Rais Magufuli, Punguza confrontation na Wazungu

Rais Magufuli, Punguza confrontation na Wazungu

wazungu wapuuzi tu wacha tuwanyooshe
Una ubavu wa kuwanyoosha?? Kumbuka budget yako nusu inatoka kwao halafu unongea upupu? Subiri ndugu zetu wa ukimwi wakianza kupukutika kwa kukosa madawa maana Trump kakata ndo mtajua, si hiyo tu chanjo ngapi tunategemea wafadhiri? Ushukuru kama huna watoto na hutegemei kuwa nao au mke basi ongea.
 
Acheni uoga. Huyo mnayemuogopa mtaji wake mkubwa ni kuwatia uoga na mafanikio yake makubwa ni pale mnapomuogopa.

Badala ya kumuambukiza Rais uoga mtieni moyo. Muungeni mkono. Kuweni naye sambamba. Mkifanya hivyo mtafanikiwa, hakuna wa kuzuia mafanikio ya watu jasiri.
 
Ni suala la stratejia na mbinu stahiki. Ni kweli wazungu wanaishi kwa kunyonya mataifa masikini. Lakini tutaendelea kuitikia "hewala bwana" mpaka lini. Inabidi kuanzia mahali. Sidhani lengo la Magufuli ni kugombana na wazungu bali anajitahidi kuona kama TZ itaweza kupata a fair deal kwenye madini yetu badala ya kubakia kulalamikia mashimo baada ya migodi kufungwa.
Halafu utayauzia wapi kama utakataa ku-negotiate nao? mtoa mada yuko sahihi kwa asilimia 100%. Ndio maana kikwete alisema ukitaka kula na wewe uliwe. Unadhani yeye hakuwa akijua kwamba wazungu wanatula? Kawaulize Zimbabwe walipochukua ardhi yao na mali yao. Wamekuwa Blacklisted na Taasisi zote kupata mikopo, si WB, IMF, IFC, IDA, nk. Hao watu waitwao wazungu wasikie tu lakini wanatisha kuliko njaa.
 
Lazima wakuadhibu!Mnakubali vipi kuingia mikataba halafu baadae mnawageuka?Unadhani nani anaweza kukubali kudhulumiwa namna hii?
Unakubaliana nani,nawekeza mabilioni kwenye miundo mbinu ya mgodi,halafu ghafla unasema mmeshtuka?Kwa nini hamkushituka kabla ya kusaini?
Ni sawa na mtu kuposa mke,akaandaa arusi kubwa,akatoa mahari kubwa,halafu wakaishi na mume muda mfupi,kisha baba mkwe anaanza kudai malipo ya ziada kwa vile mwanae ni mzuri sana.Kama mume hataki,basi amuache!!Nyie ni wehu?Kwa nini mlikubali hapo awali?Mtachezea kichapo sana na wameshaanza kutokea Malawi
 
WaTz kinachotusumbua ni unafki , tunalia na wazungu wakati tuliopaswa kuanza nao tunao humu humu ndani. Wazungu si wadhambi katika hili, tunaye Mkapa na Kikwete pia waliokuwa mawaziri wao wa madini, wana sheria wao wakuu, makamishina wao wa madini etc . Hawa watu bado wapo hai wote , tuanzie nao, waperekwe Mahakamani kama tunataka kuwa wakweli ktk suala hili.

Na bunge letu chama kimeking'oa meno na hapo ndipo penye shida, hebu angalia 2015 bunge hapa liliperekeshwa mpaka usiku wa manane ili tu wapitishe sheria ya hovyo ya Mafuta na Gesi ili Kikwete atoke amesaini. Hawa watu(Kikwete na Mkapa) tunawaona ni mashujaa tunawalaumu wazungu kweli ?!!. Huu ni unafki wa mTz.
 
Hapa kuna mambo mawili
1.Tuko sahihi kulinda rasilimali zetu

2.Uoga wetu ndio umasikini wetu.

Mapinduzi pekee yenye kubadili maisha na vizazi ni Mapinduzi ya fikra. ...mara nyingi inasikitisha watu wengi wanapokuwa na fikra mfu.

Lazima tubadili namna tulivyokuwa tunafanya mambo ili kupata matokeo tofauti.

Uoga haijawahi kumsaidia mtu yeyote kubadili hali aliyonayo. ...kama uanogopa njaa. ..fanya kazi

Kama unaona unaibiwa fanya maamuzi
 
wazungu wapuuzi tu wacha tuwanyooshe
Tunawanyoosha wazungu? Kivipi? Nchi inaeleekea kufirisika tunalia bajeti imegoma kufikia hata 35% kisa wazungu wamegoma kutoa misaada leo unasema Tunawanyoosha! Tuko wote wewe au? Tumeshaingia shimoni.....mwaka huu pia tusipopewa kwisha habari!!!! Bandari imebakia ku export tu michanga....hakuna mzigo pale mapato hakuna!!!! Subiri ifike dec utaniambia!! Ipo siku watu watakimbia nchi maana hata mishahara watakopa!!!
 
Hapa hujatumia akili ya kichwan hata kidogo. Umetumia ya kwenye makalio. Kufikiria unaweza wewe mtanzania kuwanyoosha wazungu ni kujidanganya kwa kiwango cha phd kabisa. Angalia ambao walitaka kunyooshana na wazungu na wao uwezo walikuwa nao acha sisi ambao bajeti yetu inategemea kwao.angalia miradi mingi ujenzi au uendeshwaji wake pesa zatoka wapi.

