geraldkowero1
JF-Expert Member
- Jul 5, 2014
- 1,838
- 647
Kauli Ya Jpm Mzuri Sana Anasema Asiyetaka Aache Hata Leo Mwisho Milioni 15 Tu
Sifa za kuchangia Jf ni uanachama tu.Mdomo yeyote hupewa bure na haulupiwi voucher unaweza ropoka chochote mradi huvunji sheria za nchi na kujihatarishia usalama wako mbele ya raia kwa kuropoka kwako.Mleta post hakueleza idadi ya ofisi alizotembelea na kuyasikia hayo na kwamba wanautamani uongozi wa raisi Kikwete.Hatujui uwezo wake katika utafiti na hadi yeye kuridhika na kushusha uzi kwenye jukwaa kubwa kama hili alilinganisha ofisi ngapi na adadi kubwa ya ofisi za srikali na mashirika zilizopo nchini achilia mbali za halimashauri/majiji.
Sasa nimwambie baada ya uongozi wa baba wa taifa hili mwl.Nyerere ndio nchi imempata raisi wa aina ya mwl.Nyerere.Aliokutana nao wakimlalamikia raisi Magufuli ni wale waliozoea kutenda kwa mazoea na kutochukuliwa hatua haswa waliopo nafasi za manunuzi.Nchi ilioza kwa ufisadi ulioliangamiza taifa.Haikuwepo wizara,idara,wala ofisi inayotenda haki kwa wananchi wote walichotanguliza ni rushwa na hata kiongozi wa nchi hakuonekana kuyashughulikia.Magufuli amekuwa kiongozi kwa miaka ishirini anayajua maovu na watendaji wake hivyo hajifunzi ila sasa anatenda.Magufuli ana uthubutu na asiyeogopa anachohitaji sana sana ni maombi ya watanzania kwa Mungu katika kuitekeleza hii kazi hatari.
Katika kampeni zake za kugombea uraisi na katika mikutano yake hakujaribu kuwabeza wagombea wa vyama vingine.Hayo yalifanywa na wapambe.Nae kwa kuelewa kutokubalika kwa chama chake kwa wananchi kwa asilimia kubwa aliepuka kujinadi na chama hicho na mlimsikia akiomba mchagueni John Pombe Magufuli na nawahakikishia mie nitawaongoza kadri ya maagizo yenu kwangu.Nchi yangu Tanzania.Mimi sio mwoga na sitamwogopa yeyote katika kuwafanyia wananchi kilicho haki kwa manufaa ya wananchi wa taifa langu hata kama itanilazimu kufa.Nitaunda mahakama ya mafisadi na mafisadi wote na bahati nzuri nawafahamu nitawapeleka wote huko.Hili ndilo lililowabadilisha hata wafuasi wengi wa upinzani na kumuunga mkono.Hakika angeendeleza tambo za chama chake za ccm mbele kwa mbele,wameipenda wenyewe,wapinzani waleteni uwanjani tuwachane chane tuwatupe kule,wataisoma namba n.k. hakika asingeshinda.Mtakao kumbuka siku chache kabla ya uchaguzi mkuu tulikuwa tunaomba kumpata kiongozi mkali,mchukua hatua kwa wakati,na wengine walifikia hatua ya kushauri hata akiongoza kidikteta mradi alinde uchumi,raslimali za taifa kuondoa mafisadi na kuwashughulikia na adumishe amani ya nchi wasingejali.Hamadi sasa mmempata wa chaguo mlilotaka na anatenda yale yale yaliyokuwa matamanio yenu na hata wapinzani wanamkubali utendaji wake mnaojiliza liza mnatakaje?Niwahakikishie tu ndani ya miaka miwili/mitatu ya uongozi wake kila kiru kitakuwa sawa.Hiyo milinganisho yenu ya viongozi waliopita naikataa na nawapa mfano mmoja hai.Ripoti za CAG alizokuwa akitoa kila mwaka zilikuwa zikiwekwa makabatini bila utekelezaji.Magufuli anachukua hatua kadri ya mapendekezo ya CAG.TUENDELEE KUMWOMBEA ULINZI WA MUNGU RAISI WETU NA TUMPE MOYO.