Rais Magufuli aweka Jiwe la Msingi Mahandaki Reli ya Kisasa

Kawe Alumni

JF-Expert Member
Mar 20, 2019
8,372
2,000
Anatatua shida za Wananchi kijiji kwa kijiji

Pia ataweka jiwe la msingi ujenzi wa reli ya kisasa kutoka kilosa hadi makutupora

===

Rais Magufuli amekwishafika eneo la uwekaji wa jiwe la msingi ambapo amepewa maelezo ya kina juu ya Mahandaki hayo na namna ambavyo yatakavyofanya kazi.

Rais ameshiriki katika uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa Mahandaki katika reli ya kisasa pamoja na kupiga picha ya pamoja kwa ajili ya kumbukumbu ya tukio hilo.

Rais ameshafika tayari kwa ajili ya kuongea na Wananchi kuhusu tukio la uwekaji wa jiwe la msingi la Mahandaki reli ya kisasa ambapo Wimbo wa Taifa na Wimbo wa Jumuiya ya Afrika Mashariki zimeimbwa.

Viongozi wa Dini ya Kiisalamu na Kikristo wamekaribishwa ili kufungua tukio hili kwa dua ambapo kwa pamoja wamemshukuru Mungu pamoja na kumuombea mafanikio Rais Magufuli na taifa kwa ujumla.

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro amepata nafasi ya kuwatambulisha viongozi waliohudhuria katika tukio hili pamoja na kumshukuru na kumkaribisha Rais katika tukio hilo. Zaidi ya hayo Mkuu wa Mkoa ameeleza baadhi ya miradi na mafanikio yaliyotelekezwa na awamu ya tano.

Mhandisi na mtendaji Mkuu wa TANROADS Mfugale amepata nafasi ya kuzungumza na kutoa ufafanuzi wa kina kuhusu ujenzi huu wa SGR. Ameeleza kuwa Mradi huu unatarajiwa kukamilika Mwezi januari mwaka 2021.

Zaidi ya hayo, Viongozi mbalimbali Wabunge na Mawaziri wamepata nafasi ya kuzungumza ambao wote kwa pamoja wameendelea kumpongeza Rais Magufuli kutokana na maendeleo na miradi mbalimbali aliyoifanikisha katika mkoa wa Morogoro.

Rais Magufuli: leo ni siku muhimu sana. Nimeweka jiwe la msingi la ujenzi wa Mahandaki manne yenye urefu wa km 2.7 ukijumlisha barabara ya juu ya aina yake ya nusu kilomita itakayojengwa hapa, sasa barabara za juu haziko Dar es Salaam tu hata Kilosa zipo

Amesema mara yake ya kwanza kuona barabara ya kupita chini ya Mlima aliiona Uingereza alipokuwa anasoma, lakini amefarijika sasa kuna reli ya hivyo Tanzania

Amesema wapo waliomuona anaota wa kuwa aliposema nataka kujenga reli. Amewapongeza viongozi wote wa dini na wanachi kwa ujumla kwa juhdui zao za kufanikisha reli hiyo iliyogharimu Tsh Trilion 6.05

Amesisitiza kutumia fedha za ndani, kutumia cash kukamilisha ujenzi huo

Amesema anatambua matatizo yanayowakumba watu wa maeneo hayo kuwa ni migogoro ya mashamba, ambayo ni kwa kuwa mashamaba mengi yamechukuliwa na matajiri na wameshafuta mashamba zaidi ya 40,

Alichotaka kifanyike kwa wilaya ya Kilosa, wajadili jinsi ya kuyagawa bure mashamba yaliyofutwa, mashamba hayo yatagawiwaw kwa wananchi masikini. Amesema kuwa migogoro hiyo inawahusisha kwa kiasi kikubwa viongozi

Magufui aagiza ndani ya siku sabab mashamba mengine yaliyobaki wayafute na kisha kuyagawa kwa raia.

