Juzi tumemsikia Raila Odinga akisema rais Samia alikwenda Nairobi kwa lengo la kuwapatanisha Raila na Odinga katika tafrani zao za kisiasa.
Sisi watanzania tunajiuliza inakuwaje rais wetu kwenda nchi nyingine kufanya jambo la kisiasa mathalani kufanya upatanishi kimyakimya?
Kwani kulikuwa na haja gani ya kuficha jambo kama hilo ilhali halina athari kwa usalama kwake au kwa nchi? Mbona Odinga ameliweka wazi jambo hilo?
Tumeona pia rais wetu akifanya makubaliano makubwa kabisa na Dubai kuhusu bandari yetu. Mkataba huo haukujulikana hata na watu muhimu serikalini hadi mzalendo mmoja alipouvujisha!
Je, ni mambo mangapi yanafanywa kimyakimya na rais na serikali yake pengine bila ya kuwa na faida zozote kwa watanzania?
Kwa mfano ndege yetu uliyokuwa imekamatwa Uholanzi iliachiliwa mwezi uliopita lakini hatukuambiwa nchi imelipa kiasi gani.
Tafadhali Rais Samia acha usiri katika mambo ambayo taifa linapaswa kufahamu.