Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 98,348
- 144,919
Ziara ya MTUKUFU mheshimiwa rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli huko visiwani Zanzibar iliyofanyika siku chache zilizopita imeniacha na maswali kadhaa.
Baadhi ya kauli zake akiwa ziarani huKo zimenifanya nijiulize kama kweli ile katiba mpya itaweza kupatikana chini ya utawala wake.
Kama ikitokea inapatikana, ni kweli itakuwa ni katiba yenye kuwakilisha na kulinda matakwa na maslahi ya Watanzania wote au itakuwa ni katiba yenye kuendeleza na kulinda matakwa na maslahi ya CCM tu?
Mtu mwenye kutoa kauli kama hizo hapo kwenye hiyo video ni mtu anayekupa imani wewe Mtanzania kuwa anaweza kuongoza zoezi la upatikanaji wa katiba mpya kweli?
Jamaa anaonekana ni katili, mwenye visasi, na ambaye yupo tayari hata kuvunja sheria na kutumia madaraka yake vibaya ili mradi tu alipize kisasi kwa kile anachoona au kudhani ulimfanyia vibaya.
Msikilize hapo anapoongelea suala la Maalim Seif kumgandisha rais Dkt. Shein. Rais mzima anaongelea mambo ya visasi hadharani namna hiyo?
Sasa kwa mfano hapo kwa nini watu tusidhani kwamba yeye ni dikteta? Maana madikteta ndo zao hizo. Wakiona au kudhani umewafanyia jambo fulani baya basi lazima walipize kisasi.
Hapo kwa nini tusidhani kwamba hili sakata la Freeman Mbowe, Bilicanas, na shirika na nyumba la taifa nalo si la kisiasa?
Kwa nini tusidhani kufungiwa kwa vile vituo vya redio na gazeti pia ni suala la visasi vya kisiasa?
Yaani huyu jamaa anawarahisishia sana kazi ya kujenga hoja juu ya udikteta wake wale wote ambao wamekuwa wakimuita dikteta tokea aliposhika madaraka.
Hakuna tena haja ya kusema yeye ni dikteta. Matendo yake na maneno yake mwenyewe yanajieleza!
Kama ni halali ya kisheria kwa Maalim Seif kupata stahiki zake kutokana na utumishi wake, wewe eti unasema usingempa kwa sababu alikukaushia. Nachoka kabisa.
Ngoja hayo niyaache. Tuje kwenye mkutano mkuu wa Umoja wa Mataifa utaofanyika baadae mwezi huu.
Hapo napo sijui itakuwaje? Ataenda mwenyewe kwa mara ya kwanza kama rais au ndo watatumwa akina Majaliwa na Bi. Samia?
Tutajua muda si mrefu.
Manake mwenzake aliyemtangulia alikuwa hakosi. Kwanza mida kama hii tayari usikute angekuwa keshatia timu huko Marekani akijivinjari kwenye ma Animal Kingdom theme park ya Disney huko Florida😀.
Sasa tutaona huyu Ngosha naye itakuwaje.