RAIS ATAJA SABABU ZA KUWAFUKUZA VIGOGO MTERA
Amesema viongozi walikuwa wanafungulia maji bwawa la Mtera ili waseme kina cha maji kimepungua, ili umeme uwe wa mgao ili waweze kuuza majenereta

Pia amezungumzia matatizo mengine ikiwemo kuuza vitu ghafi na kuagiza vitu kama tomato sauce, kwenye upande wa pamba tulikuwa tunauza pamba ikiwa ghafi ambayo walionunua walitengeneza nguo na kuvaa kisha kuturudishia mitumba.

Katika uzinduzi huo, aliyekuwa Mbunge wa Kilombero, Peter Lijualikali alikuwepo na alimsimfu Magufuli kwa kutengeneza miradi mbalimbali
 

Valuhwanoswela

JF-Expert Member
Jun 27, 2019
383
500
Rais kasoma sayansi Tanzania, hana uelewa wa Aa Baa, Cchaa Daa, ya fasihi kama huyo mleta mada.

Itakuwaje tuamini wewe unaelewa zaidi yaliyosemwa kuliko wao!
Rais wetu mpendwa amesema amesoma Uingereza ambako ndo kwa mara ya kwanza aliona mahandaki ya treni lakini hasemi alisoma kwa lughà gani maana watu wa kule Kisukuma kinawapiga chenga.

Pia hasemi ni handaki gani aliona lakini inaonyesha hakuona lile la kutoka Dover, Uingereza mpaka Calais, Ufaransa chini ya bahari meli zinapita juu treni chini umbali jaribu sawa na toka Dar hadi Zanzibar. 4

Angekuwa aliona angeimarisha Muungano kwa kuchimba handaki mpaka Zenj siyo haya chini ya vichuguu.
 

cariha

JF-Expert Member
Apr 9, 2015
9,103
2,000
Nmepiga hesabu kila mwaka napunguza 90,000/= ya deni.
Pesa yote takribani milioni inaenda kufidia hiyo asilimia 6. Kama hiyo 6% ikiondolewa watu watapata moyo wa kurejesha mikopo.
Pia mikopo italipika kirahisi na bodi ya mikopo watapata pesa ya kutosha kusomesha wanafunzi.
Aisee hyo sita ifutwe hivi wabunge waliosomeshwa na body ya mikopo huwa wanakatwa hyo asilimia kwanini huwa wanapitisha vitu bila kufikiria wengine. Imagine wafanyakazi wa serikali mishahara midogo hafu kukatwa laki mbili parefu sana aisee
 

Nguruvi3

Platinum Member
Jun 21, 2010
13,681
2,000
Huyu Sam Mahela ameajiriwa kwa kigezo gani?

Matamshi yake mabovu sana

Mpangilio wa mada hovyo sana

Uelewa wa ufafanuzi wa hoja anayosema ni kiwango duni sana

Anaongea kwa kihoro kama kada na si mwandishi wa habari

Kiwango cha chini na hovyo sana, kumsikiliza ni kinyaa sana

Pascal Mayalla
 

Wacha1

JF-Expert Member
Dec 21, 2009
14,084
2,000
Kaanza kampeni mapema huku hataki wenzake wafanye hata vikao vya ndani
Lazima ufahamu ukiwa rais una kuwa na majukumu Zaidi, hivyo kwa JPM ambaye yupo kwa ajili ya Watanzania wigo wake ni Tanzania nzima. Wabunge kwenye majimbo yao nk. Wewe vile vile unaweza kupiga kampeni kama hiyo lakini lazima uwe rais kwanza, kazi unayo. Je, utaupataje huo urais?
 

Kalamu1

JF-Expert Member
Jul 7, 2018
6,589
2,000
Rais wetu mpendwa amesema amesoma Uingereza ambako ndo kwa mara ya kwanza aliona mahandaki ya treni lakini hasemi alisoma kwa lughà gani maana watu wa kule Kisukuma kinawapiga chenga. Pia hasemi ni handaki gani aliona lakini inaonyesha hakuona lile la kutoka Dover, Uingereza mpaka Calais, Ufaransa chini ya bahari meli zinapita juu treni chini umbali jaribu sawa na toka Dar hadi Zanzibar. Angekuwa aliona angeimarisha Muungano kwa kuchimba handaki mpaka Zenj siyo haya chini ya vichuguu.
Natamani kumwita mkuu 'Kawe Alumni' asome mchango wako huu, lakini niliahidi simsumbui tena kwani kazi nyingi imemzonga.

Huyu jamaa anapenda sifa hata haoni aibu kusema uongo wakati akijua watu wanajuwa kuwa haelewi kitu juu ya hayo anayoyazungumzia.

Sijawahi kuona mtu asiyejisikia vibaya kwa kusema uongo mbele za watu kama huyu.

Ni tabia ya kipekee sana aliyonayo.

Sasa tumchochee kichwa aweke 'daraja' au 'handaki' ziwa Tanganyika ili tuvuke kiurahisi kwenda Kongo!
 

Tangawizi

JF-Expert Member
Jun 25, 2009
3,264
2,000
Mwambieni aache kuishika shika watu Mikono.
Korona IPO asitegemee waganga na wachawi
Aliyetuleta duniani, akatuacha tuwe kama tulivyo, siku akitaka atachukua. Hakuna cha kujificha ndani, wala kuacha kusalimia watu. Upuuzi gani huo? Kwani waliokufa wana madhambi mengi kuliko waliobaki hai mpaka sasa?
 

Samwel Ngulinzira

Verified Member
Aug 5, 2017
1,711
2,000
Aisee hyo sita ifutwe hivi wabunge waliosomeshwa na body ya mikopo huwa wanakatwa hyo asilimia kwanini huwa wanapitisha vitu bila kufikiria wengine. Imagine wafanyakazi wa serikali mishahara midogo hafu kukatwa laki mbili parefu sana aisee
Aliyeshiba hamkumbuki mwenye njaa! Msimu huu ndio wa kuleta mabadiliko vinginevyo hii 6% itaendelea kutuumiza.
 

bachelor sugu

JF-Expert Member
Jan 30, 2018
2,675
2,000
Yaani mahandaki mengibe yameshakamilika kwa asikimia jubwa halafu leo ndo mmeweka jiwe la msingi kuzindua ujenzi wake

Aisee kweli CCM akili zenu mnazijua wenyewe duh.
 

Sakasaka Mao

JF-Expert Member
Sep 29, 2016
5,593
2,000
matamshi yale ni jadi ya Rais na ni sahihi kupitia taaluma yake ya ualimu Discipline kwanza na hajaanza leo na hatakiwi kuacha utamaduni huo mpya uliotukuka wa kuwachana hadharani anaowatumbua ili wanaoteuliwa kujaza nafasi wajipange! hiyo inaitwa Social Sanction yaani uchafu wa mtu inaambiwa jamii nzima ili wote mumjue nanyi mjipange nayeye mtumbuliwa akome kujitapa mbele ya jamii au kutunga uongo wa kujisafisha! Magu kataja walevi kina Kitwanga, Mabosi kina Gambo nk! yuko sahihi ni Mzungu pure!!

Mimi namuunga mikono na miguu kila anaemtumbua atutangazie uchafu sisi ndio tuliompigia kura anawajibika kwetu si kwa wateule wake!

nchi yetu ilibaki maskini kwa miaka sitini kwa kukosa Rais mwenye ujasiri kama yeye na kwa kukosa uwajibikaji wa viongozi na kwa tabia mbaya ya chama chetu kuficha mambo machafu ya viongozi wake na badala ya kuwatumbua wakawa wanahamishwa vituo!!
 

Chakaza

JF-Expert Member
Mar 10, 2007
34,977
2,000
Hakika vijana kama hawa wa Chadema unaona kabisa wanafanya sanaa yao kwa mapenzi kabisa sio pesa. Ni tofauti na wale wanaoiimbia ccm kwa mamilioni ya pesa kutoka hazina ya taifa maana ccm haina pesa hizo ndio maana wapo watumishi hata mishahara ni shida kuwalipa
 

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
36,309
2,000
Huyu Sam Mahela ameajiriwa kwa kigezo gani?

