Rais neno lako halijatujenga

Rais neno lako halijatujenga

Unafahamu, "herd immunity?" Raisi ni muumini wa hiyo. Hataki kinga ili watu wengi waumwe, wa kufa wafe, na wa kupona wapone ila wawe wamejijengea kinga dhidi ya Covid19 katika miili yao!
herd immunity doesnt work always. especialy kirusi kikiwa kinatabia ya kubadolika.. mutations.
ndio maana leo tuna variants wa UK,variants qa south africa. una variants wengine

na katika wave hii ya pili hawa variant ndio wamekuwa wakali zaidi. maana kwenye mutation zao.. wamekuwa na uwezo wa kukwepa kinga.
sweden wali practise hii kitu first virus outbreak.. wali survive.. second wave imewala mbaya..
mpaka sasa wana 12598 death, with 627000 maambukizi.

wame request chanjo.
 
Kiri mwenyewe na familia yako! Sisi na JPM wetu tutaendelea kumkiri Mungu siyo corona!
Ni kama kuangalia nyoka wa shaba badala hao waliokuwa wanawauma wana wa Israeli! Kama umetumwa, nenda kawaambie bado tupo macho na hatuna mpango wa kulala!
Mungu tunaomba uturehemu! Mungu tunaomba utuponye magonjwa yote! Mungu tunaomba uiponye nchi yetu Tanzania, amen! Mungu tunaomba uzidi kumlinda kumuongoza na kumbariki rais wetu mpendwa Mh Dr JPM na serikali zetu zote! Mungu tunaomba uzidi kuilinda na kuibariki nchi yetu Tanzania!
Rais hapendwi kwa sura, kabila au chama chake pale kwa kuwaongoza watu wake kwenye njia salama.

Sijatumwa na mwanadamu bali na hekima ya Mungu iishiyo ndani yangu. Tangu mwanzo Mungu ametoa uhuru kwa mwanadamu, ama kumfuata yeye aliye chanzo cha hekima au yule mwovu bingwa wa ulaghai. Wenye Roho wa Mungu wote, itafuteni hekima ya Mungu kwenye hili janga. Ujumbe wa Mungu ni kuwa, 'nimemshirikisha mwandamu katika uuambaji, nimemshirikisha mwanadamu katika uponyaji, nimeshirikisha mwanadamu katika wokovu'
 
Kila mmoja katika nafasi yake, japo kwa viwango fulani, amewahi kufanya kosa.

Umadhubuti wa kiongozi haupo katika kutofanya kosa bali katika kutafuta suluhisho sahihi baada ya kufanya kosa.

Hatua ya kwanza ya kupata suluhisho sahihi la kosa, ni kukiri umefanya kosa. Mwalimu Nyerere aliwahi kusema,

"..... kukiri upungufusiyo kujidhalilisha bali ni kitendo cha kujiimarisha"

Rais Magufuli, ninaamini amefanya makosa mengi katika kukabiliana na corona. Lakini watanzania tulikuwa tayari kumsamehe maana corona imekuja kwa mara ya kwanza, na hakuna aliye na uzoefu wa kukabiliana nayo.

Mimi ni mmoja wa wahanga wa corona, mtoto wa kaka yangu katika umri wake wa ujana, amepoteza maisha ya Duniani, na kwa dalili alizopitia, tuna hakika ni corona. Lakini kuna rafiki yangu amepoteza ndugu zake 4 na marafiki wa familia 3. Leo baada ya Rais kumpoteza msaidizi wake wa karibu, kwa dalili zinazoonesha, kwa tatizo la corona, tulitarajia kupata neno la faraja kutoka kwa Rais.

Kuna mambo tuliyatarajia kutoka kwa Rais:

1) Watanzania wote kwa umoja wetu, kukiri kuwa tumepatwa na janga la corona

2) Kukiri kuwa hatujawa na jitihada za dhati kukabiliana na corona

3) Kukiri kuwa tumeishi kimbumbumbu bila hata ya kuwa na jitihada za tafiti za kujua ukubwa wa tatizo

Kisha Serikali ingetangaza hatua za pamoja tunazozichukua kama Taifa.

