Rais Magufuli na Libya

Rais Magufuli na Libya

Utakula huo Uhuru?

Uhuru ndio utajenga barabara na kuhakikisha watoto wote wanaenda shule na kupata elimu bora? Uhuru ndio utaleta madawa hospitalini?

Ingekuwa hivo nchi za kiafrika zisingekuwa hapa kimaendeleo miaka zaidi ya 50 tangia zilipoanza kupata Uhuru.
Wewe una akili ndogo(Sina nia yakukudhalilisha )

Where there is freedom there are all elements of full or partial development.

Bila uhuru utajenga hiyo barabara saa ngapi?

Bila uhuru hao watoto hata wakilipiwa ada wanaendaje shule? Kama hawapo huru wataelewa nini?

Bila uhuru ni wakulima wapi watalima na kutegemea kuvuna baada ya muda flani?

Think again,
 
Kuna walibya WALIPOULIZWA Kwanini wanataka Gaddafi aondoke walijibu kuwa wanapenda demokrasia zaid. Wazungu wakasema shwari. Walibya wakasaidiwa kumtoa Gaddafi madarakan, tena kwa aibu kubwa. Kilichofuata ndo kama tunavyoona. Hakuna maendeleo wala demokrasia. Hakuna Uhuru wala fursa. Yaliyobaki ni majuto. Libya imevurugwa
Heri maskini huru kuliko tajiri mtumwa!
 
Nini maana ya dikteta? Vigezo gani vinavyotumika kumwit gadafi dikteta? Je kukaa madarakani muda mrefu ni udikteta?
Kuna waswahil kila kitu kinachosemwa na wazungu wanaamini hata kama hakipo
 
Halafu hili wala hatukumohoji.....ndo hasara ya kuchagua Rais bila debates wala kuhojiwa

Rais sasa ghafla kawa kama 'mtu mpya'

kila anachoongea tunabaki tunashangaaa

mara matuta ondoa
mara vyakula vya wenye njaa marufuku
mara wagonjwa walipie huduma
 
Ninacho amini mimi gadafi hakuwa dikteta ila ni propaganda tu za wazungu ili kumchafua na ilivaounekani hafai
Raisi dikteta ni yule asiye sikiliza raia wake wanataka
Rais dijteta ni watu wenye kujikusanyia mali nyingi wawapo madarakani ila gadafi alitumia pamoja na wananchi wake
Huo udikteta wake upo wapi?????????
Alikuwa akiwapinga wazungu wazi wazi nani leo rais wa afrika anayeweza kufanya hivyo ndio maaana walimchukia na kumpaka matope kidogo mzee wetu mugabe anaweza kuongea
Sasa udikteta wa gadafi upo wapi acheni kulishwa sumu na wazungu mkiamini wapo sawa
Na dunia hii hakuna dikteta mbaya zaidi ya mzungu
 
Utakula huo Uhuru?

Uhuru ndio utajenga barabara na kuhakikisha watoto wote wanaenda shule na kupata elimu bora? Uhuru ndio utaleta madawa hospitalini?

Ingekuwa hivo nchi za kiafrika zisingekuwa hapa kimaendeleo miaka zaidi ya 50 tangia zilipoanza kupata Uhuru.
Hivi Afrika kusini kwa vile zilijengwa barabara nzuri,hospitali nzuri ,shule, vyuo vikuu, na vingine vingi tu kuliko mahali pengine Afrika kudai uhuru hakukuwa na maana?
 
Cha muhimu tupate mtu kama Gaddafi. Aweze kutumia rasilimali za nchi kututoa hapa tulipo kama Gaddafi alivyo fanya kwa libya. Magufuli anaonekana anaweza. Tumpe muda.
Wa tz hawaja liona hilo tumezowea kupinga hadi ukweli
 
Wa kusema na kuchagua wanayemtaka na hicho ndicho kinachofanyika hapa nyumbani Ref. Zanzibar
Mataifa gani raia wana uhuru wa kusema vyovyote wanavyotaka? Kwa taarifa yako voting haiwezi kufanya mtu kuwa kiongozi wa nchi bila ya vetting
 
Gaddafi alimsaidia Iddi Amini awaue watanzania leo tunamtetea mbona tunakuwa wasahaulifu
 
Mataifa gani raia wana uhuru wa kusema vyovyote wanavyotaka? Kwa taarifa yako voting haiwezi kufanya mtu kuwa kiongozi wa nchi bila ya vetting
Kwa kauli zako basi sisi waTz na wa Africa tunapotezewa muda na chaguzi zisizo real
 
