Heshima kwenu wakuu,
Juzi rais alipotutembelea huku kwetu Kagera, rais Magufuli alijinasibu kwamba yeye ni Muyango yaani "abayango" hujiita Wazilankende. Akadai babu yake alizikwa pale Bukoba mjini Sehemu inaitwa Uswahilini pale karibu na Sanamu la Mayunga. Jina la babu yake limenitoka nikikumbuka ntaedit niweke hapa ila ni kama alisema aliitwa Mzee Mshalila(?).
Huyu mzee Mashalila alizaa watoto watatu, bahati mbaya hawa watoto wapo hadi leo sema akili zao hazipo sawa. Wapo Uswahili pale Bukoba Mjini.
Kwa wasiofahamu sifa ya Wazilankende ngoja nifafanue kidogo. Nkende ni ngedere, sasa hawa wazilankende ni marafiki wa ngedere. Yaani hata akimuona ngedere barabarani inatakiwa awabebe ndizi. Akikuta ngedere amekufa inabidi alie au anaumwa inabidi amtibie. Hao ndo wazilankende.
Hata ukiangalia kwenye hotuba ya Mbunge wa bukoba mjini Mh. Lwakatare wakati anamkaribisha alisema karibu nyumbani Mzilankende "wayanga waija" hatimaye umekuja(kwa tafsiri isiyo sahihi.).
Ndugu zake rais Magufuli waliopo Bukoba ni Oscar Mashalila, Dotto Mashalila watatu nmesahau jina la mtoto wa tatu, sema ni maarufu tu mjini japo hapo sawa.
Huo ulikuwa ni utangulizi. Swali langu ni;
Rais Magufuli ni nani?
1. Mzilankende
2. Msubi,
3. Msukuma
Au Muyango?
Kusema kweli mtakuwa mumenaidia sana.