Rais saidia Mwanza MWAUWASA maji kutoka TZS 700 hadi 1220TZ kwa unit moja

Acha hadithi za abunuasi. Unakurupuka leo kupost kitu ambacho tunajua Mwauwasa kabla ya kupandisha bei waliruhusiwa na Ewura. Walipoita wadau kuja GoldCrest kutoa maoni yao ulikuwa wapi? Ulisubiri ili baadae ujifiche nyuma ya keyboard uanze kulalamika?
Gharama lazima zipande with time. Cum 1 kuinunua kwa bei hiyo ni fair tu. Mamlaka zinaotoza 1,800 mbona wateja hawajaandamana. Weka constraints zote kama zamani(constant) alafu bei ikipanda utaruhusiwa kuropoka.
Twende mbele turudi nyuma, hilo ongezeko litamtokea mtu puani kampeni za uchaguzi ujao, mtaani kwetu mambomba mengi yamefungwa wameshindwa kulipa bili ya August ambayo wengi imerange elfu 50 mpaka 80 kwa matumizi ya kawaida, hata mimi niliona ni maajabu, swala lakwenda Goldcrest sio kila mtu anaweza ndio maana tukawachagua wawakilishi wetu ambao wanakula kila mwisho wa mwezi kwaajili ya kazi hizo "kutuwakilisha" cha pili Goldcrest sio accessible kwa all type of people, je Muwsa ipo mjini tu ? inamatawi maeneo kibao kama Buzuruga, mbona hawakwenda huko kuchukua maoni? Toka nimekaa maeneo yote ya Tanzania sijaona sehemu yenye gharama za juu za maji kama Mwanza, Cha ajabu kuna ziwa lenye fresh water lakini ukitembea km moja kwenda ndani Hakuna maji ya Muwsa kabisa (From Busisi to Usagara) hii HAIKUBALIKI...
 
Hii kauli ya ziwa liko mlangoni, kitengo cha huduma kwa wateja ati customer care wanakujibu kama lipo mlangoni si uchote ziwani hapo mlangoni kwako why use maji yetu, DAAAAAAA
Ni sawa tu hata hilo ni jibu pia (nothing good or bad but thinking makes it so )ila unadhani kama kuna uwekezaji huru na wa ushindani wenye huduma kama za maji umeme unadhani zingekuwa juu kiasi hicho tatizo wengi twadhani maji ni kuoga na kunywa tu tunasahau uwekeazji huo unatakiwa kuwa moja ya chachu ya kilimo cha umwagiliaji NK Mathalani kama mtu anatumia hata kulima kilimo kidogo cha umwagiliaji mchicha bei itakuwaje tujaribu kuona huduma hizi za maji na umeme zina athali ya moja kwa moja kwenye maisha yetu. wakati flani tabata maji ya kunywa yalikuwa yanaigarimu sana familia yangu kwani ilinilazimu kununua ya chupa hali haikuwa hivyowakati naishi msasani kwa sababu maji yalikuwa yakipatina kirahisi
 
sasa iwapo huduma zote tunalipia 100%, mwehu wewe kodi zetu ninin? mlipane mishahara basi

sekta za Maji na afya ni huduma Ila lazima uendelevu na kujiendesha uangaliwe.

Kama Maji Mwanza ni ghali hamia vijijini penye unafuu.

Mnapenda kulalama sana. Hiyo Bill ya mwezi haifikii bili yako ya siku ya bia.

Kuoga sio lazima ni hiari. Lipa ankara ya Maji la sivyo tunakukatia.
 
kama unataka hesabu za mapipa fanya mwenyewe, kwani mbona wao wanatuuzi kwa units na sio mapipa? hala iwe pipa au unit suala ni ongezeko la 75% kwa mwezi agosti somehow reversed from 100% kwa mwaezi julai.

Tuwe tunaelewana kwenye hoja ndio tuweke michango yetu

Mkuu ungeweka wazi kwanza hio unit 1ni sawa na pipa ngap za maji
 
Naandika kwa ufupi sana maana najua unavyombo vya kukupatia habari na taarifa za uhakika, mimii napiga filimbi tu.

(Matumizi ya kati ya 15-25 Units Julai 2019 maji yalipanda kwa 100% yaani kutoka 700 hadi 1400TZS kwa unit moja,Agosti 2019 maji yakashuka kidogo kutoka 1400 hadi 1220TZS kwa unit moja
Juni 2019 mali yakuwa 700TZs kwa unit moja

Kwa hiyo maji yamepanda kutoka 700 hadi 1220TZS sawa na 75% ongezeko la bei. hali ni kuhujumu kazi na jitihada za rais kuwakomboa wanyonge walau wamudu maji safi na salama. Mufumko wa bei huu ni kejeli kwa jitihada za serikali na fedheha kwa rais wetu.

Maji mwanza yako zero kilometer yaani ziwa Victoria. Kwa nini maji yapande bei kwa 75% au why mtu ama taasisi husika walipitishe ongezeko la 100% kiisha kushusha kidogo to 75%?

Mheshimiwa Rais nani katika mishahara wake ama biashara zake anapata ongezeko la 100% au 75%

Maisha lazima yawape wananchi uhueni sio kwa ongezeko hilo la 75% wakati nyongeza mara nyingi inapaswa kuwa 10%-0%.
Wizara naona wametutelekeza big times
Customer care ya Mwauwasa inakatia simu wateja kisa hawawezi kuelezea nini kimepandisha bei kwa asilimia 100 au hiyo 75 ya Agosti. Hii ni fedheha nyingine, Mnabadilishana simu wakati wa maongezi bila taarifa kwa mteja kama mnavyopandisha maji bila taarifa kwa mteja.