Matamshi yake mabovu sana

Mpangilio wa mada hovyo sana

Uelewa wa ufafanuzi wa hoja anayosema ni kiwango duni sana

Anaongea kwa kihoro kama kada na si mwandishi wa habari

Kiwango cha chini na hovyo sana, kumsikiliza ni kinyaa sana

Pascal Mayalla
Pole sana!, ni graduate wa fani ya habari na ndio ma graduates wetu, ila pia, anavyoongea kuna watu ndio wanampenda!.
P
 

Nguruvi3

Platinum Member
Jun 21, 2010
13,681
2,000
Pole sana!, ni graduate wa fani ya habari na ndio ma graduates wetu, ila pia, anavyoongea kuna watu ndio wanampenda!.
P
Mkuu anavyoongea na kutamka maneno inashangaza sana. Fuatilia hiyo clip utaona jinsi alivyoboronga maneno ya kawaida kabisa ya kiswahili bila kuleta maana.
Pili, ukimsikiliza vizuri yeye ni kutumia maneno 'basi, naona pale'' mara nyingi . Inachosha sana

Tatu, hakutulia ni kama mtu ana kijaziba fulani, ashakum ! mwandishi na mtu mzima unakuwa na pose halafu mistari ya maneno inalingana ukitafakari unachosema ni sahihi? Huyu bwana utafikiri ni mtangazaji mwanadada wa TV ya Kim UN wa Korea. Alichobakiza ni kuruka ruka, mh mh! haifai

Mwisho, haieleweki anaongelea nini, mara madaraja halafu vituo vya afya, kisha anarudi miundo mbinu halafu maji , halafu ndege akielekea kwenye SGR. Kwa msikilizaji makini hasa tunaosikiliza watangazaji mbali mbali ninabaki nikijiuliza huyu kapate hii kazi na kwanini anapewa kipindi katika wakati kama ule.

Pascal, nikiwakumbuka akina SS Mkamba, David Wakati, Sekioni, Tido , Salama Mfamao (RIP), Halima Kihemba,Florian Kaiza, Uncle Nyaisanga (RIP) n.k. wakati wanatoa maelezo ya jambo fulani yaani utafurahi
Unapata elimu wakati unahabarika.

Sasa rudi umsikilize Sam Mahela, yaani jana ilikuwa kichefu chefu tuuu!!
Niliangalia online (Nina allergy na TBC) hata hivyo haikusaidia, nilikuwa na kichefu chefu acha tu

Alishindwa hata kueleza daraja la Ubungo linasaidiaje wananchi na Taifa.
Nilimsikia akisema litainua uchumi wa watu kuuza ndizi haraka na kurudi nyumbani!

Ile ilikuwa fursa ya yeye kueleza foleni zilikuwa na athari gani kwa Taifa kwa ujumla wake
Sam anatueleza watu wanarudi kibamba mapema, faida ya uchumi!! Tena kwa jazba hatulii kitini bwana yule

Halafu alishindwa kuelewa kuwa ni TV ya Taifa. Hata kama anapiga debe la CCM kuna matumizi ya maarifa si namna ile. Hilo tu linakimbiza wasikilizaji sasa TBC na Radio Uhuru wanashindana kwa wanachama wa Lumumba.

Najiuliza sana, hivi yule bwana alipata kazi ile kwa kigezo gani!

In short the guy is disorganized and discombobulated.
 

Babati

JF-Expert Member
Aug 7, 2014
32,506
2,000
Lazima ufahamu ukiwa rais una kuwa na majukumu Zaidi, hivyo kwa JPM ambaye yupo kwa ajili ya Watanzania wigo wake ni Tanzania nzima. Wabunge kwenye majimbo yao nk. Wewe vile vile unaweza kupiga kampeni kama hiyo lakini lazima uwe rais kwanza, kazi unayo. Je, utaupataje huo urais?
Polepole na Bashiru nao ni marais? shame on you
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom