Rais Samia afunga mjadala wa machinga; ataka wapangwe vyema bila uonevu

Niliandika tarehe 13/09/2021 nayo itapita wamachinga watakuwapo, Leo tarehe 13/09/2021 Rais akiongelea kuhusu wamachinga alisema hataki kuona nguvu yoyote ikitumika kuwaondoa wamachinga, kauli hii ya Rais ni muendelezo wa kuwajengea kiburi wamachinga.

Nilisema jukumu la kuwaondoa ni la Rais tu mkuu wa mkoa hana ubavu wa kuwaondoa wanyonge wapigakura wa Rais.

Je, viongozi wengine wanasababu ya kuwapa muda wa kuondoka sehemu wasizositahili?

Hapa, wawaache tu.


----Zaidi soma--

Rais Samia Suluhu amesema haya...

Najua kwamba Serikali tumetoa fursa kubwa kwa machinga kufanya biashara zao ili kujiingizia vipato vyao. Wakuu wa Mikoa na Wilaya wanawapanga lakini imefika wakati wameenea kila mahali, mpaka kwenye maduka wao wanaziba na wenye maduka hawauzi wanauza wao mbele.

Sasa baadhi ya wenye maduka wamepata mtindo wa kutoa bidhaa ndani na kuwapa wamachinga kuuza, tendo hili linatukosesha kodi kwa sababu machinga halipi kodi. Nitoe wito kwa wakuu wa mikoa, muwapange vyema machinga bila kuleta vurugu, fujo na uonevu

Niwaombe ndugu zangu machinga nanyi mkafuate sheria. Ndugu zangu mlioapa leo na wengine mliopo na kwingine, mwende mkachape kazi, nami nikitoka hapa nakwenda kuchapa kazi, naenda kuchapa kazi ya marekebisho.


Wamachinga huwezi kuwaondoa hata Mara moja ukitaka kuleta vurugu za kutisha waondoe wamachinga mitaani
 
Unadhani mko wangapi? Nyie ni tone la maji kwenye bahari.
20210913_165441.jpg
 
Machinga hawezi ondoka maeneo yao kwa maneno matupu.Bila Rungu Wamachinga hawataondoka.Rais kauli zake hazieleweki
 
Machinga ataondoka Bila kukung'utwa Rungu?
Hiyo sasa kazi kwao maana wanachokitaka wao hakiwezekani,hakuna mahali mtu unaweza kufanya shughuli zako mahali kokote tu tena bila utaratibu kwa kisingizio cha unyonge kwani kama ni unyonge ni umaskini basi kuna masikini kuliko wao.
 
Kuwe na Meza nzuri sio kila mmoja aweke uchafu wake, pia waache nafasi kwa wapita njia.
Maajabu niliyakuta stendi ya sabasaba Dodoma, bidhaa wanaweka chini mabasi yanafanya kukwepa mmchinga aliyeweka bidhaa chini
 
Raisi Samia kauli zake zinatanabaisha jinsi gani alivyo dhaifu.

Hii kauli imebeba ukike zaidi kuliko kimamlaka.

Hii imekaa kama ya mama wa nyumbani anayejaribu kuamulia ugomvi wa wanae wanaogombania vitumbua

Rais Samia anataka kuwatumikia mabwana wawili kwa wakati mmoja.

Hii ni alama kuwa Tanzania bado tuna ombwe la kiuongozi......kutoka kwa mwendazake mpaka Samia....bado tupo gizani.
 
Kiukweli sekta ya wamachinga ndio yenye watu wengi zaidi kwa sasa hapa nchini na hakuna namna utaweza kuwahamisha maana ukiwapeleka Brundi watajaza nchi ile yote.

Rais Samia yuko sahihi kabisa kwamba hawa wamachinga wawekewe utaratibu mzuri wa kufanya biashara zao.

Mungu ni mwema wakati wote!
 
Kiukweli sekta ya wamachinga ndio yenye watu wengi zaidi kwa sasa hapa nchini na hakuna namna utaweza kuwahamisha maana ukiwapeleka Brundi watajaza nchi ile yote...
Mkuu sekta yenye watu wengi ni kilimo (wakulima na wafugaji), nguvu kubwa zielekezwe huko katika mnyororo mzima wa uzalishaji. Hii itasaidia kukuza uchumi, kuongeza ajira na kupunguza hao machinga
 
Niliandika tarehe 13/09/2021 nayo itapita wamachinga watakuwapo, Leo tarehe 13/09/2021 Rais akiongelea kuhusu wamachinga alisema hataki kuona nguvu yoyote ikitumika kuwaondoa wamachinga, kauli hii ya Rais ni muendelezo wa kuwajengea kiburi wamachinga...
Samia anawaonfoa wamachinga kwa staha na ustaarabu,na ujue anaposema wakuu wa mikia na wilaya wawapange ujue tayari kila kitu kimepangwa na kinafuata ni utekelezaji tu

Sent from my SM-N960F using JamiiForums mobile app
 
Kiukweli sekta ya wamachinga ndio yenye watu wengi zaidi kwa sasa hapa nchini na hakuna namna utaweza kuwahamisha maana ukiwapeleka Brundi watajaza nchi ile yote...
Hauwezi kuwawekea utaratibu (hewa) bila kuwagusa, yeye Rais anatakiwa awaambie ni utaratibu huu ndio ninautaka, fullstop.
 
Back
Top Bottom