Rais Samia aagiza wote waliotajwa kwa wizi wa Fedha za Umma kwenye Ripoti ya CAG washughulikiwe

Kulikuwa na haja gani kutoa tamko hadharani?

Ripoti imewaweka wazi, yeye kama Rais angewaita kama wakuu ama wa Takukuru au Polisi, kuanza kushughulika na ukamatwaji wa wahusika...
Political milage
 
Tatizo ninaloliona hapa ni kwamba kwenye hiyo speech alitakiwa aamuru hao woootee walioko kwenye ripoti ya CAG wakamatwe kwa sababu nina uhakika hawatachukuliwa hatua na hivyo vyombo maana wanalindana. Kwenye eneo hili JPM alifanikiwa, alikuwa hacheleweshi kutoa amri watu wanadakwa fasta.
Kwenye wezi Magufuli alikuwa hafikirii mara mbili wakina Singa na Rugemalila walidakwa kama vifaranga tu, ila kwa kuwa ashatoa tamko tutegemee kamatakamata kabla ya mwaka huu kuisha.
 
Mbowe so mlimfunga enzi za JPM thou mahakama ya rufaa ikagundua hakua na hatia!! Ila majitu kma chenge na yule Vice chairman wa ACACIA waliotupa hasara ya matrillion hta kamati ya maadili tu ya CCM hawakuitwa; in fact mmoja kapewa ubunge na mwingine alipewa uenyekiti wa bunge.

Alafu mtu anakuja hapa eti JPM alikua chuma??
 
Kufa ni ibada na kila mtu atakufa siku yake ikifika....ikiwemo wewe, utakufa tu siku ikifika..
Haya mkuu lkn tusiweke dhana ktk mambo ambayo hayana uhalisia. Namaanisha kuwa tusiamini kuwa mzee wa Lupaso ndio kaingilia kati kesi ya faili la mwenzake, wakati na yeye inasemekana alikuwa na la kwake linalohusu migodi ya dhahabu kule...
 
Rais Samia amesema haya...

Mkurugenzi wa TPA, Waziri na TAKUKURU mpo, naamrisha ripoti ya CAG mkaisome, halafu mchukue hatua, fedha nyingi sana imepotea watu tunachekeana tu, na bado waliotajwa kwenye ripoti bado wapo maofisini wanaendeleza wizi,"-



Tanzania sasa kumekucha,Moto unawaka, Wale wote waliokuwa wanamchukulia Mama poa sasa moto umewaka kwa ghafla,

Sasa kama ulitajwa na CAG umetafuna cha Umma kaa mguu sawa, Tutaelewana tu ngoja tuone,

Ushauri wangu nyie wenye dhamana acheni kugusa pesa ya Umma huyu mama sio Hayati Dkt John John Joseph Pombe Magufuli aliyewachekea,
Magufuli aliweka mtu wake bandarini,

Samia ana kazi kubwa yakupambana na mafisadi walioachwa na marehemu
 
Mnapenda sana kum overrate JPM ila jiulize Makonda na Sabaya wakati wanafanya madudu alikua haoni? Lugola na Nchambi walifungwa? Vipi waliobeba pesa za ESCROW Kwenye masandarusi wapo jela gani? Walioingiza serikali hasara ya matrillion kwenye Tanzanite na dhahabu wapo jela gani? In fact si alimpa ubunge wa makambako?

JPM alikamata watendaji tu ila hakugusa wanasiasa, otherwise kamati Kuu nzima ya CCM wangekua jela sahivi.
Inaelekea kazi inaanza, tusubiri tuone, Karma at work !!
 
Safi mama wanyooshe mafisadi wote wanaotaka kukuangushia jumba bovu wakati ufisadi wao ulikuwa awamu ilopita
 
Awamu iliyopita imezalisha mafisadi wengi sana wamechezea sana fedha za umma kwa kuficha na kuvitisha vyombo vya habari kutotangaza maovu yaliyokuwa yanatendeka. Sasa moto huo unawaka. Mjitathimini.
Mbona mnaongea matatizo ya Tanzania kama yalianza 2015? Unafiki mkubwa sana. Awamu gani ambayo haina mafisadi na wezi? Wale kina Idd Simba walikuwa awamu gani?
 
anaweza? hili sio suala la masikhara...asipepese macho akiletewa mafaili..haya mafaili yanamajina ambayo lazima usiku ukose usingizi..

vijana walimpima JPM walipompa faili fulani, naye akasema apigwe pingu tu hakuna namna dah wale vijana wakaona hiki kweli chuma ikabidi Mzee wa Lupaso aokoe jahazi, dah sijui ingekuaje leo hii japo naamini ungekuwa ndio mwanzo wa Tanzania waitakao wengi...ile movie mzee wa Lupaso angeicha tu mwisho wake..
Kwahiyo mzee wa lupaso asingeingilia Kati mzee wa remote angekula pingu?
 
Umesikia awamu ya tano imetajwa ama umehemukwa!!
umepatwa na mhaho!
Mungu wetu alikuwa mkubwa kuliko Mungu wa Chato ambae alikuwa amejaa kibri pamoja na ulevi wa madaraka.
pB.jpg
 
Back
Top Bottom