Rais Magufuli, katiba mpya, na Umoja wa Mataifa

Ziara ya MTUKUFU mheshimiwa rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli huko visiwani Zanzibar iliyofanyika siku chache zilizopita imeniacha na maswali kadhaa.

Baadhi ya kauli zake akiwa ziarani huKo zimenifanya nijiulize kama kweli ile katiba mpya itaweza kupatikana chini ya utawala wake.

Kama ikitokea inapatikana, ni kweli itakuwa ni katiba yenye kuwakilisha na kulinda matakwa na maslahi ya Watanzania wote au itakuwa ni katiba yenye kuendeleza na kulinda matakwa na maslahi ya CCM tu?

Mtu mwenye kutoa kauli kama hizo hapo kwenye hiyo video ni mtu anayekupa imani wewe Mtanzania kuwa anaweza kuongoza zoezi la upatikanaji wa katiba mpya kweli?

Jamaa anaonekana ni katili, mwenye visasi, na ambaye yupo tayari hata kuvunja sheria na kutumia madaraka yake vibaya ili mradi tu alipize kisasi kwa kile anachoona au kudhani ulimfanyia vibaya.

Msikilize hapo anapoongelea suala la Maalim Seif kumgandisha rais Dkt. Shein. Rais mzima anaongelea mambo ya visasi hadharani namna hiyo?

Sasa kwa mfano hapo kwa nini watu tusidhani kwamba yeye ni dikteta? Maana madikteta ndo zao hizo. Wakiona au kudhani umewafanyia jambo fulani baya basi lazima walipize kisasi.

Hapo kwa nini tusidhani kwamba hili sakata la Freeman Mbowe, Bilicanas, na shirika na nyumba la taifa nalo si la kisiasa?

Kwa nini tusidhani kufungiwa kwa vile vituo vya redio na gazeti pia ni suala la visasi vya kisiasa?

Yaani huyu jamaa anawarahisishia sana kazi ya kujenga hoja juu ya udikteta wake wale wote ambao wamekuwa wakimuita dikteta tokea aliposhika madaraka.

Hakuna tena haja ya kusema yeye ni dikteta. Matendo yake na maneno yake mwenyewe yanajieleza!

Kama ni halali ya kisheria kwa Maalim Seif kupata stahiki zake kutokana na utumishi wake, wewe eti unasema usingempa kwa sababu alikukaushia. Nachoka kabisa.

Ngoja hayo niyaache. Tuje kwenye mkutano mkuu wa Umoja wa Mataifa utaofanyika baadae mwezi huu.

Hapo napo sijui itakuwaje? Ataenda mwenyewe kwa mara ya kwanza kama rais au ndo watatumwa akina Majaliwa na Bi. Samia?

Tutajua muda si mrefu.

Manake mwenzake aliyemtangulia alikuwa hakosi. Kwanza mida kama hii tayari usikute angekuwa keshatia timu huko Marekani akijivinjari kwenye ma Animal Kingdom theme park ya Disney huko Florida😀.

Sasa tutaona huyu Ngosha naye itakuwaje.

ngosha is too local; he is going nowhere. i think majaliwa or samia will represent him.
 
Mlitaka katiba mpya kwa J.K akawachekea halafu mwisho wa siku wakaspend more than 200 billion na hamjaipatam.. hao ndio aina ya wanasiasa ambao tunawataka... watudanganyedanganye maana tukiambiwa ukweli unauma...

Kheri ya Magufuli anayesema dry kuwa hatafanya kitu fulani ili ujue Remedy utaipata wapi
 
Ulichoandika ni kweli tupu Mkuu, kuhusu kuhudhuria mkutano wa Umoja wa Mataifa hilo sahau kabisa atazungumza kwa lugha ipi kwenye kikao hicho cha Umuja wa Mataifa? Ni lazima tutasikia Mama Samia atamuwakilisha kama siyo Majaliwa.

Lugha ndio kigezo cha kuhudhuria mkutano wa umoja wa mataifa? Putin huwa anaongea kiingereza hapo mkutanoni?
 
Ziara ya MTUKUFU mheshimiwa rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli huko visiwani Zanzibar iliyofanyika siku chache zilizopita imeniacha na maswali kadhaa.

Baadhi ya kauli zake akiwa ziarani huKo zimenifanya nijiulize kama kweli ile katiba mpya itaweza kupatikana chini ya utawala wake.

Kama ikitokea inapatikana, ni kweli itakuwa ni katiba yenye kuwakilisha na kulinda matakwa na maslahi ya Watanzania wote au itakuwa ni katiba yenye kuendeleza na kulinda matakwa na maslahi ya CCM tu?

Mtu mwenye kutoa kauli kama hizo hapo kwenye hiyo video ni mtu anayekupa imani wewe Mtanzania kuwa anaweza kuongoza zoezi la upatikanaji wa katiba mpya kweli?

Jamaa anaonekana ni katili, mwenye visasi, na ambaye yupo tayari hata kuvunja sheria na kutumia madaraka yake vibaya ili mradi tu alipize kisasi kwa kile anachoona au kudhani ulimfanyia vibaya.

Msikilize hapo anapoongelea suala la Maalim Seif kumgandisha rais Dkt. Shein. Rais mzima anaongelea mambo ya visasi hadharani namna hiyo?

Sasa kwa mfano hapo kwa nini watu tusidhani kwamba yeye ni dikteta? Maana madikteta ndo zao hizo. Wakiona au kudhani umewafanyia jambo fulani baya basi lazima walipize kisasi.

