Rais neno lako halijatujenga

Rais neno lako halijatujenga

Unafahamu, "herd immunity?" Raisi ni muumini wa hiyo. Hataki kinga ili watu wengi waumwe, wa kufa wafe, na wa kupona wapone ila wawe wamejijengea kinga dhidi ya Covid19 katika miili yao!
Hiyo principle aliitumia Darwin bila mafanikio hadi alipokuja kusahihishwa na kina Mendel na wengine waliogundua na kutumia antibiotic( penicilin).
 
Kwani we huwezi kuchukua tahadhari hadi rais akuambie?
Ni kweli mkuu ila huko vijijini kutokana na uelewa duni hawana habari hasa ila anapotamka kiongozi ndiyo huingia ktk fahamu na kuona Kuna tatizo.Lazima waelekezwe.

Siku hizi Kuna TV kila mahali vijijini wanaona Rais anaita barakoa Ni mavitambaa, wanaona msibani Rais hajavaa barakoa na hakuna hata Ile social distancing. Akiongea badala ya kusema korona ipo inauwa tuchukue tahadhari anasema njia ya kuondoa korona Ni kumwomba mungu.

Kuna mungu gani mwenye huruma na mzembe. Tunachukua tahadhari zote huku tukimwomba mungu

Haongelei habari ya chanjo km plan B pale hali itakapokuwa mbaya zaidi.

Utachukua tahadhari zote kutokana na ufahamu wako lkn wengine hawana habari na hivyo utabaki kuwa ktk hatari tu, ndiyo shida iko hapo. Hebu angalia kwenye daladala watu walivyoshonana wanapimuliana.

Chukua tahadhari mshauri na mwenzako ili kwa pamoja tuweze kuokoa uhai.
 
Kila mmoja katika nafasi yake, japo kwa viwango tofauti, amewahi kufanya kosa.

Umadhubuti wa kiongozi haupo katika kutofanya kosa bali katika kutafuta suluhisho sahihi baada ya kufanya kosa.

Hatua ya kwanza ya kupata suluhisho sahihi la kosa, ni kukiri umefanya kosa. Mwalimu Nyerere aliwahi kusema,

"..... kukiri upungufu siyo kujidhalilisha bali ni kitendo cha kujiimarisha"

Rais Magufuli, ninaamini amefanya makosa mengi katika kukabiliana na corona. Lakini watanzania tulikuwa tayari kumsamehe maana corona imekuja kwa mara ya kwanza, na hakuna aliye na uzoefu wa kukabiliana nayo.

Mimi ni mmoja wa wahanga wa corona, mtoto wa kaka yangu katika umri wake wa ujana, amepoteza maisha ya Duniani, na kwa dalili alizopitia, tuna hakika ni corona. Lakini kuna rafiki yangu amepoteza ndugu zake 4 na marafiki wa familia 3. Leo baada ya Rais kumpoteza msaidizi wake wa karibu, kwa dalili zinazoonesha, kwa tatizo la corona, tulitarajia kupata neno la faraja kutoka kwa Rais.

Kuna mambo tuliyatarajia kutoka kwa Rais:

1) Watanzania wote kwa umoja wetu, kukiri kuwa tumepatwa na janga la corona

2) Kukiri kuwa hatujawa na jitihada za dhati kukabiliana na corona

3) Kukiri kuwa tumeishi kimbumbumbu bila hata ya kuwa na jitihada za tafiti za kujua ukubwa wa tatizo

Kisha Serikali ingetangaza hatua za pamoja tunazozichukua kama Taifa.

Badala yake Rais ametaka kuonesha kuwa yeye ni mwenye imani kubwa kwa Mungu kuliko hata maaskofu wetu na mashekhe, na labda kumzidi hata Papa. Yaani tuishi kwa kutegemea miujiza ya Mungu. Mimi ni muumini mkristo mkatoliki, ninatamka kuwa Rais ana upotofu mkubwa wa neno la Mungu. Ni kweli Kristo Yesu alipokuja Duniani aliponya, alifufua na kutenda miujiza mingi. Lakini kama waumini tunatakiwa kujua kwa nini Yesu alitenda miujiza ile? Yesu hakuja kubadilisha mpango wa Mungu, hakuna kuleta mwisho wa magonjwa, mwisho wa vifo vya miili au mwisho wa njaa ya mwili. Bali miujiza ile ililenga kuonesha ukuu wa Mungu, kwamba Mungu akitaka hakuna anachoshindwa. Lakini mpango wake juu ya maisha ya mwanadamu uliachwa vile vile.

