Hivi ilikuwa yule Saddam Hussein Rais wa Kuwait au LibyaHuwa anaongelea na Iraq pia...
Nambie saiv wana ubora gani unafuu gan wameupata baada ya kifo cha gadafi?? Unapaswa kuelewa Magufuli anacho maanishaNi mara kadhaa sasa nimemsikia mtukufu rais Dkt.John Pombe Joseph Magufuli, akiwa anazungumzia suala la amani, akiitolea mfano nchi ya Libya kipindi cha Gadafi.
Kwamba mambo huko Libya yalikuwa safi tu. Vijana waliokuwa wanaoa walipewa hela, nyumba, na mengineyo.
Inawezekana kweli walikuwa wanapewa hivyo vitu lakini je, walikuwa wako huru kiasi gani?
Gadafi alikuwa dikteta. Tena dikteta mkubwa tu aliyeng'ang'ania madaraka kwa muda mrefu sana hadi walipomfurumsha.
Mtukufu rais Magufuli naye watu wengi wameshaanza kumwona kuwa ni dikteta. Hataki watu wafanye siasa kwenye maeneo yasiyo yao.
Tumeshaona na kusikia watu wakikamatwa na kufunguliwa mashitaka kwa makosa ya kumtukana/ kusema maneno mabaya dhidi yake.
Tumeona vyombo vya habari vikifungiwa kwa sababu zisizo na mashiko.
Sasa haya mambo ya yeye kuisifia Libya ya Gadafi mimi yananitatiza.
Nabaki najiuliza maswali tu. Ina maana yeye Magufuli alikuwa anamwona Gadafi kuwa ni kiongozi bora aliyeweza kutunza amani huko Libya hadi awe anaisifia sifia hivyo?
Kama Gadafi ndo mmoja wa viongozi ambao Magufuli anawaona kama mfano mzuri wa utunzaji wa amani, watu wakimwona na yeye dikteta watakuwa wanakosea kweli?
Ndo mambo ya ndege wafananao hayo au..?
Hivi wewe ukichukuliwa ukawekwa jela na ukalishwa kila aina ya chakula unachotaka je utafurahia ayo maisha ya kifungoni ( bila uhuru)Pamoja na mapungufu yake, maisha yalikuwa nafuu sana kipindi cha Gadafi kulilo ilivyo sasa, hilo wala si jambo la kujadiliana. Hata hao waliovamia wanapata wakati mgumu maana hawakujua hali ingekuwa kama ilivyo sasa. Better the devil you know...
Unampangia ase3 wapi na wapi asisemee?Hiyo mifano kwa nini asiitoe kwa south Africa ambayo ilikumbatia ubaguzi mpaka wakasababisha maafa kama anavyofanya yeye ubaguzi?
Basi kama mtukufu anamuona Gaddafi alikuwa poa sana ni vizuri nae akitupeleka kuwa kama nchi ya Libya tupewe kila kitu yeye awe mtawala wa milele kama Gaddafi na baadae tuje kuwa kama Libya.Kuna walibya WALIPOULIZWA Kwanini wanataka Gaddafi aondoke walijibu kuwa wanapenda demokrasia zaid. Wazungu wakasema shwari. Walibya wakasaidiwa kumtoa Gaddafi madarakan, tena kwa aibu kubwa. Kilichofuata ndo kama tunavyoona. Hakuna maendeleo wala demokrasia. Hakuna Uhuru wala fursa. Yaliyobaki ni majuto. Libya imevurugwa
Kifupi ni kwamba Mheshimiwa huwachukulia Muammar Ghadaffi na Saddam Hussein kama 'role models' wake. Anawasifia na kuwarejea kila anapoongelea suala la amani. Kwake amani huletwa kwa 'fimbo ya chuma'. Na kwake uhuru na amani ya nafsi si mambo ya msingi sana kama mtu anapata 'huduma muhimu'. Kifupi ni kwamba kwa mtazamo wake mtumwa ambaye 'bwana' wake anamhudumia kwa mavazi, malazi na chakula ni bora kuliko mtu huru anayehangaika kupata mkate wake wa kila siku kadiri anavyojaaliwa.Ni mara kadhaa sasa nimemsikia mtukufu rais Dkt.John Pombe Joseph Magufuli, akiwa anazungumzia suala la amani, akiitolea mfano nchi ya Libya kipindi cha Gadafi.
Kwamba mambo huko Libya yalikuwa safi tu. Vijana waliokuwa wanaoa walipewa hela, nyumba, na mengineyo.