Unanza na Mwanamke unashangaa kawa Mwanaume, inadibi uanze upya na kasha simu inakatwa twaaaaa
Wizara naona wametutelekeza big times, RaiS tupia jicho lako, Tunajua haya mambo kwako ni within minutes tunapata majibu mwafaka.

Mzee wetu umekulia maisha kama yetu wengi hapa TZ maji ni uhai, kupandisha maji kwa namna hiyo ni kushawishi matumizi ya maji machafu na Ambayo sio salama hivyo kuhujumu jitihda zako za Kuongeza Madawa na Vifaa tiba,

Vituo vya Afya na Hospitali maana dawa zimeongezeka sasa kuna watu wanafanya jitihada ya kuonesha dawa hizo bado hazotoshi na ni jitihada mfu. Maana wagonjwa yakiongezeka ni wewe umejumlisha madawa wao wametoa hence zero workdone. Nawasilisha kwa unyenyekevu.


Dar kwa unit moja ni tshs. 1,615
Kwa maji ni ghali sana hii, maji ni uhai, nilidhani serikali ingefaa kwa namna yoyote ile, maji iwe bidhaa rahisi kabisa, kuliko chochote kile, serikali yetu sikivu wapunguzieni wananchi gharama hizi kubwa za maji, DAWASCO kwa mfano, kwa mwezi nyumba ndogo tu ya Room 3 ya mwananchi wa kawaida wanalipa 30,000 hadi 50,000 kwa mwezi, gharama hizi ni kubwa sana.. Maji hayapaswi kuwa ghali hivi, ni hatari kwa hali halisi ya maisha ya wananchi.. Just like umeme, uko juu sana kwa unit moja, nategemea Stigler's wakianza kuzalisha umeme ushuke bei, sbb umeme uko juu sana hapa Tanzania, hata Mh. Rais kalisemea hili kila siku akiongelea umeme.
 
Unadhani unasaidia viongozi ila unawapotosha sana, kwani aliyetuuzia 700TZS alikuwa mjinga?

Huyu hawezi kuwa baharia. Anapenda cha bure.
Kikombe cha chai hakifiki hata lita kinauzwa jero ila Maji ndoo sijui 40 anataka alipe 800??. Kuna uchakavu wa miundo mbinu ya Maji, tozo mbalimbali za sura n.k, kuyatreat hayo Maji, kulipa salary wataalum n.k.

Water table Mwanza iko juu, achimbe kisima chake.

Tuliyowapunguzia shuleni tukachukue kwenye maji. Tulia hivyo hivyo.
 
unajua dar maji yanatoka kilomita 100 hivi, na ni ya mto ambayo ni machafu sana, sasa mwanza 0kilomita maji masafi nya yawe salama, ambapo pia haifanyiki ndio maana unaambiwa chemsha maji kabla ya kunywa, so pamoja na dar kuwa bei ghali bado unaweza ukaona mwanza ni wizi mtupu. wizi sio hulka ya serikali ya awamu wa tano, wacha RAIS alitupie jicho

Dar kwa unit moja ni tshs. 1,615
Kwa maji ni ghali sana hii
 
inategemea maji unayapata wapi, kwani mbona tanga sementi sio sawa na Mwanza, kwani mbona Petroli DAR na TANGA autwara sio sawa na Mwanza vile wao bahari na bandari zipo hapo

1,200 kwa unit unapiga kelele hivi,je sisi tunaolipa sh 1,800 kwa unit tufanyeje?
 
unajua dar maji yanatoka kilomita 100 hivi, na ni ya mto ambayo ni machafu sana, sasa mwanza 0kilomita maji masafi nya yawe salama, ambapo pia haifanyiki ndio maana unaambiwa chemsha maji kabla ya kunywa, so pamoja na dar kuwa bei ghali bado unaweza ukaona mwanza ni wizi mtupu. wizi sio hulka ya serikali ya awamu wa tano, wacha RAIS alitupie jicho

Maji ya Dar yanatoka Ruvu, kama 50 km toka mjini kati hakuna sbb yoyote ile kuuza maji ghali hivi.. Atleast Dar wangeuza kwa unit tshs 900 hv au hata tshs 1,000 isizidi hapo..

Maji kuuzwa shs 1,600 ni ghali sana
 
dar kibaha maili moja ni 48Km, iwe ruvu ni 50, hapana kaka. Kuna picha ya ndege, kwa matiasi, mlandizi kongowe kabla hujafika ruvu na kabla hujafika ruvu mtoni

Maji ya Dar yanatoka Ruvu, kama 50 km toka mjini kati hakuna sbb yoyote ile kuuza maji ghali hivi.. Atleast Dar wangeuza kwa unit tshs 900 hv au hata tshs 1,000 isizidi hapo..

Maji kuuzwa shs 1,600 ni ghali sana
 
kama hakuna huduma za jamii tunapata kutoka kwa serikali walau kwa kiasi umeme unalipa 100% maji 100% afya Bima Barabara 100% uliza lita ya mafuta kuna kodi kiasi gani, JE hizo kodi ni za nini? VAT 18%, PAYE 30% , Stamp Duty, Excise Duty, Corporate tax 30%, withholding tax 10%, DSE hisa 5% etc

Hizo mamlaka za maji zinatakiwa zijitegemme kwa makusanyo yake yenyewe na vilevile nadhani wanatakiwa kutoa kiasi fulani kwenye mfuko mkuu wa taifa.Ila nadhani pia inachangiwa labda na gharama za uzalishaji madawa na mambo mengine. Tusilaumu tuu labda ni kuwauliza wahusika.
 
Back
Top Bottom