Rais neno lako halijatujenga

Rais neno lako halijatujenga

Lakini at least wanaonyesha wanajali kuliko nyie wasukuma mnaotegemea "kupasua kuku" kukabiliana na CORONA.
Nani anajua huu upepo unaovumia hadi Ikulu utaishia wapi?!
Tumeona Marekani Donald Trump, Uingereza Waziri Mkuu wao Boris Johnson na Prince Charles waliugua COVID 19 wakatibiwa na kupona, nyie hapa mmeshindwa kumfukiza Eng.Kijazi apone na nyungu zenu za akina Jafo.?!
Haya ngoja tuone kwani mmeanzisha sasa MAZOEZI YA VIFUA !!!!
Yani unaongea kama vile Magufuli ana dawa ila kakataa kukupa!

Kama unataka aseme kitu juu ya hayo mabarakoa, hajakukataza kuvaa.
 
Kipindi cha uchaguzi ningetegemea tumwone akimtegemea Mungu huyu huyu amsaidie kushinda pamoja na wabunge wake. Badala yake hakumtaja kabisa akamweka kando akatumia mabavu kuwanyanganya wananchi haki yao. Hapa ndipo tunapokwama kumwelewa mkuu anapomtaja tena Mungu ambaye alimtupa wakati wa uchaguzi. Bado tunasubiri Mungu wa kweli atufute machozi kwenye machungu ya uchaguzi uliopita. Viongozi wa dini wakimtaja Mungu tunaelewa ila huyu jamaa akimtaja nasikia kukereka sana.
 
Kila mmoja katika nafasi yake, japo kwa viwango tofauti, amewahi kufanya kosa.

Umadhubuti wa kiongozi haupo katika kutofanya kosa bali katika kutafuta suluhisho sahihi baada ya kufanya kosa.

Hatua ya kwanza ya kupata suluhisho sahihi la kosa, ni kukiri umefanya kosa. Mwalimu Nyerere aliwahi kusema,

"..... kukiri upungufu siyo kujidhalilisha bali ni kitendo cha kujiimarisha"

Rais Magufuli, ninaamini amefanya makosa mengi katika kukabiliana na corona. Lakini watanzania tulikuwa tayari kumsamehe maana corona imekuja kwa mara ya kwanza, na hakuna aliye na uzoefu wa kukabiliana nayo.

Mimi ni mmoja wa wahanga wa corona, mtoto wa kaka yangu katika umri wake wa ujana, amepoteza maisha ya Duniani, na kwa dalili alizopitia, tuna hakika ni corona. Lakini kuna rafiki yangu amepoteza ndugu zake 4 na marafiki wa familia 3. Leo baada ya Rais kumpoteza msaidizi wake wa karibu, kwa dalili zinazoonesha, kwa tatizo la corona, tulitarajia kupata neno la faraja kutoka kwa Rais.

Kuna mambo tuliyatarajia kutoka kwa Rais:

1) Watanzania wote kwa umoja wetu, kukiri kuwa tumepatwa na janga la corona

2) Kukiri kuwa hatujawa na jitihada za dhati kukabiliana na corona

3) Kukiri kuwa tumeishi kimbumbumbu bila hata ya kuwa na jitihada za tafiti za kujua ukubwa wa tatizo

Kisha Serikali ingetangaza hatua za pamoja tunazozichukua kama Taifa.

Badala yake Rais ametaka kuonesha kuwa yeye ni mwenye imani kubwa kwa Mungu kuliko hata maaskofu wetu na mashekhe, na labda kumzidi hata Papa. Yaani tuishi kwa kutegemea miujiza ya Mungu. Mimi ni muumini mkristo mkatoliki, ninatamka kuwa Rais ana upotofu mkubwa wa neno la Mungu. Ni kweli Kristo Yesu alipokuja Duniani aliponya, alifufua na kutenda miujiza mingi. Lakini kama waumini tunatakiwa kujua kwa nini Yesu alitenda miujiza ile? Yesu hakuja kubadilisha mpango wa Mungu, hakuna kuleta mwisho wa magonjwa, mwisho wa vifo vya miili au mwisho wa njaa ya mwili. Bali miujiza ile ililenga kuonesha ukuu wa Mungu, kwamba Mungu akitaka hakuna anachoshindwa. Lakini mpango wake juu ya maisha ya mwanadamu uliachwa vile vile.

