Kwanini Rais Magufuli mitano tena?

Elius W Ndabila

JF-Expert Member
Jul 17, 2019
322
645
Na Elius Ndabila

0768239284

Unaweza kumzungumza Rais Magufuli kwa lugha yoyote. Leo ninaomba nikupatie mambo tisa kama si kumi ambayo yanamuongezea Rais Magufuli wafuasi. Sifa hizi ndizo ambazo zitamuongezea kura Rais Magufuli ukilinganisha na mwaka 2015. Ambatana nami!

ELIMU, Kwa miaka yake minne na miezi kadhaa tumeshuhudia mapinduzi makubwa katika sekta ya elimu. Watanzania, hasa Watanzania wa kawaida ambao ndio walikuwa wahanga kwa kusomesha watoto wao kwenye shule za serikali walikuwa wa kikubwa na adha nyingi.

Ugumu huu ulitokana na ada na mrundikano wa michango mingine ambayo iliwafanya baadhi ya wanafunzi kuto kuendelea na masomo yao. Baada ya Mh Rais kuingia madarakani mwaka 2015 alifuta michango na ada kwa shule zote za serikali kuanzia shule ya msingi hadi kidato cha nne. Baada kufuta ada na michango hiyo serikali imekuwa inatumia zaidi ya bilioni 23 kila mwezi ili kuhakikisha Watanzania hawa wanapata haki yao ya kupata Elimu.

Kuondolewa kwa michango mashuleni kumefanya kuongezeka kwa wanafunzi maradufu wale ambao walikuwa hawaendi shuleni kwa kukosa ada na michango. Ifahamike kuwa watotowengi hawakuweza kwenda shule kwa kukosa karo au michango ambayo ilielezwa ni kwa ajili ya kuboresha elimu.

Upande wa Elimu ya juu Mh Magufuli ameongeza bajeti ya fedha ya mkopo kwa wanafunzi wanaostahili mikopo na kuongeza idadi kubwa ya wanafunzi wenye sifa kupata fedha hizo. Fedha hizi zinafika kwa wakati vyuoni na kuondoa migomo yote vyuoni ambayo tulishuhudia katika vipindi vilivyopita.

Tukiwa bado kwenye sekta ya elimu tumeshuhudia shule zinaendelea kuboreshwa na kuongeza vyumba vya madarasa baada ya wanafunzi kuongezeka. Mh Magufuli kwa kipindi chake amekarabati shule za zamani na vyuo mbali mbali ambavyo vilionyesha kuchoka kama vile Msasani Tukuyu na maeneo mengine Tanzania kote.

Kwa wadau wa Elimu hizi ni sababu chache kati ya nyingi ambazo wamejiandaa kumpatia Rais Magufuli miaka mitano mingine li aweze kuendeleza kasi ya mabadiliko katika sekta hii mhimu ya kuondoa ujinga na kuwajaza watu elimu na maarifa. Kazi iliyobaki ni kuendelea kuongeza madarasa na viti kwa ajili ya wimbi kubwa la waafunzi wanaosajiliwa kila mwaka kuanza masomo.

AFYA, Yapo mambo mengi ambayo tunaweza kuzungumza kwenye sekta ya afya na tukakesha ambayo Rais Magufuli ameweza kuyatekeleza. Kwanza ifahamike kwamba kipindi cha Rais Magufuli ameongeza bajeti ya dawa kutoka zaidi ya 30 bilion hadi kufikia zaidi ya 270 bilion hili ni ongezeko kubwa mno.

Hili limesaidia kuwa na dawa za kutosha kwenye maeneo yetu ya kupatia tiba. Haitoshi pamoja na kuboresha hospitali za rufaa, mikoa na kanda kuwa bora zaidi, Rais Magufuli amehakikisha anajajenga na kuboresha hospital za Wilaya. Rais Magufuli amehakikisha anajajenga na kuboresha vituo vyote vya afya ambapo adhima yake ni kuhakikisha kila kata inakuwa na kituo cha afya na kila kijiji kuwa na zahanati ili kuzipunguzia hospital kubwa mzigo. Leo hii vijiji vingi vina Zahanati na ambavyo havina basi vipo kwenye hatua mbalimbali za uenzi.

Maisha ya mwanadamu ili aweze kuishi ni lazima afya kuboreshwa. Kama kunamapinduzi makubwa kiasi hiki kwenye sekita ya afya unakuwa na hoja gani ya kumshawishi mtanzania asimchague Rais Magufuli?