Badala yake Rais ametaka kuonesha kuwa yeye ni mwenye imani kubwa kwa Mungu kuliko hata maaskofu wetu na mashekhe, na labda kumzidi hata Papa. Yaani tuishi kwa kutegemea miujiza ya Mungu. Mimi ni muumini mkristo mkatoliki, ninatamka kuwa Rais ana upotofu mkubwa wa neno la Mungu. Ni kweli Kristo Yesu alipokuja Duniani aliponya, alifufua na kutenda miujiza mingi. Lakini kama waumini tunatakiwa kujua kwa nini Yesu alitenda miujiza ile? Yesu hakuja kubadilisha mpango wa Mungu, hakuna kuketa mwisho wa magonjwa, mwisho wa vifo vya miili au mwisho wa njaa ya mwili. Bali miujiza ile ililenga kuonesha ukuu wa Mungu, kwamba Mungu akitaka hakuna anachoshindwa. Lakini mpango wake juu ya maisha ya mwanadamu uliachwa vile vile.

Mungu anamshirikisha mwanadamu katika uumbaji, katika kukuza watoto na hata katika uponyaji. Maana yake katika jambo ambalo Mungu anatenda, ameweka ushiriki wa mwanadamu. Usipotaka kushiriki usimjaribu Mungu.

Rais usiwapotoshe watu, wala usipotoshe neno la Mungu.

Yaani sisi tunaowategemea Polisi na wakurugenzi kupora kura, sisi tunaoruhusu wasiojulikana wapoteze na kuua watu wanaotukosoa, sisi tunaowabambikia watu kesi za uhujumu uchumi, leo ndio tuwe na imani kuwazidi Maaskofu na Maimamu na hata Papa, maajabu makuu! Tusimtanie Mungu, tusimchezee Mungu. Mungu anatuvumilia katika uovu wetu kwa sababu anataka kutoa nafasi ya kwyeu ya kutubu, badala ya kutubu, tunamjaribu?

Tumwombe Mungu awajalie watawala japo hekima ndogo ya kukabiliana na janga hili la corona. Na wala wasimtumie Mungu kuficha udhaifu wao wa wajibu kama viongozi.

Watawala adhabu yenu mbele za Mungu ni kubwa mnapowapotosha wasio na uelewa. "Ole wao wanaowapoteza wadogo hawa, wanastahili kufungiwa jiwe la kusagie shingoni na kutumbukizwa majini", asema Bwana.

1000000% kweli tupu.✔✔✔✔
 
Huyu mzee amekulia kwenye mfumo dume hivyo hawezi kukiri hata siku moja, kwa utamaduni wake ni kosa kukiri.
wewe ulishafiwa ndugu au jirani kwa Corona nje magonjwa mengine?
 
Sasa wewe mwenye akili unaeishi kwa kakaako umesaidia nini kutatua janga la corona?
Wakati mwingine tufiche kidogo upumbavu wetu ili kuponya Taifa. Rais ndiye Kiongozi, ndiye mfariji, ndiye tumaini la Wananchi, kauli yake ni faraja tosha. Kama tunavyopambana na Maralia, TB, Ukimwi n.k na kuona matangazo katika Televisheni, Radio na kupewa nguvu na mataifa yakiyoendelea kwa kuwa hatuwezi kupambana nayo ndivyo ilitakiwa Rais kuonesha uwazi wa kuvamiwa na janga hili halafu kwa pamoja tutafute namna ua kupambana nalo kwa kuwa sisi hatuwezi. Wapo watu kwa kauli za Rais hawachukui tahadhari kwa imani kuwa Corona haipo. Tuwazr kwa lengo la kusaidia na sio kuponda hapa as if akifa ndugu yako hao Viongozi watahudhunika
 
Wizara ya afya imepewa likizo ya lazima..
Huku Madaktari,Manesi na wenzao wakihatarishiwa afya na maisha yao kwa kuwa wagonjwa hawa wanafariki kw a changamoto ya upumuaji wanahudumiwa katika hospitals zetu hadi umauti unawakuta.Sioni tahadhari za kutosha kuwalinda watumishi wa sekta ya afya kwa kuwapatia vitendea kazi vinginevyo tutapoteza raslimali watu.
 
Kiri mwenyewe na familia yako! Sisi na JPM wetu tutaendelea kumkiri Mungu siyo corona!
Ni kama kuangalia nyoka wa shaba badala hao waliokuwa wanawauma wana wa Israeli! Kama umetumwa, nenda kawaambie bado tupo macho na hatuna mpango wa kulala!
Mungu tunaomba uturehemu! Mungu tunaomba utuponye magonjwa yote! Mungu tunaomba uiponye nchi yetu Tanzania, amen! Mungu tunaomba uzidi kumlinda kumuongoza na kumbariki rais wetu mpendwa Mh Dr JPM na serikali zetu zote! Mungu tunaomba uzidi kuilinda na kuibariki nchi yetu Tanzania!
Huyo Mungu mnayemuomba naamini hasikii maombi yenu. Mungu wetu Muumba Mbingu na Ardhi, Mmiliki wa kila kitu, Mungu Baba, Mwana na Roho Mtakatifu ametupa maarifa ya kujua baya na jema, hukai ukiomba tu Mungu akakupa, bali anasema utafute. Mungu huyu muweza wa yote ndiye amewapa uwezo wanadamu wa kutambu kuwa huu ni ugonjwa ma ili kuutibu fanyeni haya. Mungu wetu muweza hasemi uombe tu, hapana
 
Kila mmoja katika nafasi yake, japo kwa viwango tofauti, amewahi kufanya kosa.

Umadhubuti wa kiongozi haupo katika kutofanya kosa bali katika kutafuta suluhisho sahihi baada ya kufanya kosa.

Hatua ya kwanza ya kupata suluhisho sahihi la kosa, ni kukiri umefanya kosa. Mwalimu Nyerere aliwahi kusema,

"..... kukiri upungufu siyo kujidhalilisha bali ni kitendo cha kujiimarisha"

Rais Magufuli, ninaamini amefanya makosa mengi katika kukabiliana na corona. Lakini watanzania tulikuwa tayari kumsamehe maana corona imekuja kwa mara ya kwanza, na hakuna aliye na uzoefu wa kukabiliana nayo.

Mimi ni mmoja wa wahanga wa corona, mtoto wa kaka yangu katika umri wake wa ujana, amepoteza maisha ya Duniani, na kwa dalili alizopitia, tuna hakika ni corona. Lakini kuna rafiki yangu amepoteza ndugu zake 4 na marafiki wa familia 3. Leo baada ya Rais kumpoteza msaidizi wake wa karibu, kwa dalili zinazoonesha, kwa tatizo la corona, tulitarajia kupata neno la faraja kutoka kwa Rais.

Kuna mambo tuliyatarajia kutoka kwa Rais:

1) Watanzania wote kwa umoja wetu, kukiri kuwa tumepatwa na janga la corona

2) Kukiri kuwa hatujawa na jitihada za dhati kukabiliana na corona

3) Kukiri kuwa tumeishi kimbumbumbu bila hata ya kuwa na jitihada za tafiti za kujua ukubwa wa tatizo

Kisha Serikali ingetangaza hatua za pamoja tunazozichukua kama Taifa.

Badala yake Rais ametaka kuonesha kuwa yeye ni mwenye imani kubwa kwa Mungu kuliko hata maaskofu wetu na mashekhe, na labda kumzidi hata Papa. Yaani tuishi kwa kutegemea miujiza ya Mungu. Mimi ni muumini mkristo mkatoliki, ninatamka kuwa Rais ana upotofu mkubwa wa neno la Mungu. Ni kweli Kristo Yesu alipokuja Duniani aliponya, alifufua na kutenda miujiza mingi. Lakini kama waumini tunatakiwa kujua kwa nini Yesu alitenda miujiza ile? Yesu hakuja kubadilisha mpango wa Mungu, hakuna kuleta mwisho wa magonjwa, mwisho wa vifo vya miili au mwisho wa njaa ya mwili. Bali miujiza ile ililenga kuonesha ukuu wa Mungu, kwamba Mungu akitaka hakuna anachoshindwa. Lakini mpango wake juu ya maisha ya mwanadamu uliachwa vile vile.

Mungu anamshirikisha mwanadamu katika uumbaji, katika kukuza watoto na hata katika uponyaji. Maana yake katika jambo ambalo Mungu anatenda, ameweka ushiriki wa mwanadamu. Usipotaka kushiriki usimjaribu Mungu.

Rais usiwapotoshe watu, wala usipotoshe neno la Mungu.

Yaani sisi tunaowategemea Polisi na wakurugenzi kupora kura, sisi tunaoruhusu wasiojulikana wapoteze na kuua watu wanaotukosoa, sisi tunaowabambikia watu kesi za uhujumu uchumi, leo ndio tuwe na imani kuwazidi Maaskofu na Maimamu na hata Papa, maajabu makuu! Tusimtanie Mungu, tusimchezee Mungu. Mungu anatuvumilia katika uovu wetu kwa sababu anataka kutoa nafasi ya kwetu ya kutubu, badala ya kutubu, tunamjaribu?

Tumwombe Mungu awajalie watawala japo hekima ndogo ya kukabiliana na janga hili la corona. Na wala wasimtumie Mungu kuficha udhaifu wao wa wajibu kama viongozi.

Watawala adhabu yenu mbele za Mungu ni kubwa mnapowapotosha wasio na uelewa. "Ole wao wanaowapoteza wadogo hawa, wanastahili kufungiwa jiwe la kusagie shingoni na kutumbukizwa majini", asema Bwana.
Hafai hata kidogo kuongoza taifa, hafai!
 
Wakati mwingine tufiche kidogo upumbavu wetu ili kuponya Taifa. Rais ndiye Kiongozi, ndiye mfariji, ndiye tumaini la Wananchi, kauli yake ni faraja tosha. Kama tunavyopambana na Maralia, TB, Ukimwi n.k na kuona matangazo katika Televisheni, Radio na kupewa nguvu na mataifa yakiyoendelea kwa kuwa hatuwezi kupambana nayo ndivyo ilitakiwa Rais kuonesha uwazi wa kuvamiwa na janga hili halafu kwa pamoja tutafute namna ua kupambana nalo kwa kuwa sisi hatuwezi. Wapo watu kwa kauli za Rais hawachukui tahadhari kwa imani kuwa Corona haipo. Tuwazr kwa lengo la kusaidia na sio kuponda hapa as if akifa ndugu yako hao Viongozi watahudhunika
Tahadhali ipi unayotaka watu wachukue?
 
Tahadhali ipi unayotaka watu wachukue?
Tungejifunza kwa Waisrael. Tuone wenzetu wamefanya nini hata kuweza kushusha vifo kwa 94% ukilinganisha na hapo awali. Leo Israel ukipata Covid 19, uwezekano wako wa kufa ni kama haupo.

Kwa Dunia nzima, idadi ya wanaokufa ni kama 3 - 4% ya watu waliopatwa na maambukizi. Leo kwa Israel 94% ya hao 3-4%, wanapona. Ni sawa na kusema wana uhakika karibia wote wanaoambukizwa Covid 19, wanapona. Kwa nini tusinijifunze kwa watu kama hawa?

Lakini Waisrael wanasema kilichowafanya wafikie hapo ni kuwapima watu wao wote mara kwa mara, na anayegundulika ni Covid 19 positive, mara moja anaingizwa kwenye Covid 19 management protocol.

Alipotupoteza kabisa Magufuli, ni kufuta upimaji.

Israel 99.2% ya wote waliopata maambukizi mpaka sasa wamepona. Wanahangaikia 0.8% cases. Mpaka mwisho wa mwezi hawatarajii kuwa na cases za vifo. Sayansi inatenda kazi.
 
Vifo vyao tangu ugonjwa unaingia ni vingapi?
 
Kila mmoja katika nafasi yake, japo kwa viwango tofauti, amewahi kufanya kosa.

Umadhubuti wa kiongozi haupo katika kutofanya kosa bali katika kutafuta suluhisho sahihi baada ya kufanya kosa.

Hatua ya kwanza ya kupata suluhisho sahihi la kosa, ni kukiri umefanya kosa. Mwalimu Nyerere aliwahi kusema,

"..... kukiri upungufu siyo kujidhalilisha bali ni kitendo cha kujiimarisha"

Rais Magufuli, ninaamini amefanya makosa mengi katika kukabiliana na corona. Lakini watanzania tulikuwa tayari kumsamehe maana corona imekuja kwa mara ya kwanza, na hakuna aliye na uzoefu wa kukabiliana nayo.

Mimi ni mmoja wa wahanga wa corona, mtoto wa kaka yangu katika umri wake wa ujana, amepoteza maisha ya Duniani, na kwa dalili alizopitia, tuna hakika ni corona. Lakini kuna rafiki yangu amepoteza ndugu zake 4 na marafiki wa familia 3. Leo baada ya Rais kumpoteza msaidizi wake wa karibu, kwa dalili zinazoonesha, kwa tatizo la corona, tulitarajia kupata neno la faraja kutoka kwa Rais.

Kuna mambo tuliyatarajia kutoka kwa Rais:

1) Watanzania wote kwa umoja wetu, kukiri kuwa tumepatwa na janga la corona

2) Kukiri kuwa hatujawa na jitihada za dhati kukabiliana na corona

3) Kukiri kuwa tumeishi kimbumbumbu bila hata ya kuwa na jitihada za tafiti za kujua ukubwa wa tatizo

Kisha Serikali ingetangaza hatua za pamoja tunazozichukua kama Taifa.

Badala yake Rais ametaka kuonesha kuwa yeye ni mwenye imani kubwa kwa Mungu kuliko hata maaskofu wetu na mashekhe, na labda kumzidi hata Papa. Yaani tuishi kwa kutegemea miujiza ya Mungu. Mimi ni muumini mkristo mkatoliki, ninatamka kuwa Rais ana upotofu mkubwa wa neno la Mungu. Ni kweli Kristo Yesu alipokuja Duniani aliponya, alifufua na kutenda miujiza mingi. Lakini kama waumini tunatakiwa kujua kwa nini Yesu alitenda miujiza ile? Yesu hakuja kubadilisha mpango wa Mungu, hakuna kuleta mwisho wa magonjwa, mwisho wa vifo vya miili au mwisho wa njaa ya mwili. Bali miujiza ile ililenga kuonesha ukuu wa Mungu, kwamba Mungu akitaka hakuna anachoshindwa. Lakini mpango wake juu ya maisha ya mwanadamu uliachwa vile vile.

Mungu anamshirikisha mwanadamu katika uumbaji, katika kukuza watoto na hata katika uponyaji. Maana yake katika jambo ambalo Mungu anatenda, ameweka ushiriki wa mwanadamu. Usipotaka kushiriki usimjaribu Mungu.

Rais usiwapotoshe watu, wala usipotoshe neno la Mungu.

Yaani sisi tunaowategemea Polisi na wakurugenzi kupora kura, sisi tunaoruhusu wasiojulikana wapoteze na kuua watu wanaotukosoa, sisi tunaowabambikia watu kesi za uhujumu uchumi, leo ndio tuwe na imani kuwazidi Maaskofu na Maimamu na hata Papa, maajabu makuu! Tusimtanie Mungu, tusimchezee Mungu. Mungu anatuvumilia katika uovu wetu kwa sababu anataka kutoa nafasi ya kwetu ya kutubu, badala ya kutubu, tunamjaribu?

Tumwombe Mungu awajalie watawala japo hekima ndogo ya kukabiliana na janga hili la corona. Na wala wasimtumie Mungu kuficha udhaifu wao wa wajibu kama viongozi.

Watawala adhabu yenu mbele za Mungu ni kubwa mnapowapotosha wasio na uelewa. "Ole wao wanaowapoteza wadogo hawa, wanastahili kufungiwa jiwe la kusagie shingoni na kutumbukizwa majini", asema Bwana.

Mkuu, kuna kuna mambo mawili ambayo Rais Magufuli hafahamu na mbaya zaidi viongozi wa dini zote wapo kimya hawataki kumfahamisha mambo hayo.

Mambo yenyewe ni haya:-

(1) kumtegemea Mungu---- ni katika hali ipi Mungu anatakiwa ategemewe.
(2) Juhudi za binadamu----- ni juhudi zipi mwanadamu anatakiwa azifanye kutanzua shida zake.

Juhudi za binadamu na kumtegemea Mungu ni vitu vinavyoenda sambamba kwani kumtegemea Mungu bila kutia juhudi katika shida ni kumjaribu Mungu kitu ambacho Rais Magufuli ndicho anachofanya, kutegemea juhudi zako binafsi katika shida bila kumtegemea Mungu hicho ni kiburi.

Katika hili janga la watu "kushindwa kupumua" hadi kupelekea vifo ilitakiwa serikali ichukue hatua na katika hizo hatua ndipo tumuombe Mungu atie baraka zake lakini kumuomba Mungu tu bila kuchuka hatua yeyote hapo ni sawa na Kumjaribu Mungu kitendo ambacho kinaendelea kutugharimu kila uchao.

Wito kwa kila mwananchi tuchukue tahadhari kujikinga kwani; kila mchuma janga hula na nduguze, wahenga walisema.
 
Back
Top Bottom