Rais Magufuli, vunja vunja Wizara hii katika uchapakazi wako Ikulu

KooZito

JF-Expert Member
Dec 14, 2020
396
1,377
Baada ya ukimya na kutoonekana kwa JPM kama ilivyo kawaida yake, Waziri Mkuu Kasim Majaliwa amewatoa hofu Watanzania, "Rais ni mzima bukheri wa afya na anachapa kazi Ikulu".

Naye Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan akasema, "nchi iko salama, tushikamane kuliko wakati wowote."

Kwa kauli hizi ninaamini Mkulu yuko bize Ikulu akipiga kazi kama ilivyo slogan yake "hapa kazi tu".

Kama mwananchi wake namshauri katika hizo kazi anazochapa basi aivunje Wizara ya Afya, Jinsia, Wazee na Watoto. Hii wizara ni kubwa mno.

Napendekeza, kutokana na unyeti wa suala la Afya, Afya ibaki peke yake na Waziri wake. Hayo mengine yabaki kama Wizara ya Jamii.

Popote duniani wizara ya Afya ni sekta nyeti mno. Vita hii ya Covid-19 imethibitisha unyeti wa wizara hii. Ni vigumu yule mama kujigawa kushughulika na afya na hapo hapo ashughulike ni wazee, kina mama na watoto. Tunaweza kuona alivyofeli kuongoza wizara hii lakini kimsingi ni ukubwa na upana wake.

Hizo kazi unazochapa Ikulu, chapa na hili. Ahsante.

Au nasema uongo ndugu zangu!
 
Embu tucheze kamali kidogo tujue huyu mzee yupo kweli au hayupo

Roma ampitie Lissu hapo Brussels waje tuangalie kama nyumba haina mwenyew. Ni mtazamo
 
Wizara kubwa wapi,hizo ni fikra za uvivu.nchi yenyewe bado Ina pop.mil 60+,je ingekuwa bil 1+ Kama China!!
 
Wizara kubwa wapi!? Hizi ni fikra za uvivu na ulegelege.nchi yenyewe pop.mil 60+ ndo unasema wizara kubwa,je pop ingekuwa bil.1+Kama China ungesemaje!?
 
Ukitaka kumtesa Mtanzania, mnyime Habari anayotaka kuisikia kwa hamu na shauku kubwa. 😁😁😁 ni mtazamo tuu msikasirike washkaji
 
Back
Top Bottom