuchapa kazi, naenda kuchapa kazi ya marekebisho.


Hapa kasema Waondolewe, Period
 
Hujamuelewa Mh Rais.

Kasema waondolewe kwa utaratibu bila kelele na vurugu
Yaani unategemea "waondoke bila kelele", wakati ndio ofisi na maisha yao yapo hapo. Ngoja tuone muujiza wa machinga kuondoka "bila kelele na vurugu"
 
Hujamuelewa Mh Rais.

Kasema waondolewe kwa utaratibu bila kelele na vurugu.

Hiyo ni Go ahead ya Wamachinha kuondolewa. Hiyo kinga hakuna tena ya kutoguswa.
Hata mimi kauli ya Mh Rais nimeitafsiri hivi mkuu, binafsi nimeona katoa green light waondolowe.
 
Na wewe hujaelewa, maana yake machinga wabaki lakini wasizibe maduka lakini pia watoe mwanya basi waenda kwa miguu nao weweze kupita yaani wapangwe vizuri sio kufunga njia kabisa kabisa., machinga hawezi ondoka mjini pigaua
Kuondolewa baadhi yao ni lazima maana kama hilo unalosema lingewezekana hata sasa ingekuwa hivyo lakini kwa wingi wao wa sasa haiwezekani jamaa kupangwa na wakatosha hivyo lazima wengine wapungue.
 
Back
Top Bottom