Maisha ya kupewa bure tu sio maisha.
Hakuna ajira .
Zilizopo wanapewa watu kutoka sirte nyumbani kwa gadafu.
Nilikaa na wa libya ...nikamuuliza kuhusu hili..imekuwaje mkamuondoa gadafi wakati kila kitu. Na huku Afrika tunamuina mtu wa maana? mnapata? Akanijibu kuwa ni kiini macho tu. Pesa zikigaiwa ni mfano wa rushwa. Mtu unakosa maendeleo binafsi walibya walibaki omba omba kusubiri ration ya bure.
Na walofaidi ni kabila lake zaidi.
Akasema fedha nyingi watoto wake walificha nje.
Na yeye kupoteza fedha nyingi kujijenga kwa mataifa ya afrika kwa kuwalipia hata fees za AU
Kuwasaidia pesa nyingi bila ya mtu kuhoji
Walibya walikua gerezani...
Wanakula cha kugaiwa na wamejianamia
Hao uliokaa nao wakakwambia hivyo leo hii kawaulize tena wanaonaje maisha kipindi cha Gadaffi na sasa?
Ni kawaida ya binadamu kuona alicho nacho sio bora akatamani asichokuwa nacho mpaka kile alichokuwa nacho kikimponyoka ndipo huona umuhimu wake.
JK si alitukanwa sana akaitwa dhaifu na wapinzani na watanzania wengi, lakini sasa wanamtamani.
Same applied to Gadaf na Magu muda wake ukiisha atasifiwa.
 
Hiyo mifano kwa nini asiitoe kwa south Africa ambayo ilikumbatia ubaguzi mpaka wakasababisha maafa kama anavyofanya yeye ubaguzi?
Waafrika ni watu wa ajabu sana. Afrika kusini imefika hapo ilipo kwa sababu ya udikteta wa makabulu. Leo hii waafrika wenyewe wanapoamua kutumia udikteta japo kwa kipindi kifupi ili kuinyoosha nchi na mambo yaende watu wanaona wanaonewa. Tanzania ilipokuwa imefikia ilihitaji mtu mkali kidogo ili arekebishe mapungufu yaliyopo, aweke misingi mizuri ya nchi ndiyo mambo mengine yafuate. Inawezekana Magufuli ndoto yake kubwa ni kuifanya Tanzania iwe kama Libya ya Gadafi! Tumpe muda afanye anachotaka kwa sababu anadhamira ya dhati na Tanzania. Huu ukata na mambo mengine yanayojitokeza ni kwa sababu anajenga msingi wa kuiongoza Tanzania, ndio maana watu wanakua katika mgumu. Kwa kifupi tumpe muda na tumruhusu aendelee na kuishape Tanzania anayo itaka baadae mambo mengine yatafuta kiulaini tu.
 
Wakati mwingine unaweza kuwa mtu wa aina fulani lakini ukakosa sifa kutokana na kile unachokitetea. Ngabu unahoja dhaifu, hoja ambayo huwa naifananisha na nyimbo za mipasho. Umekuwa mmoja kati ya wenye kuziba macho na kujitia upofu hata pale linapofanywa jambo lililosahihi. Umekuwa na hulka ya kujifanya unajua kila kitu lakini hutambui kuwa hujui. Mwana Africa yoyote asiyetambua kile alichokifanya GADAFI katika uhai wake na kile kinachoendelea baada ya kuondoka kwake Ni muongo na mtu wa kuogopwa

Unafki hausaidii katika kutafuta kilicho cha kweli. Mipasho kama hii haipaswi kuandikwa na wewe. lakini kwa kuwa umekuwa muimbaji wa taarab endelea kutawala jukwaa ipo siku utapata ufalme kama sio umalikia. TANZANIA NI YA KWETU
It is of my opinion, hii ndio mipasho as opposed to hoja aliyopost NN.
Uje na hoja fafanuzi kuonesha ni wapi mtoa mada hajasema ukweli!
 
Waafrika ni watu wa ajabu sana. Afrika kusini imefika hapo ilipo kwa sababu ya udikteta wa makabulu. Leo hii waafrika wenyewe wanapoamua kutumia udikteta japo kwa kipindi kifupi ili kuinyoosha nchi na mambo yaende watu wanaona wanaonewa. Tanzania ilipokuwa imefikia ilihitaji mtu mkali kidogo ili arekebishe mapungufu yaliyopo, aweke misingi mizuri ya nchi ndiyo mambo mengine yafuate. Inawezekana Magufuli ndoto yake kubwa ni kuifanya Tanzania iwe kama Libya ya Gadafi! Tumpe muda afanye anachotaka kwa sababu anadhamira ya dhati na Tanzania. Huu ukata na mambo mengine yanayojitokeza ni kwa sababu anajenga msingi wa kuiongoza Tanzania, ndio maana watu wanakua katika mgumu. Kwa kifupi tumpe muda na tumruhusu aendelee na kuishape Tanzania anayo itaka baadae mambo mengine yatafuta kiulaini tu.
Acha kudanganya watu wewe
 
Utakula huo Uhuru?

Uhuru ndio utajenga barabara na kuhakikisha watoto wote wanaenda shule na kupata elimu bora? Uhuru ndio utaleta madawa hospitalini?

Ingekuwa hivo nchi za kiafrika zisingekuwa hapa kimaendeleo miaka zaidi ya 50 tangia zilipoanza kupata Uhuru.
Hujajua maana ya uhuru bado
 
Back
Top Bottom