Rais Magufuli yashamshinda?

Rais Magufuli yashamshinda?

Hivi ni mimi tu au na wengine mpo mnaoona kama vile mambo yashamshinda huyu Magufuli?

Kuna hali fulani hivi naiona ambapo jamaa ni kama anaamka tu kila asubuhi na kutoa maamuzi ya kukurupuka kurupuka.
Yaani yeye ni amri tu....fanya hivi....fukuza huyu....twende kule...nk.

Yapo baadhi ambayo ni mazuri ambapo mtu unaona kabisa hapa nia ni nzuri lakini kuna mengine yenye ukakasi sana hadi kunifanya nianze kuhoji hekima na busara za huyo bwana!

---
Mimi ni mmoja wa watu wanaoamini kuwa rais wetu huyu, mheshimiwa mtukufu Dkt. John Pombe Joseph Magufuli si kiongozi mzuri hata kidogo, hususan katika ngazi ya urais.

Hilo nimekuwa nikilisema kwa muda mrefu sasa. Nakumbuka hata ile siku alipoteuliwa kuipeperusha bendera ya CCM nilisema hivyo humu humu JF.

Kwa kiasi fulani namkubali kwenye usimamizi lakini si kwenye uongozi. Hana kabisa haiba ya kiuongozi. Pia hana sifa za kuweza kuwa kiongozi mzuri.

Ni mtu mwenye jazba. Ana jeuri. Mwenye kuongea bila kufikiria athari za maneno yake[nyakati zingine]. Wengine wanasema eti kuwa hashauriki. Kwa ufupi ni mengi sana yanasemwa juu yake kiasi kwamba mengine ni vigumu kwa watu wa mbali kama sisi kujua kama ni ya kweli au la. Hivyo kwa sisi wa mbali tunaenda na yale tuyaonayo na tuyasikiayo toka kwake yeye mwenyewe.

Sasa kwa jinsi vile mambo yanavyoenda sasa hivi kuna kila dalili huenda nchi imeshamshinda kuiongoza. Hivyo ndivyo niuonavyo mwelekeo.

Hata ndani ya chama chake ukiangalia vizuri utaona nyuso nyingi tu za manung'uniko toka kwa wakereketwa. Wengi wao siku hizi wanashindwa hata kumtetea. Wapo kimyaaaa utadhani wagonjwa. CCM hawana furaha kabisa.

Naamini asipojiangalia na kujifanyia tathmini basi hiyo kazi itamshinda kabla hata hajafikia nusu ya muhula wa hii miaka mitano.

Niliwahi kuandika kuhusu 'a police state'. Jikumbushe....

https://www.jamiiforums.com/threads/a-police-state.1105346/#post-17414170
uelewa wako mdogo yasimshinde kinyata issue ya madakitari yamshinde ngosha we acha kabisa ngosha ana uhakika na anachofanya amejipanga vilivyo.
 
uelewa wako mdogo yasimshinde kinyata issue ya madakitari yamshinde ngosha we acha kabisa ngosha ana uhakika na anachofanya amejipanga vilivyo.

Oh basi sawa....yangu macho tu.
 
Hivi ule mpango wa kufanya usafi kila mwisho wa mwezi bado upo?
kwa mawazo yangu naona urais wa nchi wapewe watu wa pwani tu-wao mara nyingi ni easy going na hawana makuu kutokana na environment walizokulia-Hawa akina ngosha theory za development walizokariri zinawapelekesha kiasi wanashindwa tofautisha reality na njozi na malengo yasipofikiwa wanageuka mbogo na kuharibu kabisa
 
Hivi ule mpango wa kufanya usafi kila mwisho wa mwezi bado upo?
Ni mambo yanayotokana na kukosa mfumo. Kwamba, mfumo umekuwa amri na si taratibu na mpangilio. Usafi umefilia mbali na kufeli bila kificho

Haya unayoona yanatokana na ukweli kuwa mfumo wetu upo upo na si mfumo kama mpangilio bali mfumo kama kundi, kikundi au mtu. Kila asubuhi tunashuhudia maanguko
 
Tatizo kubwa sana ninaloliona ni kwamba Rais wetu hana mpangilio katika kufanya kazi zake. kwa mfano, aliamua kushughulikia tatizo la vitanda katika Hospitali. Ni kweli vitanda ni tatizo kubwa na linahitaji ufumbuzi. lakini je, katika muktadha wa afya na matibabu, ukosefu wa vitanda ndio tatizo namba moja? uwepo wa vitanda utapunguza vifo katika hospitali zetu kwa kiwango kikubwa? maana kuna matatizo ya vifaa tiba, kuna matatizo ya madaktari na wauguzi, na juu ya yote kuna matatizo ya mfumo. mfano kama hospitali za chini zinaimarishwa, maana yake mrundikano utapungua Muhimbili.

Katika Elimu, pamoja na matatizo lukuki yaliyopo katika sekta hii: ubovu wa mitaala, matatizo ya walimu, nyumba za walimu, madarasa, maabara, madawati, na mengine mengi, yeye akakomaa na madawati. ni kweli ni moja ya matatizo, lakini je, linaweza kuleta mabadiliko makubwa, impact kubwa katika elimu kama likitatuliwa kwanza hilo?

Kukosa mpangilio kunakuja pia katika maamuzi. ana utaratibu wa kutoa maamuzi ya ghafla. bila mpango, bila bajeti. mfano mzuri ni hii amri ya Serikali kuhamia Dodoma. haijulikani kama kuna tathmini imefanyika kuona impact ya kuhamia ghafla namna hii.

Mwendo wa namna hii matokeo huwa baadaye ni kujikuta umesababisha matatizo mengi kuliko unavyoweza kuyakabili. JK alikuwa na kawaida ya kupaa kwenda majuu mambo yanapomzidia. Magu yeye atakuwa na kautaratibu gani ili angalau apumue? kutumbua majipu zaidi?
Mpangilio upo ila kipaumbele ndio kidogo shida na hii inatokana na nchi kuwa ktk uozo mwingi, si rahis uamue kuanza hapa tu.
 
Leo nimemuotea ndoto Raisi wako wanakula chakula na Yule rais wa Korea mwenye Kiduku daaaaaaaa sijui maana yake nini jamani???
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Tatizo kubwa sana ninaloliona ni kwamba Rais wetu hana mpangilio katika kufanya kazi zake. kwa mfano, aliamua kushughulikia tatizo la vitanda katika Hospitali. Ni kweli vitanda ni tatizo kubwa na linahitaji ufumbuzi. lakini je, katika muktadha wa afya na matibabu, ukosefu wa vitanda ndio tatizo namba moja? uwepo wa vitanda utapunguza vifo katika hospitali zetu kwa kiwango kikubwa? maana kuna matatizo ya vifaa tiba, kuna matatizo ya madaktari na wauguzi, na juu ya yote kuna matatizo ya mfumo. mfano kama hospitali za chini zinaimarishwa, maana yake mrundikano utapungua Muhimbili.

Katika Elimu, pamoja na matatizo lukuki yaliyopo katika sekta hii: ubovu wa mitaala, matatizo ya walimu, nyumba za walimu, madarasa, maabara, madawati, na mengine mengi, yeye akakomaa na madawati. ni kweli ni moja ya matatizo, lakini je, linaweza kuleta mabadiliko makubwa, impact kubwa katika elimu kama likitatuliwa kwanza hilo?

Kukosa mpangilio kunakuja pia katika maamuzi. ana utaratibu wa kutoa maamuzi ya ghafla. bila mpango, bila bajeti. mfano mzuri ni hii amri ya Serikali kuhamia Dodoma. haijulikani kama kuna tathmini imefanyika kuona impact ya kuhamia ghafla namna hii.

Mwendo wa namna hii matokeo huwa baadaye ni kujikuta umesababisha matatizo mengi kuliko unavyoweza kuyakabili. JK alikuwa na kawaida ya kupaa kwenda majuu mambo yanapomzidia. Magu yeye atakuwa na kautaratibu gani ili angalau apumue? kutumbua majipu zaidi?
Vyema sana lakn mambo yote haya hayawez kufanyika kwa siku1 inahitaji muda.
Zungumza na wenye maduka Kkko hadi Posta...
 
*Bongowood2017*
season 1-madawa ya kulevya..
season 2-vyeti feki vya paul makonda
season 3-mtoto feki wa gwajima
season 4-uvamizi clouds
season 5-Makonda chapa kazi
season 6-tume ya nape kufanya kazi
season 7-Napee kwishneyi
Season 8-Magazeti yamkera magufuli
season 9- Nape anyooshewa bastola
season 10- magufuli ana shoot scene mpya bandarini
season 11-Kinana anatumwa kutibiwa India
usikose season 12*
 
Uliona mbali sana Ngabu. Kila kitu sasa hivi ni vululuvululu!

Hahaaaa...halafu nahisi na bado!

Halafu nyumbu wa humu wanadai eti mimi ni pro-Magufuli kisa Usukuma!

Wakati Magufuli mwenyewe wala si Msukuma!
 
naona kaamua kumwachia bashite a run the show na maigizo yake
 
Mkuu inabidi uwe mtabiri mkubwa wa masuala ya kitaifa. Una upeo wa kuona mbali sana.

Thread zangu nyingi zinazomhusu Magufuli ziko spot on.

Jaribu tu kuzifuatilia na utaligundua hilo kiurahisi sana.

Nilizungumziaga uwezo wa Magufuli pindi tu alipopewa uteuzi na CCM...Julai 2015 kama sijakosea.

Na naamini nilikuwa sahihi tokea wakati huo.
 
Back
Top Bottom