Dkt. Samizi amshukuru Rais Samia kutafuta fedha za ujenzi wa barabara ya Kibondo-Mabamba

BWANKU M BWANKU

JF-Expert Member
Jan 12, 2019
328
414
Mbunge wa Jimbo la Muhambwe mkoani Kigoma Mhe. Dkt. Florence George Samizi amesema Rais Samia ameweka historia nyingine jimboni kwake kwa kufanikisha kutafuta fedha Bilioni 63 kuanza ujenzi wa barabara kubwa ya kiuchumi kutoka Kibondo- Mabamba inayokwenda kuunganisha mkoa wa Kigoma Kagera na Geita pamoja na Nchi jirani ya Burundi.

Dkt. Samizi ameyasema hayo leo mjini Kibondo mkoani Kigoma kwenye hafla ya utiaji saini wa mkataba wa ujenzi wa barabara hiyo ya Kibondo-Mabamba yenye Km 47.9 kwa kiwango cha lami, barabara iliyokuwa kero kwa muda mrefu, lakini sasa Serikali ya Rais Samia imetafuta fedha na sasa barabara hiyo inakwenda kujengwa.

Wananchi wa Muhambwe wampongeza sana Rais Samia na Serikali yake kwa ushindi mkubwa wa kutafuta fedha na kuanza mchakato wa kuijenga barabara hiyo ya kiuchumi inayokwenda kufungua shughuli za kiuchumi za Wana Kibondo, Kigoma na mikoa jirani ya Kagera na Geita pamoja na Nchi jirani ya Burundi.

Hafla hiyo ya utiaji saini iliongozwa na Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhe. Prof. Makame Mbarawa, mkuu wa mkoa wa Kigoma Mhe. Thobias Andengenye pamoja na viongozi wengine mbalimbali wa mkoa na wilaya.

#Hakunakinachosimama
#KaziInaendelea.
 

Attachments

  • IMG-20230108-WA0014.jpg
    IMG-20230108-WA0014.jpg
    28.4 KB · Views: 7
  • 255683300056_status_4089cb4e2e104a0e97b91812279ec3f4.jpg
    255683300056_status_4089cb4e2e104a0e97b91812279ec3f4.jpg
    68.8 KB · Views: 8
  • IMG-20230108-WA0015.jpg
    IMG-20230108-WA0015.jpg
    37.8 KB · Views: 7
  • IMG-20230108-WA0017.jpg
    IMG-20230108-WA0017.jpg
    79 KB · Views: 8
  • IMG-20230108-WA0013.jpg
    IMG-20230108-WA0013.jpg
    124.5 KB · Views: 9
Back
Top Bottom