Rais Magufuli atahudhuria UN General Assembly Jumatatu?

Rais Magufuli atahudhuria UN General Assembly Jumatatu?

Hebu tupende kudumisha lugha yetu bhana.....kwan kuitukuza lugha ya kigen huo ni ukoloni mambo leo tuamke kifikra wana Afrika mashariki, tena ningefurahi sana kama Raisi JPM awepo na azungumze kiswahili kwenye mkutano huo
Au wengine mnakubaliana na usemi wa Trump kwamba tutawaliwe upya maana mnaitukuza sana hii lugha ya kigeni kwa kutokujua huo ni ukoloni
Wewebona ushatawaliwa tangu muda na bado unatawaliwa? Maana kila kitu cha nchi yako wamewekeza wazungu,sasa huo nao si ni utumwa? Misaada wanakupa wazungu,hadi bajeti kuna kiasi unawategemea.kwanza kiswahili sahau kuja kuwa lugha ya kimataifa
 
Kuna marais wa nchi nyingi tu ambao huwa hawahudhurii hiyo mikutano mfano Rais wa Botswana. Kuna faida gani kwenda hadi NY kuhutubia nusu saa wakati hamna mtu anayejali nini unazungumza wala kuchukua hatua yeyote
 
Jamani mm napita tu ila mnatoa maneno yenye ukweli lakini angalieni .
 
Alikuwa ni mtu poa sana,hata ngeri alikuwa anapasua sana

Suala sio ngeli mkuu,
Marais Kama Putin wa Urusi huwa wanahutubia mikutano ya umoja wa mataifa kwa Lugha za nchi zao Na tafsiri inafanyika kwa wasioelewa.
Kwa nini sisi watanzania hatujithamini?
Inakera sana kuona watu wanashika bango humu kuwa rais hajui kiingereza, fikra za kitumwa kabisa!
Kiingereza ndio kitatuondolea umaskini?
 
UN UNARUHUSIWA KUTUMIA LUGHA YOYOTE..HATA KAMA MAGU ATATUMIA KISWAHILI TRANSLATOR MACHINE ZIPO...
SO HAKUNA WASI...
MBONA WARUSI WACHINA ETC WANAONGEA LUGHA ZAO..

OVA
kile kiswahi kitatafsirika kweli?
mfano fanizia badala ya fanyizia
 
Naomba Mungu asiende asije kutuletea aibu ya kuhutubia Kisukuma huko maana ndo zake!

Acha fikra za kitumwa! Hata akihutubia kisandawe sawa tu! Rais wa China huwa anahutubia kwa kiingereza?
 
Akienda ntaomba ban ya muda
Utapata kwani mimi nahisi kaka katumia muda huu wa majonzi ya Kagera kufanya rehearsal ya hotuba yake kwenye UN. Watu wanahoji kama ni lazima, mimi nadhani ni wajibu wa wakuu wa nchi kuhudhuria kwani ndicho kikao kikuu cha UN ambacho kila mkuu wa nchi anatoa lake la moyoni na kuelelzea kinachomkera. Kumbuka Mugabe ambavyo kila mwaka hakosi na kila mwaka ndo anapata mwanya wa kuwabeza watawala wa UK na US mpaka mara nyingi nchi nyingi huwa zinatoka. Kumbuka wakati wa Rais wa Venezuela alivyokuwa akitoa vigongo naye. Mwalimu alitumia kikao hiki hiki kwenye Senventees kumtetea China aingie kwenye UN na alikubaliwa at last.
Tunaomba kaka Pombe aende atoe ya moyoni, aelezee mikakati ya TZ kumaliza ufisadi na aongelee mifarakano ya Maziwa makuu inavyotuzalishia wakimbizi ili hali wakimbizi wanaoangaliwa ni wale wa Syria na kwingine wakati vita ya kongo na sintofahamu ya Burundi imefumbiwa macho. Awaelezee jinsi alivyoleta elimu ya bure na aseme alivyoanza na madawati na siyo madaftari, kalamu na vitabu vya kiada kwa kila mtoto. Naamini yupo busy na mazoezi na atapanda ndege yetu wenyewe kwenda na kutua JFK. Amina.
 
Acha fikra za kitumwa! Hata akihutubia kisandawe sawa tu! Rais wa China huwa anahutubia kwa kiingereza?
Kiswahili siyo lugha inayotambuliwa kwenye UN hivyo haina wakalimani. Kiingereza, kifaransa, kispanishi, kiarabu, kichina (mandarini) na kirusi basi. Rais ana uwezo wa kuhutubia sababu hotuba yake itaandaliwa na watu wanaoweza kuandika kimombo safi tu.
 
Kuuliza sio ujinga,
Imeandikwa wapi kuwa kiswahili hakitambuliki huko UN General assembly?
Kwa hiyo Tanzania kinakotokea kiswahili sio nchi huru?
 
Kuuliza sio ujinga,
Imeandikwa wapi kuwa kiswahili hakitambuliki huko UN General assembly?
Kwa hiyo Tanzania kinakotokea kiswahili sio nchi huru?
Siyo kuandikwa tu ila inajulikana katika umoja wa mataifa lugha zinazoongeleka na ambazo zina wakalimani. Lugha ya kiswahili ina wazungumzaji wengi lakini karibu wote wanatokea eneo moja ambalo kabla ya hapo lilikuwa na lugha zilizotambulika kama rasimi. Rwanda, Burundi, Congo zote mbili walitumia kifaransa. Kenya, Uganda, Tanganyika, Zanzibar, tulitumia kiingereza kama lugha rasmi na mpaka sasa tunaitumia hivyo hatujajitoshereza kuweza kupigania haki yetu ili kiswahili kiwe lugha ya kutumika UN. Ukiangalia wenzetu Kenya hata kwenye bunge wengi wanatumia kiingereza bado je watawezaje kukitetea kiswahili? Uganda ndo kabisa waganda hawataki hata kukisikia wanadai ni lugha ya watumwa. Ingia kwenye page ya UN unaweza kujua mengi.
 
Hapo kwenye kiingereza kutambulika Kama Lugha rasmi hapa Tanzania sidhani Kama Ni sahihi,
Viongozi wetu tu wa juu serikalini hawaongei kiingereza fasaha, itakua raia wa kawaida mtaani?
Nadhani urasmi wa kiingereza Afrika mashariki Ni kwa nchi za Kenya Na Uganda ambao kwao hata muuza mchicha anaonge kiingereza kizuri tu!
Narudi kwa suala la UN,
Kama wakalimani wa Lugha ngumu Kama Kiarabu Na Kichina walipatikana, basi wa kiswahili hawajashindikana kupatikana ila Ni dharau za wazungu kwetu sisi waafrika,
Kilichobaki Ni kuwaonyesha kuwa tuna Lugha yetu Na tunaipenda Na kuithamini,
Kama rais akienda, ahutubu kwa kiswahili, wakiona umuhimu wa kutafuta tafsiri watafute, wasipoona waache!
 
Back
Top Bottom