MIUNDOMBINU
, Unapozungumzia miundombinu basi tunazungumzia barabara, reli, viwanja vya ndege na bandari. Baada ya serikali ya awamu ya nne kujitahidi kuunganisha mikoa mingi kwa barabara za lami/Bitumen, Rais Magufuli sasa anafanya kazi ya kuziunganisha Wilaya kwa barabara za lami na kuboresha ambazo zilikuwa zimechoka.

Ukipita kila mahaliutashudia moshi wa vumbi ambayo ni matokeo ya miamba inayochorongwa ili kutengeneza barabara. Nani leo Wilaya yake hakuna matrekta yanayofukua miamba na kujenga barabara? Karibia wilaya zote kuna makandarasi wanaendelea na kutengeneza barabara.

Viwanja vya ndege vya Katavi, Iringa, Kigoma, Geita, Dodoma Rais Magufuli kavirudisha. Nenda Mtwara, Ruvuma, Kagera nk mambo yanaenda. Huku viwanja vya Mbeya, terminal 3 DSM, Mwanza n.k vikiwa kwenye mwonekano mpya. Adhima ya JPM ni kila mkoa kuwa na kiwanja kizuri ili wote wanufaike na ndege zao.

Haitoshi bandari mambo yanafanyika, njia ya reli ya kwenda Kilimanjaro imefufuliwa huku kasi ya SGR haina mfano wake. Moja ya faida kubwa tutakazopata kutokana na reli, kwanza ni kupunguza ajali kwa kuwa gari zitapungua barabarani kwa kuwa mizigo mingi itasafirishwa kwa treni. Pili barabara hazitaharibika hovyo hovyo kwa kuwa gari kubwa zitapungua barabarani. Hivi unamudanganyaje Mtanzania asimchagua Rais Magufuli? Hata usipomchagua basi ndege na Wanyama watamuchagua.

USAFIRISHAJI, Kwenye sekta ya usafirishaji Rais Magufuli amefufua shirika la ATCL ambalo lilikuwa limekufa. Leo hii mikoa ya Tanzania ndege zinapishana angani zinazoenda mikoani kama ilivyo kwa magari. Ndege zinafaida nyingi na moja wapo ni kuharakisha safari. Kama ulikuwa na uwezo wa kusafiri kwa gari hadi mbeya kwa masaa 14 na leo unaenda kwa saa 1:30 kwa nini usimpigie Rais Magufuli kura?

NIDHAMU KAZINI, Zamani ulikuwa ukienda kupata huduma maofisini wanakuangalia kwanza. Yaani wanaku value. Wakiona mwepesi mwepesi watakwambia njoo siku furani kama kidogo wa kibabe watakwambia subiri kwenye benchi na usiombe awe amevaa miwani. Wakati mwingine uliishiwa kutukanwa matusi, na kama ndo ulikuwa mgonjwa basi ugonjwa unaongezeka. Ili uhudumiwe ilikuwa lazima utoe rushwa na aina yeyote ya Rushwa ilihusika.

Rais Magufuli alishawazika wote na mashetani yao. Kwa sasa ukienda ofisini unaulizwa tukusaidie nini? Kila mtu anatimiza wajibu wake, wamebaki wachache ambao mioyo ilishakata tama ya maisha. Ukikuta na watu ambao walishaonja machungu ya kutohudumiwa maofisini na leo wakienda wanahudumiwa unahitaji sijui akili ya kiwango gani kuwashawishi kwa Rais Magufuli hafai? Watakuona wewe ni Beberu

VITA YA RUSHWA, Rushwa imepunguzwa kwa kiasi kikubwa. Hata kama ipo si ya wazi kama ile ya zamani ya unaniachaje? Leo watu wanaona aibu kusema, labda wakiwa gizani. Waliobainika wengi wapo ndani na Rais Magufuli hakuangalia sura ya mtu. Na kwa kusistiza hilo aliamua kuanzisha mahaka ya mafisadi. HUYU NDIYE MZEE MAKAMBA ALISEMA ATAWABATIZA KWA MOTO.

VITA YA MADAWA YA KULEVYA, Rais Magufuli alianza kwa kudhibiti kwenye viwanja vyote vya ndege na kwenye malango yote ya mipakani. Alitambua kuwa kutokudhibiti wimbi hili la matumizi na usambazaji wa madawa ya kulevya anaweza kuwa na taifa la mateja. Akaamua kuingia kwenye vita ngumu ambayo ilikuwa inafanywa na watu wakubwa. Pamoja na kwamba halijaweza kudhibitiwa kwa asilimia mia moja, lakini kuna unafuu mkubwa.

