Rais Magufuli, katiba mpya, na Umoja wa Mataifa

Rais Magufuli, katiba mpya, na Umoja wa Mataifa

Ni bora hiyo katiba isubiri tu hadi huyu aondoke, katiba itakayokuja chini ya huyu ndugu itakua ya kulipiza visasi tu, inaweza ikampa more power maana kumbuka hata bungeni wanaomkubali ni majority, whats to stop him from forcing his own views kwenye katiba? maana kila anachoongea wao wanakikubali without question. Wapinzani wakikataa ataita jeshi aseme wanafanya usafi bungeni.

Polepole ambao hawajamuelewa bado watamuelewa tu, kuna watu wamejifunga akili watakuja kufunguka when its already too late, wengine pia hawatokuja kufunguka, ndiyo uzuri wa kuongoza taifa ambalo more than 50% wana uwezo mdogo wa kufikiri, ukiwapa stunt kidogo za kufirisi masikini watakua tayari kukupigania kwa lolote lile.
 
Naona jinsi anavyojitahidi kulitungia taifa sheria zake mwenyewe without any restraints by parliament in which are full of personal interest! I think in every time he make a public appearance he tries to make clear on how he is capable of destroying the opposition! He is so out of control....president of the Worst character!
 
Binafsi natilia shaka Elimu yke na uelewa wake na uwezo wake wakufikiri nina hakika ayupo sawa
 
Sasa unagombea urais wa nini ikiwa unaogopa kuiwakilisha nchi yako katika mikutano muhimu duniani? Ndiyo narudia tena ni lugha inagomba kama wewe unajua sababu nyingine za muhimu za yeye kutohudhuria zaidi ya vikao vitano vya kimataifa tangu aingie madarakani tuwekee hapa ili na wengine tujue kinachojiri hata ashindwe kusafiri.
Tatizo sio lugha mkuu, ni kile anachoongea kutoka moyoni. Pumba
 
Ajenda ishabadilika!

Badala ya hapa kazi tu imekuwa hapa visasi tu.
Very true.....

Pia tumetengeneza taifa la watu waoga, watu wa kujipendekeza, kila siku tunatengeneza mizigo, matuzu....watu wa ndio kwa kila jambo, watu wasio HOJI wala kudadisi. Hii kitu ni mbaya sana
 
Kama ni mzuri sana kama anavyozungumza,basi ni vizuri tuu maana nchi imepata mtu atakaeielekeza kule aliko.Kama ni mbaya sana kama anavyozungumzwa,basi ni vizuri tuu maana nchi imepata mtu atakayeonyesha kule iliko.
Muda ni pazia linalofunguka taratibu.Usijifiche nyuma yake ukiwa hujavaa nguo.
 
Huyu mtu anadhalilisha taasisi nzima ya urais,ajifunze kutoka kwa marais wa nchi zilizoendelea,huyu miezi tu matamko ya kijinga 20 kidogo,Obama anamalizia utawala wake hajawahi kuongea mambo ya kipuuz namna hii
Mkuu quote zako zinamiba? maana unacjoma choma wahusika...
 
Nahisi katiba tuliyonayo kwa sasa ni nzuri tuendelee nayo mpaka hapo baadae
 
Nahisi katiba tuliyonayo kwa sasa ni nzuri tuendelee nayo mpaka hapo baadae
Wewe Jamaa nilijua hatupo nawe ila nime google ndio nimeona ni Mo Mtoi ndie aliyedanja... Pole sana maana nilikutambua u marehemu...
 
Rais wa nchi ndio baba wa nchi,anatakiwa ahubiri mshikamano na kusameheana .Taifa linakua moja na inakua rahisi kusonga mbele

Rais asome hotuba hizi za papo kwa papo zinaleta nyufa miongoni mwa wananchi
 
Hoja uliyoleta Ni lugha, Hilo la uzito kiuongozi duniani sidhani Kama lina maana,
Na sio Putin tu, Gaddafi alikua akihutubia kwa kiingereza?
Kama hatokwenda, basi itakua ni ile tunaita delegation of power, ama kuna mahali imeandikwa lazima head of state ahudhurie??

