Rais Magufuli, katiba mpya, na Umoja wa Mataifa

Rais Magufuli, katiba mpya, na Umoja wa Mataifa

Lugha ndio kigezo cha kuhudhuria mkutano wa umoja wa mataifa? Putin huwa anaongea kiingereza hapo mkutanoni?
Anaongea nini kwani? Hivi hujui Putini ndo rasi pekee Duniani anaye angea lugha nyingi? Jamaa kwa sababu ya kufanya kazi KGB anaweza ongea Kifaransa, kingereza, kijeruman, kispanyola na kama aikosei Kiitaliano tena kwa ufasaha.
 
Akizingua atapigiwa kula ya kukosa Imani naye bungeni tuna tupa kule ukizingatia hata CCM kwenyewe atakiwi .hotuba zake zote azina busara hata kujikumbushia si kama za nyerere "kile kimtpkacho mtu mdomoni ndicho kimjaacho moyoni" maandiko yanasema
 
Sasa hivi Mkuu hiyo ndiyo priority number one kuelekea 2020, kama katiba mpya ile ya rasimu ya Warioba iliyopatikana kupitia mapendekezo ya Watanzania haitapatikana basi kile kitengo cha wizi wa kura na chaguzi cha CCM kitafanya tena vitu vyake 2020 ili kuhakikisha ile ndoto ya CCM kuitawala Tanzania milele inaendelea.

Hivi nyie bado mnaota 2020 mtamshinda Magufuli, endeleeni kuota.
 
Kama ni ukatili na visasi basi hata Mwenyezi Mungu ana ukatili na visasi kwa sababu aliwahi kuua watu ambao hawakukubaliana na alichokisema na kukitaka!
Hiyo dhana ya udikteta ni hisia tu kama zilivyo hisia zingine za kibinadamu..
Mkuu hiyo presidential affairs act nimeipitia, sikuona mahali ambapo Rais kwa utashi wake anaweza kukiuka sheria zilizoanishwa

Hoja ya Nyani Ngabu kama umemsoma vizuri ni kuwa kauli nyingi za mheshimiwa zinatoa nafasi kwa wanaomtuhumu kuwa ni 'dikteta' kujenga hoja.

Hapa NN alizungumzia kuhusu Rais kuzuia mafao halali ya Seif kwasababu hakukubali mkono wa Dr Shein katika mazishi ya Jumbe.

Maswali kwako, je, kukataa mafao halali ya kisheria ni jambo sahihi? Na kwa sheria ipi ya nchi?

Je, kufanya hivyo si kisasi kutokana na kukataa mkono kama alivyosema?

Kuna sheria ipi inayotoa ruhusa kwa Rais kukiuka haki za msingi za mtu kwa kutumia ofisi yake katika masuala yasiyo ya kiserikali? Je, hiyo siyo abuse of power?
 
Ulichoandika ni kweli tupu Mkuu, kuhusu kuhudhuria mkutano wa Umoja wa Mataifa hilo sahau kabisa atazungumza kwa lugha ipi kwenye kikao hicho cha Umuja wa Mataifa? Ni lazima tutasikia Mama Samia atamuwakilisha kama siyo Majaliwa.

Kwa kujifariji tu na hamjambo. Mtaendelea kujifariji hivi hivi mpaka 2025.
 
Hiv speech writers wa bwana mkubwa siku hiz wana kazi kweli?..mana all the time akiongea anaenda off script..
 
Mimi sisemi alichokifanya kule Zanzibar ni kizuri maana yeye ni mwanadamu tuu. lakini katika ubinadamu wake kaamua kuunyesha wazi maumivu yake kama mtu. Kinacho nishangaza hakuna aliyelaumu kitu Maalimu Seif alichofanya ila Magu kasikika yeye ndiye wa kuhukumiwa kuna kosa kubwa na dogo kwa Mungu? jamani wote ni binadamu tuu wacheni uzandiki
 
Mlitaka katiba mpya kwa J.K akawachekea halafu mwisho wa siku wakaspend more than 200 billion na hamjaipatam.. hao ndio aina ya wanasiasa ambao tunawataka... watudanganyedanganye maana tukiambiwa ukweli unauma...

Kheri ya Magufuli anayesema dry kuwa hatafanya kitu fulani ili ujue Remedy utaipata wapi
Kwani Mrema aliyemjumuisha kwenye serikali yake sio mpinzani?
 
Mambo Ya kumpa mtu mkono au kutompa hilo ni wazo lake kama Mwanasiasa yeyote,halina maana yeyote kwa kwani kila mtu na roho yake,kuhusu katiba na udikteta mi sio mtaalamu wa mambo Ya sheria lakini najua katiba haimruhusu rais kukaa madarakani zaidi Ya miaka kumi,na haijawahi kutokea toka demokrasia Ya vyama vingi kuzaliwa nchini kwa hiyo sikubaliani na suala lolote linalosema Magu ni dikteta kwani hajamaliza hata miaka miwili madarakani.
Mkuu rudia tena kusoma ulichoandika kama utajielewa.
 
You must be ill informed, Putin aliwahi kumjibu mtu kwenye mkutano wa umoja wa mataifa, " Kama unataka kutahiriwa, njoo Urusi, kuna mtaalamu atakutahiri Na atahakikisha hakuna kitakachoota tena"
Putin alikuwa DIKTETA. Sasa nimekuelewa huu ufananisho wako.
 
Nasubiri kwa hamu hicho kikao cha UN ili mumuone rais wangu akituwakilisha vema huko na kisha kuongea na waandishi wa habari kama wa CNN na BBC - Hard talk, kuhusu masuala mbali mbali ya nchi yake ikiwa ni pamoja na demokrasia
 
Mimi sisemi alichokifanya kule Zanzibar ni kizuri maana yeye ni mwanadamu tuu. lakini katika ubinadamu wake kaamua kuunyesha wazi maumivu yake kama mtu. Kinacho nishangaza hakuna aliyelaumu kitu Maalimu Seif alichofanya ila Magu kasikika yeye ndiye wa kuhukumiwa kuna kosa kubwa na dogo kwa Mungu? jamani wote ni binadamu tuu wacheni uzandiki
Sawa wote ni binadamu but tofauti yao magu ni rais na seif ni kiongoz wa cuf. Anachofanya magu kinatuhusu watanzania lazima tukiongee. Anachofanya seif kinawahusu wana cuf sio lazima tukiongee.
 
Back
Top Bottom