MWAUWASA mjitathmini sio lazima kutenguliwa ndipo muwajibike

Team JPM

JF-Expert Member
Nov 11, 2018
1,074
1,608
Ahsante JamiiForums kusaidia utatuzi wa kero ya maji Mwanza.

Kumekuwepo na kero kubwa ya maji katika jiji la Mwanza ingawa kuna ziwa kubwa lenye ujazo wa maji ya kutosha katika jiji hilo.

Wiki iliyopita paliandikwa makala hapa JamiiForums kulalamikia mgao wa maji usioeleweka.

Baada ya andiko hilo, aliibuka Afisa habari wa Mwauwasa na majibu yasiyorizisha lakini siku hiyo hiyo jioni, maeneo mengi jijini yalipata huduma ya maji. Kitendo hiki kinaashiria:

1. Uzembe wa mamlaka kutosimamia na kutekeleza wajibu wao barabara.

2. Hujuma ya mamlaka ili kuendesha biashara haramu ya maji, maana bei ya ndoo moja ya maji ilipabda kutoka sh 100 hadi 500.

3. Uchonganishi wa wananchi kwa chama tawala na serikali.

Jana Jumapili, waziri wa maji Mh. Aweso, ametengua uteuzi wa Mhandisi Leonard katika Nafasi ya Ukurugenzi wa MWAUWASA.

Anayekaimu nafasi hiyo na atakayeteuliwa, ajitahidi kuwasimamia watumishi wa MWAUWASA ili kutatua kero ya maji jijini Mwanza.

Ikumbukwe kwamba, MWAUWASA sawa na Mamlaka zingine za maji nchini, ni taasisi ambazo watumishi wake na viongozi wanalipwa mishahara Mikubwa na posho. Na Malipo yao hutegemea mauzo ya maji. WITO KWA WATUMISHI WOTE WA MWAUWASA MNAPOANZA WIKI MPYA BILA MKURUGENZI LEONARD.

"MKONO UNAOKULISHA, USIUKATE"
 
Back
Top Bottom