Sasa ndo umeandika nini hapa? Kwamba unamtetea Magufuli kabla hajashindwa kuhudhuria huo mkutano uliotajwa kwenye hii mada? Au unatetea kutokujua kwake Kiingereza? Hey, just be straight? Wakati mwingine kuficha ujinga wako kunakusitiri kuliko kujaribu kuutetea!
 
Mie niliwahi kuandika hapa huyu bila shaka ana hitilafu tena si ndogo ya kiakili, labda siku moja itakuja kuthibitika maana chuki anazotema nchini zinashangaza sana.

Mkuu, hawa ccm wanajua kama huyu mtu ana matatizo kichwani mwake. Nilishangaa sana walipomchagua huyu!!! haya anayoyafanya yanaashiria kwamba some thing is wrong with him. wasipochukua hatua mapema kuna hatari siku moja volcano ita-erupt na huko ndiko tunakoelekea!!
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Magu anaelewa vizuri sana siyo yeye anayetoa ruzuku wala posho,ni vijembe vya kisiasa tu.kwa kifupi anamaanisha tukikutana kwenye misiba tuweke siasa tofauti na anafahamu watu wanamuita dikteta kwa hiyo anatoa kauli za kidikteta kupata Kiki ikumbukwe siyo wana CCM wote waliopenda hawe Rais. Tukumbuke pia ni mwanasiasa and he is representing the party in power.
 
Tuje kwenye mkutano mkuu wa Umoja wa Mataifa utaofanyika baadae mwezi huu.

Hapo napo sijui itakuwaje? Ataenda mwenyewe kwa mara ya kwanza kama rais au ndo watatumwa akina Majaliwa na Bi. Samia?

Tutajua muda si mrefu.

Manake mwenzake aliyemtangulia alikuwa hakosi. Kwanza mida kama hii tayari usikute angekuwa keshatia timu huko Marekani akijivinjari kwenye ma Animal Kingdom theme park ya Disney huko Florida😀.

Sasa tutaona huyu Ngosha naye itakuwaje.
Animal Kingdom theme park stuff unamuongelea Kikwete au Magufuli? I don't see how that relates to Udikteta na Katiba Mpya.
 
Kudhani ni haki yako na kuishia kudhani huku ukitoa hitimisho ni dalili ya watu ambao hawana uwezo mkubwa kifikra au wamechoka kifikra.

Wanasayansi huwa haishii kudhani bali huwa wanautafuta ukweli.

Kama ni ukatili na visasi basi hata Mwenyezi Mungu ana ukatili na visasi kwa sababu aliwahi kuua watu ambao hawakukubaliana na alichokisema na kukitaka!

Tumezoea siasa za kinafiki kiasi kwamba anachokisema mwanasiasa siyo kile anachoimanisha au kukitenda.

Rais Magufuli anakuambia na kukitenda kile anachokisema.

Hiyo dhana ya udikteta ni hisia tu kama zilivyo hisia zingine za kibinadamu.

Jielimishe zaidi kupitia The Presidential Affairs Act Cap. 9 (RE: 2002).

Hakuna sheria inayomtaka Rais wa Tanzania kwenda UN.

Ikumbukwe kuwa, Katiba ya Tanzania 1977 katika Ibara ya 34(4) inasema;
‘’Bila ya kuathiri masharti mengineyo ya Katiba hii, madaraka ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano yatatekelezwa ama na Rais mwenyewe moja kwa moja au kwa kukasimu madaraka hayo kwa watu wengine wenye madaraka katika utumishi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano’’.

Katiba inasema Rais anaweza kukasimu madaraka kwa kiongozi yoyote ili kumuwakilisha UN.