Inawezekana kweli walikuwa wanapewa hivyo vitu lakini je, walikuwa wako huru kiasi gani?
Gadafi alikuwa dikteta. Tena dikteta mkubwa tu aliyeng'ang'ania madaraka kwa muda mrefu sana hadi walipomfurumsha.
Mtukufu rais Magufuli naye watu wengi wameshaanza kumwona kuwa ni dikteta. Hataki watu wafanye siasa kwenye maeneo yasiyo yao.
Tumeshaona na kusikia watu wakikamatwa na kufunguliwa mashitaka kwa makosa ya kumtukana/ kusema maneno mabaya dhidi yake.
Tumeona vyombo vya habari vikifungiwa kwa sababu zisizo na mashiko.
Sasa haya mambo ya yeye kuisifia Libya ya Gadafi mimi yananitatiza.
Nabaki najiuliza maswali tu. Ina maana yeye Magufuli alikuwa anamwona Gadafi kuwa ni kiongozi bora aliyeweza kutunza amani huko Libya hadi awe anaisifia sifia hivyo?
Kama Gadafi ndo mmoja wa viongozi ambao Magufuli anawaona kama mfano mzuri wa utunzaji wa amani, watu wakimwona na yeye dikteta watakuwa wanakosea kweli?
Ndo mambo ya ndege wafananao hayo au..?
Mzee Karume Zanzibar,alitujengea hadi jengo la Club ya YangaMleta uzi unataka Rais magufuli atolee mfano nchi gani zaidi ya Libya hapa afrika? Libya ni mfano mzuri wa nchi ya kiafrika iliyo tumia rasilimali zake bila misaada kunyanyua maisha ya wananchi wake
Kuna mfano bora kama huo hapa afrika? Mi siuoni
Hizi kauli zako haziwezi kufanya kazi hata hapo Rwanda. Sio kila kitu kwa lugha ya kiingereza kinafaa katika kuwakilisha hoja yako, bali mifano ya mazingira halisi ndo inasaidiaHivi wewe ukichukuliwa ukawekwa jela na ukalishwa kila aina ya chakula unachotaka je utafurahia ayo maisha ya kifungoni ( bila uhuru)
View attachment 392762
kwa hiyo wewe utakula udikteta?Utakula huo Uhuru?
Uhuru ndio utajenga barabara na kuhakikisha watoto wote wanaenda shule na kupata elimu bora? Uhuru ndio utaleta madawa hospitalini?
Ingekuwa hivo nchi za kiafrika zisingekuwa hapa kimaendeleo miaka zaidi ya 50 tangia zilipoanza kupata Uhuru.
Yes, hao ndio huwarejea kila mara kama role models wake...na sisi tunapiga makofi kwa kutumia kumshangilia!
!
labda model wake ni waina hii....Akina Sadam wa Iraq , akina Gadaffi wa Libya, akina Asad wa Syria.
Kwani hadi Gaddafi anakufa, hizo moroko na Algeria zilikuwa ni tajiri kuliko Libya? Acheni hayo maneno kabisa, maana hata moroko ilikuwa ni nchi ya kifalme na Algeria iliongozwa na rais boutfikra kwa kipindi kirefu...someni historia mueleweGadafi alikuwa ni dikteta wa kutisha.Watu kuuwawa katika mazingira ya kutatanisha ilikuwa ni kawaida mnoo wakati wa Gadaffi.Ukiwa mpinzani wa Gadaffi ata ukiwa nje ya Libya alikuwa anakutumia majasusi wakumalize.
Gadafi alikuwa ana bahati Libya ina utajiri mkubwa wa mafuta.Ndio maana aliweza kutoa huduma nyingi za kijamii bure.
Libya ingekuwa na utawala wa kidemokrasia tangu enzi za Gadaffi ingekuwa ni nchi tajiri kuzidi Morocco na Algeria.
Siku zote unapomg'oa dikteta unaacha ombwe la uongozi kwa maana uongozi wote unakuwa umeteuliwa na mtu mmoja na sio na wananchi.
Lakini imevurugwa kwa kiwango gani.. Unaweza kutoa takwimu za hivi karibuni?Kuna walibya WALIPOULIZWA Kwanini wanataka Gaddafi aondoke walijibu kuwa wanapenda demokrasia zaid. Wazungu wakasema shwari. Walibya wakasaidiwa kumtoa Gaddafi madarakan, tena kwa aibu kubwa. Kilichofuata ndo kama tunavyoona. Hakuna maendeleo wala demokrasia. Hakuna Uhuru wala fursa. Yaliyobaki ni majuto. Libya imevurugwa