KWA MAONI YANGU BINAFSI NA BILA KUFUNGAMANA NA CHAMA CHOCHOTE NAONA HII NCHI TUNAPOELEKEA SASA NI KUBAYA...
Ivi kwanini kila kitu cha wanasiasa wa upande wapili kinageuzwa uchochezi, sasa sio wanasiasa tena hadi raia wema wenye maoni na mawazo tofauti na utaratibu wa serikali ya sasa wanaitwa wachochezi, mbona mnaojiona waheshimiwa saana mmekuwa waoga hivyo, kuna yapi nyuma ya pazia?? Kumbukeni katika kundi la watu haiwezikani wote mkawa na mawazo au fikra sawa, tofauti lazma iwepo na Mwenye busara huheshimu tofauti hizo, huheshimu mawazo, fikra na maoni ya wengine bila kujali hadhi au nafasi yao katika jamii...sio kulazimisha kila kitu iwe ndio mzee!!
Nadhani mfumo wa vyama vingi uliletwa lengo kuu ikiwa ni kukuza demokrasia na pia kuondoa umwinyi wa chama kimoja, na kukipa ushindani na changamoto chama kitakachokuwa kinatawala ili viongozi waweze kuwajibika kikamilifu kabla ya chaguzi znazofuata, Nashangaa sasa mbona inakuwa hivi, Viongozi wetu mnalewa madaraka au??
Uhuru wa maoni upo wapi?? ...Acheni hzo uongozi ni dhamana hakuna wafalme bana wala miungu hapa tz, mie naamini inahitajika busara saana na hekima kuwaongoza watu wanaojielewa na sio mabavu wala nguvu na vitisho, mabavu yanamwisho wake!!
Hapa kutoa tu maoni yangu najua mtasema nachochea......Aaaah wapi mie no mtanzania naipenda nchi yang, naipenda familia yang inayonihitaji...ila sipend kabsa hii nchi mnapoipeleka nyie tunaowaita viongozi wetu na walinda amani..
Naamini ni haki yangu km mtanzania kusema hapana pale napoona mambo yanaenda sivyo, na kwenye haki yangu nitapambana had tonye la mwisho....Amina!!
HAYA NI MAONI YANGU BINAFSI NA WALA SIFUNGAMANI NA CHAMA CHOCHOTE!!