Tatizo ni Engl**h....,sio hivo visingizio....vya kikatiba
UN hamna Swa****** wala Suku*****
Time will tell...
My fall is to close.
 
"Nyani Ngabu, post: 17487507, member: 188"]Ziara ya mheshimiwa rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli visiwani Zanzibar imeniacha na maswali kadhaa.
NN ziara si kwamba imeacha maswali mengi, imefungua macho na kutuonyesha mengi.

Akiwa Unguja, alisema' mambo hayaendi kukiwa na kutoelewana...'
Hakuna shaka aliombwa kusaidia Dr Shein ana wakati mgumu kwa Taifa lisilo na raha.

Badala ya kutengeneza hali ziara imechochea hasira kutokana na lugha iliyotumika ambayo hata wanaCCM haikuwapendeza. Ziara imeacha ufa
Baadhi ya kauli zake akiwa ziarani huKo zimenifanya nijiulize kama kweli ile katiba mpya itaweza kupatikana chini ya utawala wake.
Moja ya sababu za kupiga marufuku 'shughuli' za siasa ni kuhakikisha maswala ya katiba ima hayapo au yanaletwa katika 'kisahani' bila choice

Kama ikitokea inapatikana, ni kweli itakuwa ni katiba yenye kuwakilisha na kulinda matakwa na maslahi ya Watanzania wote au itakuwa ni katiba yenye kuendeleza na kulinda matakwa na maslahi ya CCM tu?
Kwa kutumia katiba iliyopo CCM wamerudi madarakani.

Kwa nusra iliyowapata, hawadhinishi kingine bali katiba itakayolinda masilah yao.
CCM imepoteza mvuto,kinachoiweka ni vyombo vya umma vikiwemo vya maguvu.

Katiba haipo, ukiwasikiliza akina January kauli zao zimelenga kuwafurshisha Wznz
Jana limezungumziwa suala la mafuta na gesi ambalo ni agenda ya CUF

Maana yake ni kuteka agenda zote na kutengeneza katiba kwa njia ya ujanja ujanja.
Inawezekanje kuondoa suala la kikatiba kwa kutumia vikao vya CCM?
Mtu mwenye kutoa kauli kama hizo hapo kwenye hiyo video ni mtu anayekupa imani wewe Mtanzania kuwa anaweza kuongoza zoezi la upatikanaji wa katiba mpya kweli?
Kama yupo mwenye matumaini, aachane nanyo, ataugua ugonjwa wa moyo.
Katiba ya CCM itapita, watakaokataa watakamatwa na kufunguliwa mashtaka ya uchochezi. Katiba ikipitishwa wanaachiwa huru
Jamaa anaonekana ni katili, mwenye visasi, na ambaye yupo tayari hata kuvunja sheria na kutumia madaraka yake vibaya ili mradi tu alipize kisasi kwa kile anachoona au kudhani ulimfanyia vibaya.
Hili kwakweli limeleta tafsiri mbaya sana.

Ukimsikiliza anasema,'mtu aje usaini makaratasi akatibiwe..' kwa maana kuwa hata suala la ubinadamu na ugonjwa, siasa ipo mbele kuliko maisha.

Kwamba, hawezi kusaini nyaraka kwasababu ya hitilafu za kisiasa.
Kwanza, matatizo ya Shein na Seif si lazima ya jamii.

Kuna uwezekano wana matatizo binafsi, kwanini mgogoro ufanywe suala la kitaifa

Pili, hakuna sharia inayotambua mkono wa Rais.
Pengine wapo wasiokwenda mikutano yake kwasababu zile zile za maalim Seif.

Maalim ana haki ya kukubali au kukataa mkono, mikono ya wawili h ya Taifa, ni mikono wanayotuma katika kazi za kitaifa kama mkulima anavyotumia mkono katika jembe

Tatu, haki za maalim Seif si favor, zipo kisheria. Kumkatalia haki zake kwasababu ya mikono, ni kuvunja sheria, kukiuka haki za Raia na kukiuka haki za binadamu.