Hapo kwa nini tusidhani kwamba hili sakata la Freeman Mbowe, Bilicanas, na shirika na nyumba la taifa nalo si la kisiasa?

Kwa nini tusidhani kufungiwa kwa vile vituo vya redio na gazeti pia ni suala la visasi vya kisiasa?

Yaani huyu jamaa anawarahisishia sana kazi ya kujenga hoja juu ya udikteta wake wale wote ambao wamekuwa wakimuita dikteta tokea aliposhika madaraka.

Hakuna tena haja ya kusema yeye ni dikteta. Matendo yake na maneno yake mwenyewe yanajieleza!

Kama ni halali ya kisheria kwa Maalim Seif kupata stahiki zake kutokana na utumishi wake, wewe eti unasema usingempa kwa sababu alikukaushia. Nachoka kabisa.

Ngoja hayo niyaache. Tuje kwenye mkutano mkuu wa Umoja wa Mataifa utaofanyika baadae mwezi huu.

Hapo napo sijui itakuwaje? Ataenda mwenyewe kwa mara ya kwanza kama rais au ndo watatumwa akina Majaliwa na Bi. Samia?

Tutajua muda si mrefu.

Manake mwenzake aliyemtangulia alikuwa hakosi. Kwanza mida kama hii tayari usikute angekuwa keshatia timu huko Marekani akijivinjari kwenye ma Animal Kingdom theme park ya Disney huko Florida😀.

Sasa tutaona huyu Ngosha naye itakuwaje.

nikiri kwamba tangu nizaliwe sikupata kusikia speech ya ovyo kama hii kutoka kwa rais. ina maana nagekuwa yeye angemnyima maalim seif mafao yake ya kikatiba? huyu jamaa kweli ni dikteta.
 
Sasa kwanini anakwepa kuhudhuria mikutano mbali mbali tangu aingie madarakani? hebu twambie sababu ni ipi labda mwenzetu unaijua. Huwezi kumfananisha Putin na Magufuli uzito wao katika Ulimwengu wa siasa una tofauti kubwa sana.

Lugha ndio kigezo cha kuhudhuria mkutano wa umoja wa mataifa? Putin huwa anaongea kiingereza hapo mkutanoni?
 
God, grant me the serenity
to accept the things I cannot change; the courage to change the things I can; and the wisdom to know the difference.
 
Sasa kwanini anakwepa kuhudhuria mikutano mbali mbali tangu aingie madarakani? hebu twambie sababu ni ipi labda mwenzetu unaijua. Huwezi kumfananisha Putin na Magufuli uzito wao katika Ulimwengu wa siasa una tofauti kubwa sana.

Hoja uliyoleta Ni lugha, Hilo la uzito kiuongozi duniani sidhani Kama lina maana,
Na sio Putin tu, Gaddafi alikua akihutubia kwa kiingereza?
Kama hatokwenda, basi itakua ni ile tunaita delegation of power, ama kuna mahali imeandikwa lazima head of state ahudhurie??
 
nikiri kwamba tangu nizaliwe sikupata kusikia speech ya ovyo kama hii kutoka kwa rais. ina maana nagekuwa yeye angemnyima maalim seif mafao yake ya kikatiba? huyu jamaa kweli ni dikteta.

You must be ill informed, Putin aliwahi kumjibu mtu kwenye mkutano wa umoja wa mataifa, " Kama unataka kutahiriwa, njoo Urusi, kuna mtaalamu atakutahiri Na atahakikisha hakuna kitakachoota tena"
 
Sasa unagombea urais wa nini ikiwa unaogopa kuiwakilisha nchi yako katika mikutano muhimu duniani? Ndiyo narudia tena ni lugha inagomba kama wewe unajua sababu nyingine za muhimu za yeye kutohudhuria zaidi ya vikao vitano vya kimataifa tangu aingie madarakani tuwekee hapa ili na wengine tujue kinachojiri hata ashindwe kusafiri.

Hoja uliyoleta Ni lugha, Hilo la uzito kiuongozi duniani sidhani Kama lina maana,
Na sio Putin tu, Gaddafi alikua akihutubia kwa kiingereza?
Kama hatokwenda, basi itakua ni ile tunaita delegation of power, ama kuna mahali imeandikwa lazima head of state ahudhurie??
 
Sasa unagombea urais wa nini ikiwa unaogopa kuiwakilisha nchi yako katika mikutano muhimu duniani? Ndiyo narudia tena ni lugha inagomba kama wewe unajua sababu nyingine za muhimu za yeye kutohudhuria zaidi ya vikao vitano vya kimataifa tangu aingie madarakani tuwekee hapa ili na wengine tujue kinachojiri hata ashindwe kusafiri.

Mgawanyo wa madaraka,
Unaweza kunitajia hasara tulizopata Kama taifa kwa yeye kukosa kuhudhuria hiyo mikutano uliyotaja?
Kuhus lugha, nimekuuliza Putin huwa anatumia Lugha gani? Gaddafi alikua akitumia Lugha gani? Rais wa China huwa anatumia Lugha gani?
 
Mtu anazungumzia waziwazi uvunjaji wa sheria sababu ya visasi.

Kuna usemi wa ficha upumba.vu wako, usifiche hekima yako.

Jamaa akifungua tu mdomo wake anaondoa mashaka yote kuwa yeye ni dikteta!
Miafrika ndivyo ilivyo. ......
 
Back
Top Bottom