Mungu anamshirikisha mwanadamu katika uumbaji, katika kukuza watoto na hata katika uponyaji. Maana yake katika jambo ambalo Mungu anatenda, ameweka ushiriki wa mwanadamu. Usipotaka kushiriki usimjaribu Mungu.

Rais usiwapotoshe watu, wala usipotoshe neno la Mungu.

Yaani sisi tunaowategemea Polisi na wakurugenzi kupora kura, sisi tunaoruhusu wasiojulikana wapoteze na kuua watu wanaotukosoa, sisi tunaowabambikia watu kesi za uhujumu uchumi, leo ndio tuwe na imani kuwazidi Maaskofu na Maimamu na hata Papa, maajabu makuu! Tusimtanie Mungu, tusimchezee Mungu. Mungu anatuvumilia katika uovu wetu kwa sababu anataka kutoa nafasi ya kwetu ya kutubu, badala ya kutubu, tunamjaribu?

Tumwombe Mungu awajalie watawala japo hekima ndogo ya kukabiliana na janga hili la corona. Na wala wasimtumie Mungu kuficha udhaifu wao wa wajibu kama viongozi.

Watawala adhabu yenu mbele za Mungu ni kubwa mnapowapotosha wasio na uelewa. "Ole wao wanaowapoteza wadogo hawa, wanastahili kufungiwa jiwe la kusagie shingoni na kutumbukizwa majini", asema Bwana.
Nonsense
 
Kwani we huwezi kuchukua tahadhari hadi rais akuambie?
Tumekuvumilia sana ila wewe ni mpuuuzi sana! Vita dhidi ya COVID 19 inahitaji mkakati wa pamoja ili kukabiliana nao!
Taifa hili sasa wapuuzi kama wewe ndo sasa wana ujasiri wa kuongea na kushauri!
Rais Magufuli aonyeshe uongozi katika janga hili vinginevyo CORONA itamdhalilisha kama ilivyomfanya Donald Trump kule Marekani.
 
Vifo vyao tangu ugonjwa unaingia ni vingapi?
Fuatilia mada yangu nyingine

 
Tumekuvumilia sana ila wewe ni mpuuuzi sana! Vita dhidi ya COVID 19 inahitaji mkakati wa pamoja ili kukabiliana nao!
Taifa hili sasa wapuuzi kama wewe ndo sasa wana ujasiri wa kuongea na kushauri!
Rais Magufuli aonyeshe uongozi katika janga hili vinginevyo CORONA itamdhalilisha kama ilivyomfanya Donald Trump kule Marekani.
Acha hasira za kijinga wewe!

Unataka Magufuli achukue hatua gani?
 
Mungu anamshirikisha mwanadamu katika uumbaji, katika kukuza watoto na hata katika uponyaji. Maana yake katika jambo ambalo Mungu anatenda, ameweka ushiriki wa mwanadamu. Usipotaka kushiriki usimjaribu Mungu.

Rais usiwapotoshe watu, wala usipotoshe neno la Mungu.
Mkuu Hamatan, unazidi kudhihirisha umahiri wako katika Jukwaa hili.

Nimechagua maneno uliyoandika katika mistari hiyo mitatu kukumbushia anayohimiza mara kwa mara kiongozi huyu, bila kumhusisha Mungu:

Wananchi sehemu mbalimbali nchini wanahimizwa kila mara na kukumbushwa kwamba serikali haitatoa chakula. Wataachwa wafe kwa njaa!

Mbona Mungu hahusishwi katika kuwalinda hawa wananchi endapo kama njaa itawaingilia kwa ujinga wao wa kutolima mazao ya kuondoa njaa?

Huyu Mungu tunayehimizwa kumpelekea maombi maalum, ni 'specialist' wa majanga kama haya ya corona pekee?
 
Acha hasira za kijinga wewe!

Unataka Magufuli achukue hatua gani?
Wewe ni mpuuuzi na mchumia tumbo! Ulimwona JK alivyokuwa amevaa barakoa yake msibani kwa Eng.Kijazi ! That is how responsible leader acts! Masuala ya imani tunao maaskofu,mashekhe na wachungaji wanapaswa kujenga ktk msingi huo na si Rais.
Refer alichofanya Rais Joe Biden alipoingia State House Day one!
Viongozi wengine wanaogopa kuvaa barakoa kwa kuwa itaonekana wanampinga Rais!
Watanzania sisi siyo wajinga kama mnavyodhani!
 
Mkuu Hamatan, unazidi kudhihirisha umahiri wako katika Jukwaa hili.

Nimechagua maneno uliyoandika katika mistari hiyo mitatu kukumbushia anayohimiza mara kwa mara kiongozi huyu, bila kumhusisha Mungu:

Wananchi sehemu mbalimbali nchini wanahimizwa kila mara na kukumbushwa kwamba serikali haitatoa chakula. Wataachwa wafe kwa njaa!

Mbona Mungu hahusishwi katika kuwalinda hawa wananchi endapo kama njaa itawaingilia kwa ujinga wao wa kutolima mazao ya kuondoa njaa?

Huyu Mungu tunayehimizwa kumpelekea maombi maalum, ni 'specialist' wa majanga kama haya ya corona pekee?
Suala la kilimo linajulikana lakini kuhusu corona imeonesha hakuna njia yeyote ya kuzuia. Kama ipo iseme na useme imefanya kazi wapi?
 
Wewe ni mpuuuzi na mchumia tumbo! Ulimwona JK alivyokuwa amevaa barakoa yake msibani kwa Eng.Kijazi ! That is how responsible leader acts! Masuala ya imani tunao maaskofu,mashekhe na wachungaji wanapaswa kujenga ktk msingi huo na si Rais.
Refer alichofanya Rais Joe Biden alipoingia State House Day one!
Viongozi wengine wanaogopa kuvaa barakoa kwa kuwa itaonekana wanampinga Rais!
Watanzania sisi siyo wajinga kama mnavyodhani!
Barakoa inasaidia nini wewe kiazi?

Nenda amerika na ulaya wakuoneshe rundo la barakoa na malaki ya makaburi
 
Lakini at least wanaonyesha wanajali kuliko nyie wasukuma mnaotegemea " kupasua kuku" kukabiliana na korona!
Nani anajua kwa huu upepo unaovuma hadi Ikulu utaishia wapi?!
Tumeona Marekani Donald Trump,Uingereza Waziri Mkuu wao Boris Johnson na Prince Charles waliugua COVID 19 wakatibiwa wakapona ,nyie hapa na Nyungu zenu za akina Jafo mmeshindwa kumfukiza Eng.Kijazi apone!
Haya tusubiri na hao wanaoendelea na MAZOEZI YA VIFUA!
 
Mkuu Hamatan, unazidi kudhihirisha umahiri wako katika Jukwaa hili.

Nimechagua maneno uliyoandika katika mistari hiyo mitatu kukumbushia anayohimiza mara kwa mara kiongozi huyu, bila kumhusisha Mungu:

Wananchi sehemu mbalimbali nchini wanahimizwa kila mara na kukumbushwa kwamba serikali haitatoa chakula. Wataachwa wafe kwa njaa!

Mbona Mungu hahusishwi katika kuwalinda hawa wananchi endapo kama njaa itawaingilia kwa ujinga wao wa kutolima mazao ya kuondoa njaa?

Huyu Mungu tunayehimizwa kumpelekea maombi maalum, ni 'specialist' wa majanga kama haya ya corona pekee?
Nashukuru Mkuu kwa kuongeza ufafanuzi. Kama watanzania, hawawezi kutafakari kwa namna hiyo, basi ni mizoga.
 
Barakoa inasaidia nini wewe kiazi?

Nenda amerika na ulaya wakuoneshe rundo la barakoa na malaki ya makaburi
Lakini at least wanaonyesha wanajali kuliko nyie wasukuma mnaotegemea "kupasua kuku" kukabiliana na CORONA.
Nani anajua huu upepo unaovumia hadi Ikulu utaishia wapi?!
Tumeona Marekani Donald Trump, Uingereza Waziri Mkuu wao Boris Johnson na Prince Charles waliugua COVID 19 wakatibiwa na kupona, nyie hapa mmeshindwa kumfukiza Eng.Kijazi apone na nyungu zenu za akina Jafo.?!
Haya ngoja tuone kwani mmeanzisha sasa MAZOEZI YA VIFUA !!!!
 
Yona alipohubiri Ninawi utaangamizwa baada ya siku arobaini watu aliamua kufunga na kutubu, ndipo mfalme aliposikia wanachofanya watu akatangaza kufunga kwa watu wote, wananchi wakisubiri kutangaziwa na rais ni ujinga wa kiwango cha lami.
Yeyote mwenye kusubiri tamko la mkuu ndio aanze jitihada za kujikinga ni mzembe.
 
Akikiri ndio ugonjwa unaondoka? Mbona mnakuwa vipofu wa akili?
Nashangaa watu walivyomkomalia JPM utadhani yeye ndio kila Kitu.kila mmojawetu awajibike kwa nafasi
yake na sio kusubiri fulani atuwajibishe. Kama JPM anasimamia kile anachokiamini basi na kila mmojawetu asimame anapopaamini sio kulumbana haijengi na haisaidii
 
Back
Top Bottom