Rais Samia afunga mjadala wa machinga; ataka wapangwe vyema bila uonevu

elvischirwa

JF-Expert Member
Jan 26, 2013
10,080
2,000
Niliandika tarehe 13/09/2021 nayo itapita wamachinga watakuwapo, Leo tarehe 13/09/2021 Rais akiongelea kuhusu wamachinga alisema hataki kuona nguvu yoyote ikitumika kuwaondoa wamachinga, kauli hii ya Rais ni muendelezo wa kuwajengea kiburi wamachinga.

Nilisema jukumu la kuwaondoa ni la Rais tu mkuu wa mkoa hana ubavu wa kuwaondoa wanyonge wapigakura wa Rais.

Je, viongozi wengine wanasababu ya kuwapa muda wa kuondoka sehemu wasizositahili?

Hapa, wawaache tu.

----Zaidi soma--

Rais Samia Suluhu amesema haya...

Najua kwamba Serikali tumetoa fursa kubwa kwa machinga kufanya biashara zao ili kujiingizia vipato vyao. Wakuu wa Mikoa na Wilaya wanawapanga lakini imefika wakati wameenea kila mahali, mpaka kwenye maduka wao wanaziba na wenye maduka hawauzi wanauza wao mbele.

Sasa baadhi ya wenye maduka wamepata mtindo wa kutoa bidhaa ndani na kuwapa wamachinga kuuza, tendo hili linatukosesha kodi kwa sababu machinga halipi kodi. Nitoe wito kwa wakuu wa mikoa, muwapange vyema machinga bila kuleta vurugu, fujo na uonevu

Niwaombe ndugu zangu machinga nanyi mkafuate sheria. Ndugu zangu mlioapa leo na wengine mliopo na kwingine, mwende mkachape kazi, nami nikitoka hapa nakwenda kuchapa kazi, naenda kuchapa kazi ya marekebisho.

machinga.jpg
 
njoo kwetu

JF-Expert Member
Jan 11, 2016
736
1,000
Tunakosa kodi kwa sabbu ya kutaka kura 2025. Haya ni matatizo mengi ya kiafrica

Wafanya biashara siku hzi hawauzi bidhaa zao kwenye maduka. Maduka yanakuwa kama store room.

Unakuta mfanya biashara anawatenda wamachinga wamuuzie vitu vyao. Bila kulipa kodi yoyote.

Unakuta kodi ya huyo mfanyabiashara labda ni mil5 kwa mwaka. Ila hapo analipa elf 20.. Kwa mwaka mzima.

Niliandika tarehe 13/09/2021 nayo itapita wamachinga wstakuwapo, Leo tarehe 13/09/2021 Rais akiongelea kuhusu wamachinga alisema hataki kuona nguvu yoyote ikitumika kuwaondoa wamachinga.
 
Countrywide

JF-Expert Member
Mar 2, 2015
8,046
2,000
Tunakosa kodi kwa sabbu ya kutaka kura 2025... Haya ni matatizo mengi ya kiafrica...

Wafanya biashara siku hzi hawauzi bidhaa zao kwenye maduka.. Maduka yanakuwa kama store room.
Ila mbona makusanyo yameongezeka? Mwezi uliopita makusanyo yalikuwa trillion 1.6.

Kipindi Cha kikwete ambapo machinga hao unaowasema hawakuwepo lakini makusanyo kwa mwezi ilikuwa bil 800
 
May Day

JF-Expert Member
May 18, 2018
4,670
2,000
Machinga wapangwe vizuri sio kwa kuwa tu Raisi kasema hivyo basi Watendaji nao wasuse.

Na ikiwezekana Mh Raisi awape kipimo Watu wake kuhakikisha Watu wanapangwa vizuri na kuhakikisha hapo walipo sasa hawaongezeki tena...Waliopo wandikishwe watambulike kwa kupewa vile vitambulisho vyao wachangie mapato.

Yote haya yanawaezekana kupitia Viongozi wenye vision na busara.
 
elvischirwa

JF-Expert Member
Jan 26, 2013
10,080
2,000
Hujamuelewa Mh Rais.

Kasema waondolewe kwa utaratibu bila kelele na vurugu.

Hiyo ni Go ahead ya Wamachinha kuondolewa. Hiyo kinga hakuna tena ya kutoguswa.
Mmachinga apewe sehemu anayoitaka yeye, ipi hiyo! Wamepewa masoko wameyakataa, kila wapopewa hawataki wao wanataka katikati ya barabara.

Dumila Morogoro wamachinga walikuwa wanafukuzana na magari, wakajengewa banda zuri lenye choo kando ya barabara,

wakalitelekeza wakaendelea kukimbizana na magari! Hao ndio wamachinga wajukuu wa bibi.
 
Nipo huru

JF-Expert Member
Jul 20, 2021
854
1,000
Niliandika tarehe 13/09/2021 nayo itapita wamachinga wstakuwapo, Leo tarehe 13/09/2021 Rais akiongelea kuhusu wamachinga alisema hataki kuona nguvu yoyote ikitumika kuwaondoa wamachinga, kauri hii ya Rais ni muendelezo wa kuwajengea kiburi wamachinga.

Nilisema jukumu la kuwaondoa ni la Rais tu mkuu wa mkoa hana ubavu wa kuwaondoa wanyonge wapigakura wa Rais.

Je, viongozi wengine wanasababu ya kuwapa muda wa kuondoka sehemu wasizositahili?

Hapa, wawaache tu.
Hujamuelewa, kasema wanatakiwa wapangiwe maeneo rasmi sio kuzagaa ovyo lakini akataka zoezi hilo lisifanyike kwa vurugu na kuumizana.
 
Countrywide

JF-Expert Member
Mar 2, 2015
8,046
2,000
Machinga wapangwe vizuri sio kwa kuwa tu Raisi kasema hivyo basi Watendaji nao wasuse.

Na ikiwezekana Mh Raisi awape kipimo Watu wake kuhakikisha Watu wanapangwa vizuri na kuhakikisha hapo walipo sasa hawaongezeki tena...Waliopo wandikishwe watambulike kwa kupewa vile vitambulisho vyao wachangie mapato.

Yote haya yanawaezekana kupitia Viongozi wenye vision na busara.
Kupangwa vizuri ndio kuwapanga vipi.
 
Root

JF-Expert Member
Jan 23, 2012
40,466
2,000
Machinga wapangwe vizuri sio kwa kuwa tu Raisi kasema hivyo basi Watendaji nao wasuse.

Na ikiwezekana Mh Raisi awape kipimo Watu wake kuhakikisha Watu wanapangwa vizuri na kuhakikisha hapo walipo sasa hawaongezeki tena...Waliopo wandikishwe watambulike kwa kupewa vile vitambulisho vyao wachangie mapato.

Yote haya yanawaezekana kupitia Viongozi wenye vision na busara.
Machinga wasikae kwenye maduka ya watu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
elvischirwa

JF-Expert Member
Jan 26, 2013
10,080
2,000
Hujamuelewa, kasema wanatakiwa wapangiwe maeneo rasmi sio kuzagaa ovyo lakini akataka zoezi hilo lisifanyike kwa vurugu na kuumizana.
Walipewa masoko yaliyojengwa na mradi wa kuboresha manispaa DMP na wameyatelekeza. Mbagala waliambiwa wawapishe wajenzi wa barabara, wamegoma kuondoka na kusababisha usumbufu kwa wajenzi kwa kutupa taka wanamojenga na kukanyaga lami mbichi. Mmachina ni sawa na wale ndege wanaokaa migongoni mwa wanyama mbugani.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom