Hatuna mtu, lakini ili Tanzania mpya ipatiakane haina budi kuoza kwanza ndipo iote. Mimi ni mmoja kati ya wachache wanaoamini kuwa mwaka huu tutaanza kujiandaa kwa ajili ya uchaguzi mwingine. Sidhani kama ndani ya CCM watu watakua tayari kuona hali hii inaendlea.
Mbadiliko ya katiba ya CCM yanayolazimisha 'm/kiti' kugombea mhula wa pili bila kupingwa yanaeleza hoja yako.Hata ndani ya chama chake ukiangalia vizuri utaona nyuso nyingi tu za manung'uniko toka kwa wakereketwa. Wengi wao siku hizi wanashindwa hata kumtetea. Wapo kimyaaaa utadhani wagonjwa. CCM hawana furaha kabisa.
Now yuko very desperate, he was supposed to have someone on top of him kum-control huyu jamaa, bahati mbaya hata makamu wake hamuwezi
Hilo suala la rais ni taaisi ni kweli kabisa, lakini si wote wenye intelligence ya kutambua kuwa nafasi zao ni taasisi, ndiyo maana wanathubutu kujinasibu kuwa hawashauriwi na mtu kuhusu cha kufanya, kitu ambacho kinapingana na ninyi watetezi wake.Nyani Ngabu urais ni taasisi ukimuona rais anatoa maamuzi ujue information zote anazo
Nilikuwa nafanya editing, sasa ipo vizuri. Samahani kwa usumbufuMzee sijakupata hapo...ulitaka kusema nini?
Upigwe bani wewe kwani unadhani kila kitu ni ushabiki badala ya kungalia factRais ni Magufuli na ataendelea kuwa magufuli. huko anakopita ni shangwe na vigelegele. wananchi wanatamani aseme neno roho zao zifrahi. huku mko busy kutunga ngonjera na hadithi zisizo na vichwa wala miguu......
Subiri Jingalao na MOTOCHINI waisome post yako utakoga matusi.
Huko kunatakiwa kusifu na kuabudu tu
Hoja yako kwamba CCM haina raha, ina ukweli. Na upande mwingine umebaini huenda kukatokea 'kupingwa'Mzee sijakupata hapo...ulitaka kusema nini?
kweli kabisaMimi ni mmoja wa watu wanaoamini kuwa rais wetu huyu, mheshimiwa mtukufu Dkt. John Pombe Joseph Magufuli si kiongozi mzuri hata kidogo, hususan katika ngazi ya urais.
Hilo nimekuwa nikilisema kwa muda mrefu sasa. Nakumbuka hata ile siku alipoteuliwa kuipeperusha bendera ya CCM nilisema hivyo humu humu JF.
Kwa kiasi fulani namkubali kwenye usimamizi lakini si kwenye uongozi. Hana kabisa haiba ya kiuongozi. Pia hana sifa za kuweza kuwa kiongozi mzuri.
Ni mtu mwenye jazba. Ana jeuri. Mwenye kuongea bila kufikiria athari za maneno yake[nyakati zingine]. Wengine wanasema eti kuwa hashauriki. Kwa ufupi ni mengi sana yanasemwa juu yake kiasi kwamba mengine ni vigumu kwa watu wa mbali kama sisi kujua kama ni ya kweli au la. Hivyo kwa sisi wa mbali tunaenda na yale tuyaonayo na tuyasikiayo toka kwake yeye mwenyewe.
Sasa kwa jinsi vile mambo yanavyoenda sasa hivi kuna kila dalili huenda nchi imeshamshinda kuiongoza. Hivyo ndivyo niuonavyo mwelekeo.
Hata ndani ya chama chake ukiangalia vizuri utaona nyuso nyingi tu za manung'uniko toka kwa wakereketwa. Wengi wao siku hizi wanashindwa hata kumtetea. Wapo kimyaaaa utadhani wagonjwa. CCM hawana furaha kabisa.
Naamini asipojiangalia na kujifanyia tathmini basi hiyo kazi itamshinda kabla hata hajafikia nusu ya muhula wa hii miaka mitano.
Niliwahi kuandika kuhusu 'a police state'. Jikumbushe....
https://www.jamiiforums.com/threads/a-police-state.1105346/#post-17414170
yaan kama hii ya kuonyeshana mguu wa kuku, huku zanzibar chochoro zote mji mkongwe ni nape na bastolaUkipita mitaani watu washachoka na story zake...
biashara haziendi.....mood iliyopo ni kusubiri labda mambo yatanyooka soon...
sasa sijui yasiponyooka itakuaje....