Rais Magufuli amtuma RC wa Mbeya kusitisha uvunjaji wa Hotel Desderia inayomilikiwa na Joseph Mbilinyi (Sugu) kwa kisingizio cha mazingira

Hii hali ya maamuzi mengi tena mengine madogo madogo kufanywa na rais inaonyesha nchi iko kwenye hali mbaya sana. Rais amekuwa ndiye Katiba na sheria za nchi. Kwa nini nchi imeingia kwenye mtego mbaya namna hii? Kila kitu anaangaliwa rais. Hivi hata yeye haoni kuwa ni tatizo kubwa sana? Tumepata hasara kubwa sana.

Huu ni ushahidi kuwa utawala wa sheria nchi hii hauna maana yoyote.
 
Haaa imeisha iyoo.
hapo Sugu kalainishwa tayari,tena ameshatoa na shukrani za dhati kwa muheshimiwa Rais ambae awali akutambua ushindi wake.
Tuhesabu siku.
Akuna mkate mgumu mbele ya chai.
Ulitaka ajibu kivipi?? Mbona maccm mmekaa kiboyaa??
 
Kumkomoa tu ili maisha yampige. Kumbuka jiwe aliamuru bilicana iliyokuwa inamilikiwa na Mbowe na kumuingizia pesa ndefu kila mwaka ivunjwe bila sababu yoyote ile ya maana bali kuonyesha udikteta wake kwamba naivunja na hakuna chochote unaweza kufanya.
Hotel Desderia si ndio ya Sugu? Hivi wakimvunjia wanapata faida gani zaidi ya kumtia hasara mwenye hoteli pamoja na kuwafanya watu wapoteze ajira zso na serikali kukosa kodi?
 
Akizungumza hotelini hapo Mkuu huyo wa Mkoa wa Mbeya amedai kwamba amepata maelekezo kutoka kwa Rais wa Tanzania kwamba Hoteli hiyo isivunjwe kwa vile inavyo vibali vyote vilivyotakiwa kabla ya ujenzi wake na kwamba vyanzo vya maji vilivyopo karibu na hoteli hiyo havijaathirika , hivyo hakuna sababu yoyote ya kuhujumu hoteli hiyo .

Hotel ya Kisasa ya Desderia inamilikiwa na Joseph Mbilinyi aliyekuwa Mbunge wa Mbeya Mjini

Niliwahi kuweka uzi humu kuhusu jambo hili lakini ulifutwa kibabe bila hata kuupa nafasi ya kuomba maji ya kunywa , bali nilichojifunza ni kwamba UKWELI HAUFICHIKI , leo kiko wapi ?

Yanatafuta sifa za kijingaaaaaa!
 
Kwa kuwa maamuzi ya NEMC yalikuwa ya hovyo, inatakiwa aliyetoa maamuzi hayo awajibishwe
 
Wametafuta tu njia ya kumuweka jamaa Mtu kati ili mwishowe ashuke chini achane na mawazo ya siju Mbunge wa mbeya.
 
Wabunge wamenona kweli kweli wakati chama chenyewe hata ofisi HAKINA, chadema chadema chadema [sisi kwannza ustawi wa taasisi kesho]
 
Hata wa kimara watashinda kesi usione wamekaa kimya tu wanasubiria mwingine akiingia tu kesi zinafufuka Hawa watawala wanapita lakini haki za watu hazitopita asipolipa anaye atalipa mwingine.
Hata "green houses" lukuki za mh. Mbowe
 
Akizungumza hotelini hapo Mkuu huyo wa Mkoa wa Mbeya amedai kwamba amepata maelekezo kutoka kwa Rais wa Tanzania kwamba Hoteli hiyo isivunjwe kwa vile inavyo vibali vyote vilivyotakiwa kabla ya ujenzi wake na kwamba vyanzo vya maji vilivyopo karibu na hoteli hiyo havijaathirika , hivyo hakuna sababu yoyote ya kuhujumu hoteli hiyo .

Hotel ya Kisasa ya Desderia inamilikiwa na Joseph Mbilinyi aliyekuwa Mbunge wa Mbeya Mjini

Niliwahi kuweka uzi humu kuhusu jambo hili lakini ulifutwa kibabe bila hata kuupa nafasi ya kuomba maji ya kunywa , bali nilichojifunza ni kwamba UKWELI HAUFICHIKI , leo kiko wapi ?

Apo Sawa Mr RC
 
Shukrani hizo zimekuja baada ya mheshimiwa rais kumtuma mkuu wa mkoa wa Mbeya kuzuia ubomoaji wa hoteli ya Desderia iliyokua inadaiwa ujengwa eneo la chanzo cha maji

Rais Magufuli amesema Sugu kama muwekezaji aliyeamua kuwekeza mbeya pia apewe kipaumbele kwenye maeneo mengine ya uzunguni aweze kuendeleza uwekezaji

Maendeleo hayana vyama
 
Asiyeelewa! Angekataa ombi la kutaka amsugue,Hotel ingebomolewa tu! CCM Oyeee!
Kwa kweli JPM ni muungwana saanaa.
 
Shukrani hizo zimekuja baada ya mheshimiwa rais kumtuma mkuu wa mkoa wa Mbeya kuzuia ubomoaji wa hoteli ya Desderia iliyokua inadaiwa ujengwa eneo la chanzo cha maji

Rais Magufuli amesema Sugu kama muwekezaji aliyeamua kuwekeza mbeya pia apewe kipaumbele kwenye maeneo mengine ya uzunguni aweze kuendeleza uwekezaji

Maendeleo hayana vyama
Kwani kulikuwa kuna kosa kwa uwekezaji wake hadi serikali kutaka kuibomoa hoteli hii?
 
Back
Top Bottom