Mungu anamshirikisha mwanadamu katika uumbaji, katika kukuza watoto na hata katika uponyaji. Maana yake katika jambo ambalo Mungu anatenda, ameweka ushiriki wa mwanadamu. Usipotaka kushiriki usimjaribu Mungu.

Rais usiwapotoshe watu, wala usipotoshe neno la Mungu.

Yaani sisi tunaowategemea Polisi na wakurugenzi kupora kura, sisi tunaoruhusu wasiojulikana wapoteze na kuua watu wanaotukosoa, sisi tunaowabambikia watu kesi za uhujumu uchumi, leo ndio tuwe na imani kuwazidi Maaskofu na Maimamu na hata Papa, maajabu makuu! Tusimtanie Mungu, tusimchezee Mungu. Mungu anatuvumilia katika uovu wetu kwa sababu anataka kutoa nafasi ya kwetu ya kutubu, badala ya kutubu, tunamjaribu?

Tumwombe Mungu awajalie watawala japo hekima ndogo ya kukabiliana na janga hili la corona. Na wala wasimtumie Mungu kuficha udhaifu wao wa wajibu kama viongozi.

Watawala adhabu yenu mbele za Mungu ni kubwa mnapowapotosha wasio na uelewa. "Ole wao wanaowapoteza wadogo hawa, wanastahili kufungiwa jiwe la kusagie shingoni na kutumbukizwa majini", asema Bwana.
yaani i wish hawa watawala wangekusoma....kinachofanyika sasa ni kejeli kwa Muumba....hawa watu wanaabudu miungu (si Mungu)..kwa kauli zao....huu ni utawala wa kishetani.....
 
Kwani we huwezi kuchukua tahadhari hadi rais akuambie?
Pumbavu kwani nini maaana ya kuwa na raisi

Kwani korona ni ugonjwa unamkuta tu mtu mmoja mmoja kama malaria

Hili ni janga la kitaifa hivyo kila hatua lazima iongozwe kitaifa na kiongozi wa kitaifa

Kuanzia kujulishwa na taarifa za uwepo wake na hataua za kukabiliana na janga husika kama taifa

Mfano: kwa nini Raisi aliamka usiku kutoka usingizini kututangazia kifo cha Mkapa kwani si wangetuma tu tangazo wasafi FM au TBC na taarifa zingefika

Muwe mnafikiri nje ya box basi hata kidogo yaani nyinyi kila mnavyo buruzwa mnakwenda tu hovyoooo! Mxieusssszzzz!!!
 
Yani unaongea kama vile Magufuli ana dawa ila kakataa kukupa!

Kama unataka aseme kitu juu ya hayo mabarakoa, hajakukataza kuvaa.
IQ yako ndogo sana! Wewe unadhani mimi ninam- attack Magufuli, mimi nazungumzia responsible leadership katika kukabili COVID 19!

Hizi comedy anazofanya Waziri wa Afya Dr.Gwajima ndo mikakati ya uongozi!?
Hatujui mpaka sasa ni Watanzania wangapi wamepata maambukizi ya COVID 19,Hospital zetu zina hali gani kwa maana ya vitendea kazi na wauguzi ( Madaktari).

Je tunao mkakati madhubuti wa kuwalinda Madaktari wetu walio mstari wa mbele katika mapambano haya?!

Taasisi zetu za utafiti zinaendelea kufanya nini wakati huu na je tunayo think tank ya Afya inayofuatilia maendeleo ya Chanjo Duniani ili kutushauri kama Taifa ipi ya kutumia?!

Hayo ndo mambo tunataka kujua kuliko haya ya MAZOEZI YA VIFUA!
 
Suala la kilimo linajulikana lakini kuhusu corona imeonesha hakuna njia yeyote ya kuzuia. Kama ipo iseme na useme imefanya kazi wapi?
Nimekwishakwambia China, unataka uambiwe wapi ilipofanya kazi ndio ukubali?
 
e tunao mkakati madhubuti wa kuwalinda Madaktari wetu walio mstari wa mbele katika mapambano haya?!

Taasisi zetu za utafiti zinaendelea kufanya nini wakati huu na je tunayo think tank ya Afya inayofuatilia maendeleo ya Chanjo Duniani ili kutushauri kama Taifa ipi ya kutumia?!
Mambo ya msingi sana haya uliyoyataja hapa.

In fact, wakati huu sisi tunapohimiza nyungu, wenzetu wanajihusisha na kujifunza na kupata wataalam katika nyanja hizi za magonjwa ambukizi.

Sisi tupo tupo tu. Wataalam tunaotegemea wawe mstari wa mbele kisayansi, sasa ndio wanageuzwa kuwa watu wa kufanya 'propaganda' za kulinda heshima ya mtu anayefanya makosa.

Haya yote yatatughalimu sana kama taifa. Itahitaji muda baada ya kuondokana na hali hii ya kuturudisha nyuma, kuja kuwafikia wenzetu watakaokuwa wamepiga hatua kadhaa mbele.
 
rais kaamua kuwa mpinzani wa watu wake.
hataki kuheshimu maoni ya wengi.
anatumia vyombo vyetu vya dola kutulazimisha tukubali ujinga.
anatukomesha kwa kumchagua Lissu.
 
Kimuomba MUNGU NI ujinga?
rais kaamua kuwa mpinzani wa watu wake.
hataki kuheshimu maoni ya wengi.
anatumia vyombo vyetu vya dola kutulazimisha tukubali ujinga.
anatukomesha kwa kumchagua Lissu.
 
Kila mmoja katika nafasi yake, japo kwa viwango tofauti, amewahi kufanya kosa.

Umadhubuti wa kiongozi haupo katika kutofanya kosa bali katika kutafuta suluhisho sahihi baada ya kufanya kosa.

Hatua ya kwanza ya kupata suluhisho sahihi la kosa, ni kukiri umefanya kosa. Mwalimu Nyerere aliwahi kusema,

"..... kukiri upungufu siyo kujidhalilisha bali ni kitendo cha kujiimarisha"

Rais Magufuli, ninaamini amefanya makosa mengi katika kukabiliana na corona. Lakini watanzania tulikuwa tayari kumsamehe maana corona imekuja kwa mara ya kwanza, na hakuna aliye na uzoefu wa kukabiliana nayo.

Mimi ni mmoja wa wahanga wa corona, mtoto wa kaka yangu katika umri wake wa ujana, amepoteza maisha ya Duniani, na kwa dalili alizopitia, tuna hakika ni corona. Lakini kuna rafiki yangu amepoteza ndugu zake 4 na marafiki wa familia 3. Leo baada ya Rais kumpoteza msaidizi wake wa karibu, kwa dalili zinazoonesha, kwa tatizo la corona, tulitarajia kupata neno la faraja kutoka kwa Rais.

Kuna mambo tuliyatarajia kutoka kwa Rais:

1) Watanzania wote kwa umoja wetu, kukiri kuwa tumepatwa na janga la corona

2) Kukiri kuwa hatujawa na jitihada za dhati kukabiliana na corona

3) Kukiri kuwa tumeishi kimbumbumbu bila hata ya kuwa na jitihada za tafiti za kujua ukubwa wa tatizo

Kisha Serikali ingetangaza hatua za pamoja tunazozichukua kama Taifa.