Ukiwekewa vikwazo hizo dhahabu utatengenezea shanga tu uwe unavaa kwa mumeo maana soko nje hutopata. Ni kuishi nao kwa akili coz wametuzidi kwa akili na tunapo deal na mikataba yao tusiwe na mzuka au mihemko itakuja kutugharimu. Rais yeye maisha yataenda kama kawaida. Shida kwa wwe mlalahoi utaona maisha yanavyokuwa magumu.

Hizi hoja unatakiwa kutumia ubongo kujadili siyo makalio na tumbo. Ukitumia hivyo utaandika uchafu tu au waste product ya chakula.

wazungu wapuuzi tu wacha tuwanyooshe
 
Kinacho ikuta Zimbabwe ni picha tosha, Zimbabwe ilikuwa inaifuatia South Africa kwa uchumi mkubwa na ilokjwa kama ya 4 au 5 Africa ila kwa sasa no historia. wana ukosefu wa Ajira wa 98%

Wazungu ndo wanamiliki IMF, World Bank na kadhalika wanauwezo wa kufanya hii pesa yetu ukienda nayo sokoni Sh 10,000 ununue nayo pipi moja tu, Hahaaa Kilo ya nyama yaweza kuwa Laki 5
 
Mleta mada una akili sana wanaomshakia rais kwa hili siwalaumu kwakuwa hili jambo linataka uelewa, yeye anahangaika lakini wenzie waluopita waliijaza hiyo mikataba kwa mbwembwe sasa badala ya kuhangaika na mikataba anahangaika na wazungu ambao wanadocuments za mihur ya chuma ya ikulu yetu na sahihi za marais, mawazir wa nishati na madini waliopita! Wala hatuambii mikataba inasemaje anaishia kutuambia nchi inaibiwa lakini hasemi insibiwaje na ni nani alieruhusu wizi huo, sasa anabaki kuota na kukimbizana na makontena bandarini hivi hajiulizi yamefikaje barini kutoka huko migodini ambako ni mamia ya kilometa?

Watamkomesha kwa kukomesha watz mfano, enzi za ukolon nyerere alipotaifisha mashamba ya katani wazungu walioganaizi katani isinunuliwe huko walikokuwa wanauza goma likamdodea na likatudodea wote kumbuka hii ni enzi za ukoloni sasa je kuhusu hii mikataba iliosainiwa na marais wetu na maeazir tukiwa huru? Namuomba magufuli aanze na yale makaratasi ya mikataba na ikiwezekana awaite waliosaini ili wazungumze kabla ya kuwaparamia hao wazungu
 
Hayo ni mawazo ya kizamani mno, omukama ntale alikuwa akitembelea kijiji fulani anauliza nani anamke mzuri akija unampisha mkeo analala nae na kesho unamzawadia ngombe, sisi sio wa enzi ya omukama ntale.
 
KTK VYOTE NAOGOPA SANA NCHI YETU KUFIKIA ILIPO ZIMBABWE MUNGU TUONGOZE
 
Una ubavu wa kuwanyoosha?? Kumbuka budget yako nusu inatoka kwao halafu unongea upupu? Subiri ndugu zetu wa ukimwi wakianza kupukutika kwa kukosa madawa maana Trump kakata ndo mtajua, si hiyo tu chanjo ngapi tunategemea wafadhiri? Ushukuru kama huna watoto na hutegemei kuwa nao au mke basi ongea.
Hiyo bajeti nusu "inayotoka" kwao ukiicheki kwa undani zaidi unakuta ndo ile inayobebwa kwenye makontena eti ni mchanga, mzungu hakupi kitu bure hata siku moja kila kitu ni kwa faida yake!
 
Ni suala la stratejia na mbinu stahiki. Ni kweli wazungu wanaishi kwa kunyonya mataifa masikini. Lakini tutaendelea kuitikia "hewala bwana" mpaka lini. Inabidi kuanzia mahali. Sidhani lengo la Magufuli ni kugombana na wazungu bali anajitahidi kuona kama TZ itaweza kupata a fair deal kwenye madini yetu badala ya kubakia kulalamikia mashimo baada ya migodi kufungwa.
Sawa lakini ni lazima kujiandaa kikamilifu na negative repercussions na haya ndio mazingira ya hofu ya mleta uzi.
 
Mfano mzuri ni nchi ya Zimbabwe, baada ya Rais Mugabe kuwanyanganya mashamba leo hali ya uchumi wa nchi hiyo imekuwa mbaya sana, mfano mwingine ni Venezuela baada ya hayati Hugos Chaves aliyekuwa Rais wa nchi hiyo kutaifisha makampuni ya mafuta leo hii nchi hiyo pamoja na utajiri wa mafuta maandamano kila siku kutokana na hali mbaya ya uchumi, hawa wazungu walishusha bei ya mafuta kutoka dola 110 mpaka dola 50 ikawa ni vigumu kwa serikali ya Venezuela kuendelea kutoa huduma ilizokuwa inazitoa kwa wananchi wake
Mfano mkubwa ni wa hapa hapa Tanzania baada ya Azimio la Arusha mwaka 1967 Rais wa awamu ya kwanza alitaifisha makampuni, mashamba, viwanda za hawa wazungu kilichofata walituhujumu kiuchumi mpaka Mwalimu aliamua kuondoka madarakani mwaka 1985. Chukua mfano mzuri hawa majirani zetu wa Kenya walivyopiga hatua kwa kuwa na ushirikiano na hawa wazungu. Tatizo ambalo serikali ya awamu ya tano iliyorithi ni mikataba mibovu iliyosainiwa na serikali ilizotangulia ambazo inatambuliwa kimataifa.
Asante sana kwa mchango maridhawa.
 
Back
Top Bottom