Kwa taarifa yako kinachomuumiza binadamu yoyote ni ukweli, hivyo ukweli usemwe na mtu unayemuona au mwenye fake I'd bado unabaki kuwa ukweli. Mfano mrahisi, rais kila akikaa hadharani anasifiwa ile mbaya, ila huku jukwaani kuna wachache wanampa ukweli wake, huo ukweli wa fake I'd unamuumiza kuliko hizo sifa lukuki huko mtaani. Rejea udukuaji wake wa mawasiliano ya kina Makamba, maongezi yale yalimuumiza kuliko sifa za kinafiki anazopewa akiwa hadharani. Ukitaka kupata maoni halisi na ya kweli ya watu kuhusu ww, weka suggestion box, na sio kuitisha kikao cha face to face.