Badala yake Rais ametaka kuonesha kuwa yeye ni mwenye imani kubwa kwa Mungu kuliko hata maaskofu wetu na mashekhe, na labda kumzidi hata Papa. Yaani tuishi kwa kutegemea miujiza ya Mungu. Mimi ni muumini mkristo mkatoliki, ninatamka kuwa Rais ana upotofu mkubwa wa neno la Mungu. Ni kweli Kristo Yesu alipokuja Duniani aliponya, alifufua na kutenda miujiza mingi. Lakini kama waumini tunatakiwa kujua kwa nini Yesu alitenda miujiza ile? Yesu hakuja kubadilisha mpango wa Mungu, hakuna kuleta mwisho wa magonjwa, mwisho wa vifo vya miili au mwisho wa njaa ya mwili. Bali miujiza ile ililenga kuonesha ukuu wa Mungu, kwamba Mungu akitaka hakuna anachoshindwa. Lakini mpango wake juu ya maisha ya mwanadamu uliachwa vile vile.

Mungu anamshirikisha mwanadamu katika uumbaji, katika kukuza watoto na hata katika uponyaji. Maana yake katika jambo ambalo Mungu anatenda, ameweka ushiriki wa mwanadamu. Usipotaka kushiriki usimjaribu Mungu.

Rais usiwapotoshe watu, wala usipotoshe neno la Mungu.

Yaani sisi tunaowategemea Polisi na wakurugenzi kupora kura, sisi tunaoruhusu wasiojulikana wapoteze na kuua watu wanaotukosoa, sisi tunaowabambikia watu kesi za uhujumu uchumi, leo ndio tuwe na imani kuwazidi Maaskofu na Maimamu na hata Papa, maajabu makuu! Tusimtanie Mungu, tusimchezee Mungu. Mungu anatuvumilia katika uovu wetu kwa sababu anataka kutoa nafasi ya kwetu ya kutubu, badala ya kutubu, tunamjaribu?

Tumwombe Mungu awajalie watawala japo hekima ndogo ya kukabiliana na janga hili la corona. Na wala wasimtumie Mungu kuficha udhaifu wao wa wajibu kama viongozi.

Watawala adhabu yenu mbele za Mungu ni kubwa mnapowapotosha wasio na uelewa. "Ole wao wanaowapoteza wadogo hawa, wanastahili kufungiwa jiwe la kusagie shingoni na kutumbukizwa majini", asema Bwana.
Kwakua Korona iko Ikulu Msiwe na shaka stairs mapungufu
 
Huyu mzee amekulia kwenye mfumo dume hivyo hawezi kukiri hata siku moja, kwa utamaduni wake ni kosa kukiri.
kabisa kakulia mifumo dume tena ya bara huko ya kisukuma, elimu yake haijamsaidia hata kidogo,
 
"..... kukiri upungufu siyo kujidhalilisha bali ni kitendo cha kujiimarisha" [emoji1545][emoji1545][emoji1545]
 
JamiiForums-1184182641.jpg
 
Mambo ya msingi sana haya uliyoyataja hapa.

In fact, wakati huu sisi tunapohimiza nyungu, wenzetu wanajihusisha na kujifunza na kupata wataalam katika nyanja hizi za magonjwa ambukizi.

Sisi tupo tupo tu. Wataalam tunaotegemea wawe mstari wa mbele kisayansi, sasa ndio wanageuzwa kuwa watu wa kufanya 'propaganda' za kulinda heshima ya mtu anayefanya makosa.

Haya yote yatatughalimu sana kama taifa. Itahitaji muda baada ya kuondokana na hali hii ya kuturudisha nyuma, kuja kuwafikia wenzetu watakaokuwa wamepiga hatua kadhaa mbele.
Nasisitiza kukuambia kuwa wewe ni boya kichwa maji. Sio kwamba Iq yako ni very low lakini pia ni mpuuzi usie na akili. Mtalaamu wa afya anakubali kutumiwa kufanya propaganda kulinda heshima ya mtu? How? Kwa nini asisimamie taaluma yake na utalaamu wake. Bure kabisa mburula unamaliza mb zako bure kupost utumbo.
 
Back
Top Bottom