Rais Magufuli aweka Jiwe la Msingi Mahandaki Reli ya Kisasa

Kawe Alumni

JF-Expert Member
Mar 20, 2019
8,372
2,000
Anatatua shida za Wananchi kijiji kwa kijiji

Pia ataweka jiwe la msingi ujenzi wa reli ya kisasa kutoka kilosa hadi makutupora

===

Rais Magufuli amekwishafika eneo la uwekaji wa jiwe la msingi ambapo amepewa maelezo ya kina juu ya Mahandaki hayo na namna ambavyo yatakavyofanya kazi.

Rais ameshiriki katika uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa Mahandaki katika reli ya kisasa pamoja na kupiga picha ya pamoja kwa ajili ya kumbukumbu ya tukio hilo.

Rais ameshafika tayari kwa ajili ya kuongea na Wananchi kuhusu tukio la uwekaji wa jiwe la msingi la Mahandaki reli ya kisasa ambapo Wimbo wa Taifa na Wimbo wa Jumuiya ya Afrika Mashariki zimeimbwa.

Viongozi wa Dini ya Kiisalamu na Kikristo wamekaribishwa ili kufungua tukio hili kwa dua ambapo kwa pamoja wamemshukuru Mungu pamoja na kumuombea mafanikio Rais Magufuli na taifa kwa ujumla.

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro amepata nafasi ya kuwatambulisha viongozi waliohudhuria katika tukio hili pamoja na kumshukuru na kumkaribisha Rais katika tukio hilo. Zaidi ya hayo Mkuu wa Mkoa ameeleza baadhi ya miradi na mafanikio yaliyotelekezwa na awamu ya tano.

Mhandisi na mtendaji Mkuu wa TANROADS Mfugale amepata nafasi ya kuzungumza na kutoa ufafanuzi wa kina kuhusu ujenzi huu wa SGR. Ameeleza kuwa Mradi huu unatarajiwa kukamilika Mwezi januari mwaka 2021.

Zaidi ya hayo, Viongozi mbalimbali Wabunge na Mawaziri wamepata nafasi ya kuzungumza ambao wote kwa pamoja wameendelea kumpongeza Rais Magufuli kutokana na maendeleo na miradi mbalimbali aliyoifanikisha katika mkoa wa Morogoro.

Rais Magufuli: leo ni siku muhimu sana. Nimeweka jiwe la msingi la ujenzi wa Mahandaki manne yenye urefu wa km 2.7 ukijumlisha barabara ya juu ya aina yake ya nusu kilomita itakayojengwa hapa, sasa barabara za juu haziko Dar es Salaam tu hata Kilosa zipo

Amesema mara yake ya kwanza kuona barabara ya kupita chini ya Mlima aliiona Uingereza alipokuwa anasoma, lakini amefarijika sasa kuna reli ya hivyo Tanzania

Amesema wapo waliomuona anaota wa kuwa aliposema nataka kujenga reli. Amewapongeza viongozi wote wa dini na wanachi kwa ujumla kwa juhdui zao za kufanikisha reli hiyo iliyogharimu Tsh Trilion 6.05

Amesisitiza kutumia fedha za ndani, kutumia cash kukamilisha ujenzi huo

Amesema anatambua matatizo yanayowakumba watu wa maeneo hayo kuwa ni migogoro ya mashamba, ambayo ni kwa kuwa mashamaba mengi yamechukuliwa na matajiri na wameshafuta mashamba zaidi ya 40,

Alichotaka kifanyike kwa wilaya ya Kilosa, wajadili jinsi ya kuyagawa bure mashamba yaliyofutwa, mashamba hayo yatagawiwaw kwa wananchi masikini. Amesema kuwa migogoro hiyo inawahusisha kwa kiasi kikubwa viongozi

Magufui aagiza ndani ya siku sabab mashamba mengine yaliyobaki wayafute na kisha kuyagawa kwa raia.

RAIS ATAJA SABABU ZA KUWAFUKUZA VIGOGO MTERA
Amesema viongozi walikuwa wanafungulia maji bwawa la Mtera ili waseme kina cha maji kimepungua, ili umeme uwe wa mgao ili waweze kuuza majenereta

Pia amezungumzia matatizo mengine ikiwemo kuuza vitu ghafi na kuagiza vitu kama tomato sauce, kwenye upande wa pamba tulikuwa tunauza pamba ikiwa ghafi ambayo walionunua walitengeneza nguo na kuvaa kisha kuturudishia mitumba.

Katika uzinduzi huo, aliyekuwa Mbunge wa Kilombero, Peter Lijualikali alikuwepo na alimsimfu Magufuli kwa kutengeneza miradi mbalimbali
 

Gellangi

JF-Expert Member
Apr 11, 2016
1,036
2,000
Jamaa unachekesha! Unashangaa raisi kuzindua miradi
Kinachonishangaza Mimi ni kuzindua miradi kwa kurudiarudia,mradi moja unazinduliwa,unafunguliwa na viongozi msururu kwa gharama kubwa tu.Fikiria msafara wa watawala wetu unadhani ni shilingi ngapi?Hutu baba huwa simwelewi,yeye ndiyo mbunifu,mshauri na mpangaji wa miradi na mtekelezaji wake.Mzee ametumia nguvu na raslimali nyingi katika miradi ya ujenzi huku huduma muhimu zikikosekana.
 

mr chopa

JF-Expert Member
Aug 26, 2016
4,665
2,000
Kinachonishangaza Mimi ni kuzindua miradi kwa kuruzsfeeg dxaftszsgev sdiarudia,yeye ndiyo mbunifu,mshauri napangaji wa miradi na mtekelezaji wake.Mzee ametumia nguvu na raslimali nyingi katikkdva miradi ya ujenzi
Hakuna shida au labda ulitaka mbowe ndio azindue? Na atazindua sana maanake Kuna miaka 5 mingine,
 

Gellangi

JF-Expert Member
Apr 11, 2016
1,036
2,000
Watu wengi ni wanafiki wakati miaka iliyopita tulivyokuwa tunalalamika hakuna maendeleo ya miundo mbinu ni haohao CCM ndiyo walikuwa wa kwanza kututukana. Haya mambo ya barabara yangetakiwa kufanyika miaka 20 iliyopita sio sasa.

Ni ushamba tu wa maendeleo tulionao haya ni mambo ambayo tungetakiwa kuyafanya na toene ni mambo ya kawaida. Nchi nyingine wenzetu wanafanya. Ni CCM ndiyo ilifanya watu waone kama Tanzania hatuwezi sasa haohao wanahamaki !! wakati tulikuwa tunawaambia pesa zinaliwa
Walaji wa hizo fedha tuliambiwa wamedhibitiwa,hatuambiwi kivipi.Yaani mafisadi nchi hii,waliotukwamisha miaka yote hii ni kina nani?Wamedhibitiwa kwa kupelekwa mahakama ya mafisadi?Je wamehukumiwa?
Tukiambiwa tumeibiwa sana pia tupewe taarifa ya hatua zilizochukuliwa dhidi ya wezi.
Huu utawala unaendeleza yaliyotangulia kuasisiwa na wana CCM wenzao na wanalindana.Wapi mafisadi wa ESCROW, EPA,Richmond, Meremeta,1.5-2.4Trilions,Vichwa vya Treni vilivyookotwa,Gas ya Mtwara ni wanashughulikiwa lini?
Semeni yamewashinda,mpishe wake wazalendo wafurumishwe panya wote wanaotafuna hazina ya Taifa tajiri lenye Wananchi maskini.
 

Ibambasi

JF-Expert Member
Jul 25, 2007
8,341
2,000
Ukiona mtu Mpumbavu unaumia au unamuonea huruma ??? mpumbavu anaweza kuwa amesoma lakini kuna mambo hajui na anajifanya anajuwa ..."mjinga ana afadhali , ukimuelewesha akishajua anakua mwerevu ........" JK Nyerere
Hujajibu swali dogo. Unaumia kuona Rais anazindua miradi ya maendeleo?
 

Phillemon Mikael

JF-Expert Member
Nov 5, 2006
9,672
2,000
Hujajibu swali dogo. Unaumia kuona Rais anazindua miradi ya maendeleo?

Unadhani kila mtu ni Dogo hapa ndani ....
Swali lako lilikuwa ...Unaumia ? halikuwa .....Unaumia kuona Rais anazindua miradi ya maendeleo?

Ungeuliza direct ningekujibu ..kuwa hakuna mtanzania ambaye hapendi miradi ya maendeo ifanyike ..
 

Ibambasi

JF-Expert Member
Jul 25, 2007
8,341
2,000
Unadhani kila mtu ni Dogo hapa ndani ....
Swali lako lilikuwa ...Unaumia ? halikuwa .....Unaumia kuona Rais anazindua miradi ya maendeleo?

Ungeuliza direct ningekujibu ..kuwa hakuna mtanzania ambaye hapendi miradi ya maendeo ifanyike ..
Ndiyo maana nakuita dogo kama tu huwezi kuelewa muktadha wa swali la mwanzo
 

Sijijui

JF-Expert Member
Jan 14, 2018
6,194
2,000
Kama maigizo ladba ndio mwanzo ulivyo maana tukienda Kenya au Dubai tunasifia sana maendeleo sijui wao hawakuanza mwanzo kama sisi?

Shida ni kwamba hapa kwetu tunaona kabisa kuanzia msingi wa nyumba ulivyo kwa wenzetu tukisafiri hatuoni msingi tunakuta vilishafanyika ndo tofauti
Mkuu hivi Yale mahandaki kwenye reli ya Tazara rais alikwenda kuyazindua? I think kuzingua ujenzi wa mahandaki ya reli is too low for president
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom