Rais neno lako halijatujenga

Rais neno lako halijatujenga

Hamatan

JF-Expert Member
Joined
Nov 10, 2020
Posts
8,025
Reaction score
18,446
Kila mmoja katika nafasi yake, japo kwa viwango tofauti, amewahi kufanya kosa.

Umadhubuti wa kiongozi haupo katika kutofanya kosa bali katika kutafuta suluhisho sahihi baada ya kufanya kosa.

Hatua ya kwanza ya kupata suluhisho sahihi la kosa, ni kukiri umefanya kosa. Mwalimu Nyerere aliwahi kusema,

"..... kukiri upungufu siyo kujidhalilisha bali ni kitendo cha kujiimarisha"

Rais Magufuli, ninaamini amefanya makosa mengi katika kukabiliana na corona. Lakini Watanzania tulikuwa tayari kumsamehe maana corona imekuja kwa mara ya kwanza, na hakuna aliye na uzoefu wa kukabiliana nayo.

Mimi ni mmoja wa wahanga wa corona, mtoto wa kaka yangu katika umri wake wa ujana, amepoteza maisha ya Duniani, na kwa dalili alizopitia, tuna hakika ni corona. Lakini kuna rafiki yangu amepoteza ndugu zake 4 na marafiki wa familia 3. Leo baada ya Rais kumpoteza msaidizi wake wa karibu, kwa dalili zinazoonesha, kwa tatizo la corona, tulitarajia kupata neno la faraja kutoka kwa Rais.

Kuna mambo tuliyatarajia kutoka kwa Rais:

1) Watanzania wote kwa umoja wetu, kukiri kuwa tumepatwa na janga la corona

2) Kukiri kuwa hatujawa na jitihada za dhati kukabiliana na corona

3) Kukiri kuwa tumeishi kimbumbumbu bila hata ya kuwa na jitihada za tafiti za kujua ukubwa wa tatizo

Kisha Serikali ingetangaza hatua za pamoja tunazozichukua kama Taifa.

Badala yake Rais ametaka kuonesha kuwa yeye ni mwenye imani kubwa kwa Mungu kuliko hata maaskofu wetu na mashekhe, na labda kumzidi hata Papa. Yaani tuishi kwa kutegemea miujiza ya Mungu. Mimi ni muumini mkristo mkatoliki, ninatamka kuwa Rais ana upotofu mkubwa wa neno la Mungu. Ni kweli Kristo Yesu alipokuja Duniani aliponya, alifufua na kutenda miujiza mingi. Lakini kama waumini tunatakiwa kujua kwa nini Yesu alitenda miujiza ile? Yesu hakuja kubadilisha mpango wa Mungu, hakuna kuleta mwisho wa magonjwa, mwisho wa vifo vya miili au mwisho wa njaa ya mwili. Bali miujiza ile ililenga kuonesha ukuu wa Mungu, kwamba Mungu akitaka hakuna anachoshindwa. Lakini mpango wake juu ya maisha ya mwanadamu uliachwa vile vile.

Mungu anamshirikisha mwanadamu katika uumbaji, katika kukuza watoto na hata katika uponyaji. Maana yake katika jambo ambalo Mungu anatenda, ameweka ushiriki wa mwanadamu. Usipotaka kushiriki usimjaribu Mungu.

Rais usiwapotoshe watu, wala usipotoshe neno la Mungu.

Yaani sisi tunaowategemea Polisi na wakurugenzi kupora kura, sisi tunaoruhusu wasiojulikana wapoteze na kuua watu wanaotukosoa, sisi tunaowabambikia watu kesi za uhujumu uchumi, leo ndio tuwe na imani kuwazidi Maaskofu na Maimamu na hata Papa, maajabu makuu! Tusimtanie Mungu, tusimchezee Mungu. Mungu anatuvumilia katika uovu wetu kwa sababu anataka kutoa nafasi ya kwetu ya kutubu, badala ya kutubu, tunamjaribu?

Tumwombe Mungu awajalie watawala japo hekima ndogo ya kukabiliana na janga hili la corona. Na wala wasimtumie Mungu kuficha udhaifu wao wa wajibu kama viongozi.

Watawala adhabu yenu mbele za Mungu ni kubwa mnapowapotosha wasio na uelewa. "Ole wao wanaowapoteza wadogo hawa, wanastahili kufungiwa jiwe la kusagie shingoni na kutumbukizwa majini", asema Bwana.
 
Unapotosha mkuu, hakuna mfumo dume unaozuia mwanaume kukiri kosa.

Kuna mtanzania gani ambae hajakulia katika mfumo dume ?
Unafahamu, "herd immunity?" Raisi ni muumini wa hiyo. Hataki kinga ili watu wengi waumwe, wa kufa wafe, na wa kupona wapone ila wawe wamejijengea kinga dhidi ya Covid19 katika miili yao!
 