Hata zile Pombe ambazo zilikuwa zikitengenezwa Malawi zikiletwa huku na wakati kwao hawazitumii zilipigwa marufuku. KWANI HUKO KWENU KUNA ZILE POWER TENA? Hivi unawaambia nini wazazi ambao watoto wao waliuwa waathirika wakubwa wa hizi dawa na wasimchague Rais Magufuli? Jaribu kupata muda utafakari.

WATUMISHI HEWA, Ninatambua moja ya maadui wakubwa wa Rais Magufuli ni Watumishi hewa. Rais Magufuli alipoingia madarakani alianza kuwaondoa watumishi hewa na watumishi waliodanganya kwa kutumia sifa ambazo si zao kupata utumishi. SERIKALI ilitumia fedha nyingi kulipa watu ambao walikuwa hewa. Wapo waliokuwa walishakufa na wapo waliokuwa wakitumia vyeti ambavyo si vyao. Adhima ya Rais Magufuli ilikuwa ni kuhakikisha kila mtu anapata alichostahili na kudanganya.

MAKUSANYO YA SERIKALI, Rais Magufuli kwa mjibu wa mamlaka ya TRA takwimu zinaonyesha kuwa serikali sasa inakusanya zaidi ya 1.8 trillion kwa mwezi ukilinganisha na kipindi cha nyuma ambapo makusanyo yalikuwa ni bilioni 800 kwa mwezi. Ongezeko hili ni kutokana na serikali ya Rais Magufuli kubana mianya yote ya utoroshaji wa fedha na ukwepaji kodi. Kwa sasa kila mtu analipa kodi inayostahili.

Rais Magufuli aliamua kuwa mkali kwenye kodi kwa kuwa aliamini serikali yoyote makini lazima ikusanye kodi ili iweze kujiendesha. Watu wamekuwa na maswalikuwa kwa nini kama aliondoa watumishi hewa na kuongeza makusanyo mbona mishahara haiongezeki kwa kiwango kikubwa?

MAJIBU YA KAWAIDA NI KUWA MIRADI MINGI INAYOJENGWA INATEGEMEA FEDHA ZA NDANI, HAENDI KUPIGA MAGOTI NJE. ANGEENDA KUOMBA NJE KWA MIRADI YOTE BASI DENI LINGEKUWA KUBWA ZAIDI YA HAPA. Miradi ikikamilika itajiendesha na maisha yatabadilika, hata nchi zilizoendelea zilitoka huko. Waliumia wachache kwa faida ya wengi.

NISHATI Kwenye nishati Rais Magufuli amehakikisha mikataba ya madini inapitiwa upya na kuwa na win win stuation for both sides. Investors wapate chao lakini hata Taifa lipate chake. Hii imesaidia kuongeza mapato ya Taifa. Pia ameanzisha masoko kwenye kila wilaya yenye madini ili kuwe na center moja ya kuuzia madini.

Sambamba na hilo kwenye nishati ya Umeme pamoja na viiji zaidi ya elfu 13 kwenda kupitiwa na Umeme wa REA, lakini Rais Magufuli anajenga mradi wa umeme wa Nyerere ambao ulishindikana miaka yote. Mradi huo ukikamilika utakuwa unazalisha umeme zaidi ya huu tulionao sasa. Hii itafanya umeme kushuka bei. Umeme ukishuka bei basi hata bidhaa zitashuka bei kwakuwa umeme na bidhaa ni SIMULTANEOUS EQUETION kwani vinategemeana.

Pamoja na mambo mengine hivi unatoa wapi hoja za kumzuia Rais Magufuli 2020. Dunia nzima inajua kuwa kuna Rais mmoja tu afrika ambaye ameamua kufanya mapinduzi ya Taifa lake ambaye ni Rais Magufuli. Mnasubiria siku Mungu akimchukua ndipo tukaanze kumsifia? Kwa nini tusiseme akiwa hai li kumtia shime na kumuongeza ari ya kuchapa kazi kwa faida ya vizazi vijavyo? Kwani akistaafu atabomoa SGR? Akistaafu atauza ATCL? Akistaafu atabomoa mabarabara?

#JPM MITANO MINGINE.
 
Hongera Magufuli kwa kujali Watanzania Endelea kuchapa kazi Wale wasaliti wa Nchi sijui wataweka wapi sura zao

Wapinzani watafute shughuli za kufanya
 
Elimu bure ilikuwa hoja ya Chadema kwenye uchaguzi mkuu wakati wa Dr. Slaa. Afya hivi sasa ni aghali sana kiasi watu wengi wamerundikana kwenye uponyaji unaofanywa na kina Bulldozer kiasi cha kusababisha vifo.
 
Naunga mkono hoja, na kwa vile kuna miradi mikubwa 5 ya kimkakati inafanyika katika awamu yake,
  1. ATC kuwa kama Ethiopian Air au SAA
  2. SGR kuenea nchi mzima
  3. Umeme wa Stigler
  4. Ujenzi wa Mtambo wa LNG
  5. Roll out Tanzania ya Viwanda
Miradi yote hii ikikamilika, inainadili Tanzania kutoka nchi masikini kuwa ni nchi ya uchumi wa kati, uchumi wa gesi na Tanzania ya viwanda kuelekea kuwa a donor country.

Kwa vile miradi hii, yote ukiondoa Stigler, haiwezi kukamilika ndani ya kipindi chake cha urais cha miaka mitano iliyobakia, then nashauri tumpatie muda wa kutosha kukamilisha mipango yake atuache tukiwa a donor country.

P
 
Ufafanuzi wako ni wa kitaaluma, na mimi kama kijana ninayepaswa kujifunza sana kwenu Ma senior ninachukua hii kama changamoto kwangu. Kudos Mr Pascal
 
Katika mambo ambayo huwa najiuliza bila kupata majibu ni hili la kila wakati watu kumsemea na kumsifia Jiwe. Utafikiri tupo kwenye kampeni. Yaani miaka yote mitano ya madarakani wananchi hawajaona kwa macho yao uzuri wa huyu jamaa hadi waendelee kuambiwa na wengine? Kama hayo mazuri yapo na wote tunayaona, kuna haja gani ya kupoteza muda kuelezea kitu ambacho wote tunakishuhudia? Hiki mnachofanya cha kumsifia na kumsemea kila wakati kinaonyesha kwamba hayo maajabu aliyoyafanya na anayoyafanya yanaonekana kwa ninyi wachache. Na hapo ujiulize swali, kama huyu ni wa sisi wote na kwa hiyo anachokifanya tunakiona wote kuna haja gani ya kutusimulia tunachojionea wenyewe?

Yaani hiki ni kituko cha mwaka. Hadi leo mbunge au diwani akihama chama chake kwenda CCM anaanza kutuhubiria uzuri wa hili lijamaa. Kwani hayo mazuri huwa anayafanyia gizani mliko ninyi tu? Acheni kumdhalilisha hadi kuonekana ni mtu asiyeweza kusimama kwa miguu yake mwenyewe.
 
Naunga mkono hoja, na kwa vile kuna miradi mikubwa 5 ya kimkakati inafanyika katika awamu yake,
  1. ATC kuwa kama Ethiopian Air au SAA
  2. SGR kuenea nchi mzima
  3. Umeme wa Stigler
  4. Ujenzi wa Mtambo wa LNG
  5. Roll out Tanzania ya Viwanda
Miradi yote hii ikikamilika, inainadili Tanzania kutoka nchi masikini kuwa ni nchi ya uchumi wa kati, uchumi wa gesi na Tanzania ya viwanda kuelekea kuwa a donor country.

Kwa vile miradi hii, yote ukiondoa Stigler, haiwezi kukamilika ndani ya kipindi chake cha urais cha miaka mitano iliyobakia, then nashauri tumpatie muda wa kutosha kukamilisha mipango yake atuache tukiwa a donor country.

P

1.Vipi kuhusu hali ya umasikini kwa wananchi?
2. Vipi kuhusu ajira kwa vijana wanaohitumu vyuo na vyuo vikuu, maana tangia 2015 hajaijiri kama mtangulizi wake?
3.vipi kuhusu ongezeko la mishahara kwa wafanyakazi wa umma?, maisha yanapanda ila mishahara ni ileile tangia 2015
4. Vipi suala la katiba mpya( kilio cha wananchi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
1.Vipi kuhusu hali ya umasikini kwa wananchi?-
Ndio tunaibadili nchi kutoka nchi masikini hadi kuwa donor cantri.
2. Vipi kuhusu ajira kwa vijana wanaohitumu vyuo na vyuo vikuu, maana tangia 2015 hajaijiri kama mtangulizi wake?
Tunajikita katika kujiajiri na sio kuajiriwa, job creation, Tanzania ya viwanda ita create milions job openings
3.vipi kuhusu ongezeko la mishahara kwa wafanyakazi wa umma?, maisha yanapanda ila mishahara ni ileile tangia 2015
Kwa sasa tunatumia fedha zote kutekeleza miradi ya kimkakati, ikikamilika ndio tutaongeza mishahara.
4. Vipi suala la katiba mpya( kilio cha wananchi
Katiba mpya sio kipaumbele chetu!.
P
 