Katiba inatambua haki ya Raia kuishi,anapokataliwa 'makaratasi' ni visasi

Nne, hili linazidi kuleta hofu ya kufunga viongozi midomo. Nani katika wastaafu atanyanyua mdomo tena ikiwa ameshajua makatasi yake hayasainiwa?

Tutakuwa na Taifa la watu waoga na wenye nidhamu za kinafiki.

Tano, hili linatoa picha gani kwa maafisa wa chini?
Hivi siku tukisikia RC au DC amepiga marufuku wapinzani kutibiwa Hospitali tutajiuliza ni kwanini?
Hapo kwa nini tusidhani kwamba hili sakata la Freeman Mbowe, Bilicanas, na shirika na nyumba la taifa nalo si la kisiasa?
Kwa kauli za jana, hisia zinabeba uzito kuliko ilivyokuwa juzi au kabla. Kutibiwa ni tatizo seuse biashara? Tulisema, NHC walifanya ima timing mbaya au deliberate! shaka imeondoka!
Kwa nini tusidhani kufungiwa kwa vile vituo vya redio na gazeti pia ni suala la visasi vya kisiasa?
Niliposhangaa ni Rais aliposifu vyombo vya habari kuonyesha tukio la mikono. Nikajiuliza ni serikali hii hii ndiyo imekataza shughuli za bunge kuonyeshwa.

Ni wapi vyombo vya habari vinakuwa muhimu na wapi havipaswi kuonyesha matukio?
Yaani huyu jamaa anawarahisishia sana kazi ya kujenga hoja juu ya udikteta wake wale wote ambao wamekuwa wakimuita dikteta tokea aliposhika madaraka.
Inafikia mahali hoja inajipa 'uhalali' kutokana na matukio.
Tuje kwenye mkutano mkuu wa Umoja wa Mataifa utaofanyika baadae mwezi huu.Hapo napo sijui itakuwaje? Ataenda mwenyewe kwa mara ya kwanza kama rais au ndo watatumwa akina Majaliwa na Bi. Samia?
Kuna mambo yanafikirisha sana.

Tanzania ilipewa uenyekiti wa 'Troika' wa SADC.Hili ni jukumu zito, aliyepokea ni Makamu wa Rais. Hiyo ni kuwa, Rais hajawahi kushiriki na wenzake, wanamskia na anatuma VP

Rais ni mwenyekiti wa EAC, majuzi alimtuma PM katika tukio linalohusu EAC

Wakati huo huo wenzetu wanamsikia katika mikutano n.k.

Kidiplomasia, lazima wawe na wasi wasi nasi, na kwa upande wetu tunazidi kupoteza ile nguvu ya kidiplomasia. Sasa kwenda UN hilo nalo linabaki kama mtihani.
 
ukiondoa element za uvyama

kipindi hiki tumepata rais mbovu zaidi kuliko vipindi vyote vilivyopita
 
Hakuna lugha inayozungumzwa UN ila kuna six official languages zinazotumia UN na kwenye mikutano kama UN General Assembly... Lugha hzo ni English..French..Spanish..Arabic..Chinese... Russian

Kwa hyo muhutubiaji anaweza tumia moja ya hzo lugha hapo juu au Lugha nyingine yoyote ila itabidi kwanza itafasiriwe kwenda kwa moja ya hzo lugha hapo juu then United nations interpretations service itatafsiri kwenda kwenye lugha nyingine tano zilizobakia..

Kwa hyo Mkuu lugha sio tatizo anaweza kuhutubia kwa kiswahili bila shida yoyote ile..

UOTE="MsemajiUkweli, post: 17488085, member: 91662"]Kama kigezo ni lugha, kwani UN huwa wanazungumza lugha gani?

Kuna baadhi ya watu mnashangaza kweli.[/QUOTE]
 
Back
Top Bottom