"Ole wao wanaowapoteza wadogo hawa, wanastahili kufungiwa jiwe la kusagie shingoni na kutumbukizwa majini
Hiro jiwe ningelitafuta Mimi, nmepoteza marafiki hadi sasa kama sita. TLS wamepoteza members 25 kuanzia January hadi Jana 19 February 2020. Poliis wamepoteza RSO, DSO, na polisi wa kawaida wa kutosha tu. Tunataka nani afe ndio tuungane kama taifa?
 
Kwani msaidizi wake kaondolewa na kadudu hako??
Weka source mkuu
 
Tutumie hekima tu jaman hili janga lipo uwe ccm au chadema sote ni watanzania akifa hata mmoja tu nipigo kwetu sote kama ni tahadhari watu wameshachukua wengi tu wenye kujielewa tatizo liko huko vijijin jaman na watu wanavosema mh Rais atoe tamko kikawaida na kiutamaduni wetu wengi hawachukui tahadhari wakiamin rais hajasema corona ipo na hawaoni takwimu Za vifo vya corona.

Sasa kwa mwananchi wa kawaida au wakijijin asipoambiwa au isipotoka kauli ukweli ndio huo tutazika sana ndugu zetu mh Rais popote ulipo ukoa watanzania tunapoteza nguvukaz na jamiii inakuwa kwenye taharuki bila kujua lipi ni sahihi wenye kumshauri wa mshauri tunavopoteza ni vingi zaid ya ukimya wake
 
Hiro jiwe ningelitafuta Mimi, nmepoteza marafiki hadi sasa kama sita. TLS wamepoteza members 25 kuanzia January hadi Jana 19 February 2020. Poliis wamepoteza RSO, DSO, na polisi wa kawaida wa kutosha tu. Tunataka nani afe ndio tuungane kama taifa?
Kinachoumiza, wengi wanazidi kupotezwa. Lakini mbaya zaidi ni kwamba hata sisi tunaolijua tatizo hilo kikamilifu, bado hatujaikwepa hatari. Jitihada kama zile za kuvaa barakoa zina msaada mkubwa kama ninyi nyote mkivaa, na siyo wewe mtu mmoja.
 
Kila mmoja katika nafasi yake, japo kwa viwango fulani, amewahi kufanya kosa.

Umadhubuti wa kiongozi haupo katika kutofanya kosa bali katika kutafuta suluhisho sahihi baada ya kufanya kosa...
Kiri mwenyewe na familia yako! Sisi na JPM wetu tutaendelea kumkiri Mungu siyo corona!

Ni kama kuangalia nyoka wa shaba badala hao waliokuwa wanawauma wana wa Israeli! Kama umetumwa, nenda kawaambie bado tupo macho na hatuna mpango wa kulala!

Mungu tunaomba uturehemu! Mungu tunaomba utuponye magonjwa yote! Mungu tunaomba uiponye nchi yetu Tanzania, amen! Mungu tunaomba uzidi kumlinda kumuongoza na kumbariki rais wetu mpendwa Mh Dr JPM na serikali zetu zote! Mungu tunaomba uzidi kuilinda na kuibariki nchi yetu Tanzania!
 
Tutumie hekima tu jaman hili janga lipo uwe ccm au chadema sote ni watanzania akifa hata mmoja tu nipigo kwetu sote kama ni tahadhari watu wameshachukua wengi tu wenye kujielewa tatizo liko huko vijijin jaman na watu wanavosema mh Rais atoe tamko kikawaida na kiutamaduni wetu wengi hawachukui tahadhari wakiamin rais hajasema corona ipo na hawaoni takwimu Za vifo vya corona sasa kwa mwananchi wa kawaida au wakijijin asipoambiwa au isipotoka kauli ukweli ndio huo tutazika sana ndugu zetu mh Rais popote ulipo ukoa watanzania tunapoteza nguvukaz na jamiii inakuwa kwenye taharuki bila kujua lipi ni sahihi wenye kumshauri wa mshauri tunavopoteza ni vingi zaid ya ukimya wake
Wenzetu Israel wamepunguza mortality by 94%. Kilichowasaidia ni kuwapima watu wao.

Ukigundulika upo Covid 19 positive, hata kama huumwi unaingizwa kwenye Covid 19 management protocol. Ukipata matibabu wakati huo au angalao wakati hujavuka mild sysmptoms stage, uwezekano wa wewe kuuawa na Covid 19 ni 0%.

Tatizo ni pale unapoingia kwenye hatua ya kushindwa kupumua. Ukifikia hatua hiyo, umeingia kwenye hatari ya kifo.

Ni muhimu sana kupima. Kama Serikali ingekuwa inatupima, kila aliye positive, awe anaumwa au mzima, anastahili kupata matibabu, na kwa maendeleo yaliyofikiwa kwa sasa, ndani ya siku 7 - 12 anakuwa negative.

Nisistize sana NEVER EVER TRY TO PUT PATIENT KWENYE NYUNGU, HUKO NI KUMWUA. Nitapandisha kwenye uzi tofauti The Jewish Covid 19 management protocol, ambayo imewasaidia sana wayahudi. Leo Covid 19 kwa Israel, siyo tishio tena. Nina uhakika itawasaidia wengi. Mpaka sasa imekwishawasaidia marafiki zangu wengi.
 
Back
Top Bottom