1.Vipi kuhusu hali ya umasikini kwa wananchi?
2. Vipi kuhusu ajira kwa vijana wanaohitumu vyuo na vyuo vikuu, maana tangia 2015 hajaijiri kama mtangulizi wake?
3.vipi kuhusu ongezeko la mishahara kwa wafanyakazi wa umma?, maisha yanapanda ila mishahara ni ileile tangia 2015
4. Vipi suala la katiba mpya( kilio cha wananchi

Sent using Jamii Forums mobile app

Vipi Demokrasia, uhuru wa kuwa na fikra huru, uhuru...
 
Naunga mkono hoja, na kwa vile kuna miradi mikubwa 5 ya kimkakati inafanyika katika awamu yake,
  1. ATC kuwa kama Ethiopian Air au SAA
  2. SGR kuenea nchi mzima
  3. Umeme wa Stigler
  4. Ujenzi wa Mtambo wa LNG
  5. Roll out Tanzania ya Viwanda
Miradi yote hii ikikamilika, inainadili Tanzania kutoka nchi masikini kuwa ni nchi ya uchumi wa kati, uchumi wa gesi na Tanzania ya viwanda kuelekea kuwa a donor country.

Kwa vile miradi hii, yote ukiondoa Stigler, haiwezi kukamilika ndani ya kipindi chake cha urais cha miaka mitano iliyobakia, then nashauri tumpatie muda wa kutosha kukamilisha mipango yake atuache tukiwa a donor country.

P
Sasa pamoja na yote hayo yaliyofanywa na awamu hii mbona bado ni WAOGA MNO to LEVEL the playing Field?hivi ni kweli mkuu unakubaliana na our no 1 kuwa akikaa pale Magogoni anateua watendaji wakuu wa kuendesha na kutangaza matokeo ya uchaguzi wakati vile vile ni Chairman wa chama cha kisiasa kinashoshiriki katika uchaguzi huo?wewe umshakuwa mwandishi nguli wa habari ninategemea unapokuwa unatoa maoni yako unaangalia na upande wa pili wa story,hii si sawa kwa political cadres kuwa ndio waendeshe uchaguzi ;Ninaahidi hili Mr.Mayala Mwenyezi Mungu akiniweka hai next year nitakununulia return tickets na accomodations ya siku 7 nitakulipia ili uende SA ukaone jinsi uchaguzi wao unavyoendeshwa na matokeo yake yanatangazwa vipi.ni vema sisi middle class tuwe na mtazamo unaojipambanua kidogo ,but ni haki yetu to differ ILA Facts zibakie hivyo otherwise tunaifanya JF kama kijiwe cha kahawa,level uliyofikia ni ya kujivunia na watu wengi wanakuchukulia kama role model wao,always ukweli utawale .
 
Mr.Mayala kwa taarifa yako SAA ipo in ICU!!!!,President Zuma ameuiwa na guptas wake,kumbuka our own Chavdas hapa???,kamuulize mzee Mrema nini alikipata katika uchunguzi wake,na kifo hiki kikamwondoa mwasisi wa hoja hii T.Sanga bila ya ukweli kujulikana,ila kuna siku utajulikana.
 
Umejaza utumbo tu kwa sababu na wewe ni msaka tonge
Umeandika jitiahida pekee hujaandika alipoboronga
1 ajira zimeenda kuzimu
2 umaskini umependa au kuongezeka
3 mauzo ya nje yameshuka Sana
4 diplomacy ya Tanzania ipo ICU
5 haki na Uhuru wa kidemokrasia hakuna
6 Tanzania Haina Tena uchaguzi Kama Korea kaskazini
7 ameharibu zao la korosho kwa kuingilia mipango bila utafiti
8ukanda,upendeleo,ukabila ( kila kitu chato eg airport,mbuga, hospital ya rufaa,taa za Barabarani porini,mahakama ya kisasa,
9 kupotea kwa wanasiasa na wanaharakati bila maelezeo yeyote
10 kuua umoja wa kitaifa na upendo wa watanganyika
 
Ufafanuzi wako ni wa kitaaluma, na mimi kama kijana ninayepaswa kujifunza sana kwenu Ma senior ninachukua hii kama changamoto kwangu. Kudos Mr Pascal
Dogo kila uzi lazima uweke namba ya simu nakushauri kama unanjaa fanya shighuli za musiba utaonekana vyema na mukulu.
 
Back
Top Bottom