Rais Magufuli awakabidhi waislamu mchango wa fedha za ujenzi wa msikiti, Shekhe wa Wilaya amshukuru

Hili la Kanisa Katoliki Kujenga Msikiti Paroko wangu niandalie maelezo nakuja huko. Mmetufundisha misingi ya Kanisa na kanuni zake lakini hili hamjawahi kutueleza.

Kila Jumapili unatuhubiri ukuu wa Yesu Kristo na kutuhimiza kumfuata. Kesho nitakuwa hapo niandalie majibu.

Nakuunga mkono. Tutaenda wote kwa Paroko nikiwa na cheti changu cha ubatizo. Akishindwa kujibu maswali namtupia mezani cheti chake. Wanatuita kafiri halafu pesa ya kitimito wanapokea kujengea msikiti?!? ##_&_-4##3*:+ mfyuuu.
 
Mchango wa ujenzi wa msikiti ukachangwe kanisani?how!!!!

Sijaelewa....au mleta mada ni typing error?weka nyama kidogo!
kama hujaelewa hiyo ukisikia msikiti unajengwa na JKT je? una mawazo mgando au ndio zile siasa za kishamba utaelewa tu. Hiyo ni ishara ya upendo na mshikamano bila kujali imani ya mtu mwingine, ni kitu adimu sana kwa ulimwengu wa leo
 
teh.teh.. binafsi pia ilinistua lakini nilivyokuja kuiona nafasi ya rais kama kiongozi wa nchi nikakubali hata hivyo jamaa ni risk taker mkubwa Mkapa alishiriki kujenga msikiti kimyakimya watu wamejua baadaye sana.
Mkapa hakuwachangisha watu kanisani aliwasaidia kupitia mfuko wa Rais.
Nashangaa waisalam Leo kupokea fedha za makafiri ambao hata tukiwasalimiaga Asalam Aleikhum hawaitikii itakuwa fedha za wauza kitimoto
 
Pesa iliyochangwa tayari imeshaanza kununulia mifuko ya simenti wewe unakuja na sura za Quran!.

Ndio imeisha hiyo.
Hata ichanganywe vipi, itajitenga tu! Kwanza aloyekwambia tuna shida na huo mskiti nani, tunayo mingi tu na wala haijai!
 
Tatizo unalo wewe mwenye kujifanya una haki kuliko wengine.
Waliochangishiwa pesa kanisani wameshaanza kuitumia kwa lengo lililokusudiwa wewe humu jukwaani unalalama!.
Tatizo siyo mm mkuu swala n muongozo na kanuni za dini inakataza hyo kitu hvyo kanuni za dini zimekiukwa mkuu waliowekwa madarakani kuusimamia umma wa kiislam wamelifumbia macho hili

YATUPASA KUPAZA SAUTI KWA VILE HATUNA UWEZO WA KUFIKISHIA KILIO HIKI

HAKI NA BATILI HAVITANGAMANI
 
kama zinaukakasi nawashauri wazirudishe tu kanisani tunauhitaji wa fedha mno. vinginevyo wazitunze ikifika Magu kamaliza kipindi chake wazirejeshe haraka.
 
Tatizo siyo mm mkuu swala n muongozo na kanuni za dini inakataza hyo kitu hvyo kanuni za dini zimekiukwa mkuu waliowekwa madarakani kuusimamia umma wa kiislam wamelifumbia macho hili

YATUPASA KUPAZA SAUTI KWA VILE HATUNA UWEZO WA KUFIKISHIA KILIO HIKI

HAKI NA BATILI HAVITANGAMANI
Wewe unazijua kanuni za dini kuliko mashekhe na ma-alhaj waliopokea hiyo michango!!.

Pole sana.
 
Nn Alhaj we?uislamu hauangalii cheo cha mtu,ikiwa Mtume mwenyew kuna mambo aliwekwa sawa na Mungu itakuwa hao unaowataja?hii ndio sababu ya tofauti kubwa kati ya uislamu na dini nyinginezo
Wewe Unaijua misingi ya uislam kuliko Alhaj anayefanya kazi na Rais wa nchi?.

Unaijua misingi kuliko Sheikh Mkuu?.
 
Achana nae huyu,kwanza huwez zungumzia kitu kama huna taaluma nacho,anadhan hii dini inaendeshwa kwa hewalla
Kuwa sheikh mkuu hakumpelekei kutofanya makosa au kukengeuka sometimes, hata mtume mwenyewe kuna kipindi alitaka kukengeuka na ndipo ikateremshwa Sura An Nabai, kipindi alipomjia kipofu. Acha pumba!
 
Hao anaodai ni viongoz wa dini ni nan alieanzisha chombo wanachosimamia?tuanzie hapo kwanza
Tatizo siyo mm mkuu swala n muongozo na kanuni za dini inakataza hyo kitu hvyo kanuni za dini zimekiukwa mkuu waliowekwa madarakani kuusimamia umma wa kiislam wamelifumbia macho hili

YATUPASA KUPAZA SAUTI KWA VILE HATUNA UWEZO WA KUFIKISHIA KILIO HIKI

HAKI NA BATILI HAVITANGAMANI
 
Yan kama mm ndo hao mashehe izo pesa za kitimoto naweka tumbo kwa maana hazina dhambi
 
Kwani kuna dhambi gani kuchangia ujenzi wa msikiti?

Mbona tunakula kitimoto na maulamaa mitaani na hawajakatazwa kuingia ibada zao?
Mbona rostam aziz alichangia Hela za kujenga kanisa
Mm sioni shida kbsa hapo, Sema watu wanataka kuleta malumbano tu

Ova

Sent from my SM-N920T using JamiiForums mobile app
 
Hili la Kanisa Katoliki Kujenga Msikiti Paroko wangu niandalie maelezo nakuja huko. Mmetufundisha misingi ya Kanisa na kanuni zake lakini hili hamjawahi kutueleza.

Kila Jumapili unatuhubiri ukuu wa Yesu Kristo na kutuhimiza kumfuata. Kesho nitakuwa hapo niandalie majibu.
Wewe siyo mkatoliki, unababaisha watu humu, mimi ni mkatoliki najua uhusiano wa kanisa na dini ya kiislamu, kwa taarifa yako, mapadre wote wa kikatoliki duniani, hakuna ambaye hajasoma Kuruhani tukufu. Hiyo huwa ni moja ya masomo ambayo padre lazima asome kabla ya kufikia daraja la upadre na ni lazima kufaulu. Hii ni dhahiri kwamba uhusiano wa dini hizi una lengo moja la kumkomboa mwanadamu. Hongera rais Magufuli kwa uamuzi wa uliotukuka.

PapaJohn Paul wa pili mwaka 2003 alipotembelea Palestine aliingia msikitini na akashiriki swala, fuatilia hilo na achana na uchonganishi
 
Wewe sio mkazi wa Dodoma na sidhani kama uwepo wako una punguza au kuongeza chochote.
كلب واحد
Uislam hauko hivyo unavyotaka wewe, kama leo wakristo wanachanga kwa ajili ya kujenga mskiti unaona sawa, iko siku wataomba na sehemu ya mskiti wafanye biashara bado utaona sawa tu! Watu hatutakiwi kubaguana ila kiimani kuna baadhi ya vitu haviko sawa, hivyo hatuwezi kuwa sawa. Amini unavyoamini ila kwangu mimi sio sawa. Hata mafundisho tumetofautiana. Hela aliyochanga mkristo kwenda kujenga mskiti sio sawa hata kidogo.
 
Back
Top Bottom