Rais Magufuli atangaza kiama kwa mitandao ya simu

Kwa vitisho hivi, hata hizo hisa zinazouzwa zitakuwa na tija yeyote? Au wananchi wajiandae kulizwa?
 
Lake Zone na itikadi za kijamaa.

Lakini mbona zilishafeli ktk awamu ya kwanza. Acheni watu wafanye biashara na wote tutafaidika kwa namna moja au nyingine.
 
Hata wao wanajua kiama kimefika, lakini kabla yakuondoka watahakikisha wanaizorotesha sana. Kipindi cha TISS kufanya kazi ya kudhibiti uhujumu uchumi kimewadia. Kazi kwao.
Saa hao TISS hawa muda wa kufatilia waujumu uchumi kazi yao kuteka watu
 
Tajiri hakomolewi jamani. Hivi hakuna wa kumwambia hili huyu mtu?? Tajiri mara zote anahamisha gharama kwa mtumiaji wa mwisho ambaye ni mwananchi
 
Mitandao ya simu imefanya pesa nyingi kuzunguka katika simu na kuzorotesha taasisi za benki

tassisi za kibenk lazima zizorote kwasababu serikali inazichukulia benki za biashara kama adui, pesa zote zimefichwa kwenye kabati la BOT badala la mabenk ya kibiashara.

mitandao ya simu kwa siku mtu hawezi kufanya miamala zaidi ya million 3 as per BOT regulations.
 
Hicho ni kiama kwa watumiaji wa simu. Wakipandishiwa kodi na wao wanapandisha gharama za huduma na mwisho anayeumia ni mtumiaji wa mwisho sio kampuni ya simu.
 
Binafsi sifahamu sana masuala ya Hisa, lakini kupitia mijadala mbali mbali humu JF kuna mdau niliona alichangia kwa kutoa taadhari juu ya biashara ya hisa katika awamu hii ya tano, alisema katika awamu hii mkataba unaweza kuvunjwa jukwaani Raisi akitoa hotuba hivyo soko la hisa kwa baadhi ya makampuni ni 'Kizungumkuti'. Nimeanza kuelewa hii point
 
Modern government approach encourages private sector
Sishangai cz bado tupo kwenye classical approach kwamba serikali ndio kila kitu inasahau yenyewe inaitegemea sekta binafsi kwenye ustawi wa nchi kutokana na kodi na sekta binafsi inaitegemea serikali kwenye sera madhubuti
 
Kimsingi Rais ametangaza kiama kwa watumiaji wa hizo huduma na siyo kwa makampuni.

Siku zote zigo huwa analibeba mlaji wa mwisho ambaye ndio Mtanzania huyu maskini na mnyonge.

Matola taratibu ndugu yangu. Hivi unaweza kueleza ni kwanini Vodacom hawapo kwenye list wa walipa kodi wakubwa nchini? Lakini jaribu kutumia ujanja wako wa mjini ili kubaini kiasi wanacholipa hao mabwana simu TRA kila mwezi. Utalia. Nchi hii inaliwa mchana kweupe.
 
Kimsingi Rais ametangaza kiama kwa watumiaji wa hizo huduma na siyo kwa makampuni.

Siku zote zigo huwa analibeba mlaji wa mwisho ambaye ndio Mtanzania huyu maskini na mnyonge.
Watanzania huwa hata hatujui tunashangilia nini. Huu mwaka wetu!
 
Back
Top Bottom