Rais Magufuli amteua Ndg. Waziri Kindamba kuwa Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCL

Watanzania bwana. Burudani sana. Yaani mtu hata hajaanza kufanya kazi wameshaanza kumkatisha tamaa.
Mkuu, umeshawahi kuona Meneja wa Mkoa Tanroads asiye Mhandisi wa Ujenzi/Barabara? Unahisi ni kwa nini?
Kuna kazi lazima boss awe na taaluma inayoendana na kazi husika.
Kadri ya resume iliyoko humu JF,huyo CEO mpya wa TTCL inaonekana yuko vizuri kwenye mambo ya Banking, Mambo ya fedha na Uchumi.
Alitosha sana kuwa sehemu kama BOT, TRA, nk.
 
Nampongeza Ndugu Waziri Kindamba kwa kuteuliwa kwake Acting CEO wa TTCL,Sina shaka na experiences ya uongozi ameanza kuongoza mda mrefu sana tangia Azania 1996-1999, wasiwasi wangu ni ufahamu wa telecom industry hapo ndio tatizo,tuombe CTO (Chief Technical Officer ) asimuangushe maana akimpa kisogo tu au akiwa anamuingiza king basi TTCL inakufa kwa mara ya pili mikononi mwake.
 
NDUGU HOJA ZAKO ZINAMSINGI..INAWEZEKANA NDO MAANA MH RAIS KAMTEUA KUKAIMU. JUU YA CEO ANAYEONDOKA NADHANI KUNATATIZO LA KIMSINGI LILILOFANYA MPAKA MH RAIS AMUONDOE. LAKINI PIA LAZIMA TUJUE KUWA KUONGOZA TAASIS KAMA ILE SI LAZIMA UWE UMEOBOMEA KWENYE TELECOMMUNICATION TU. NACHOJUA TTCL INAWATAALAMU WENGI SANA HIVYO UKIPATA CEO WAKUJUA KUWATUMIA HUKU AKIWABINGWA WA MIPANGO YA BIASHARA NA KUWAMOTISHA WAFANYAKAZI BASI SHIRIKA LITAFANYA VIZURI SANA.NGOJA TUSUBIRI TUONE.
Usijidanganye maswala ya kitaalamu yanahitaji mtaalamu hauwezi kuwa CEO wa kampuni ya simu huku Hauna ABC za telecom eti kisa una uzoefu wa uongozi,kutegemea watu wengine ndio kilichoua makampuni na mashirika mengi maana hao unaoeategemea wakishajua kwamba we ni kilaza ni kukudanganya huku wao wakipiga 10% kwenye ununuzi,wanaweza kukwambia uaprove ununuzi wa kitu ambacho hakina umuhimu wowote ili mradi wapige pesa tu at the end kampuni haifanyi vizuri na inakufa kabisa.
 
Yaani unadanganya 40 hayajafika, dogo anatoka mtaa wa Ndanda Kkoo na baba yake ndio alikuwa na ukumbi wa kindamba miaka ya 1990s
Safi sana kaka..kuna watu wanapenda tu kubisha wasivyovijua..Waziri ni mtoto wa Kkoo misheni kota.kama ana umri Mkubwa basi in miaka 35.hazidi hapo..
 
Nch
View attachment 405735
b98761215300a0b1db354e3b48cef7be.jpg

ELIMU NA SIFA

Chuo Kikuu cha Sunderland – Uingereza
Shahada ya Uzamili ya Utawala wa Biashara (MBA)

Chuo Kikuu cha London Metropolitan – Uingereza
Shahada ya BA (Hons), Benki, Uchumi na Sheria (Daraja la kwanza)

Chuo Kikuu cha Leicester- Uingereza
Stashahada ya Stadi za Utawala (Benki na Huduma za Fedha)

Sekondari ya Tambaza, Dar es Salaam, Sekondari ya Azania, Dar es Salaam, Tanzania

KAZI NA UZOEFU

Diamond Trust Bank (T) Ltd. (Dar es Salaam – Tanzania)
Meneja wa Tawi na Mjumbe wa Timu ya Viongozi Waandamizi , Tawi la Morocco, Kinondoni, Dar es Salaam, tangu mwaka 2011 mpaka sasa.

National Bank of Commerce (NBC), Dar es Salaam – Tanzania) Fraud-Risk Meneja

City Banking and Finance College (London) - Mhadhiri na Mkuu Msaidizi wa Taaluma
Nchi nyingi ikiwemo China serikali ndio mmiliki Wa makampuni makubwa ya simu ikiwemo China mobile na China unicom,inakuwaje Tanzania tunaachia sector muhimu kama simu kwa usalama Wa Taifa zimilikiwe na watu binafsi,hizi nji zinasema tusifanye biashara mbona wao wanafanya biashara kwa kuendesha makampuni mbali mbali? Tanzania tumelala sana,ni wakati Wa kuamka sasa
 
Hata sielewi ameangalia kigezo gani huyu!

Kazaura mbona amesomea kabisa hayo maswala ya mawasiliano? Sasa unamleta mfanyabiashara ili iweje? Ataweza kweli kuchanganua maswala ya ki-injinia huyu? Au ndo yale yale ya kutegemea kumezeshwa simbi tu? Haya bwana "KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI"
Wewe hovyo kabisa,kwani umeambiwa TTTCL ina tatizo la ma engineer
Ttcl inahitaji mtu wa kuifanya ipate faida kwa kutumia kidogo,fundi hataweza kufanya kazi hiyo
 
Nakukumbusha Rais wetu mpendwa kuwa mwaka wa kwanza wa muhula wako wa kwanza unakwenda ukingoni. Hii ina maana kuwa 1/5 ya ahadi zako zinapaswa kuwa zimetekelezwa hadi sasa. Ni ukumbusho tu
Hujaona tu,Ttcl,Atc,Trl,zote zinafufuka
 
Kama ndio Kindamba wa Azania boys..mwana kariakoo.ambaye aligombea ubunge na zungu ILALA,basi huyu sio mwanaCCM wa kiviile..huyu aligombea ubunge ili kutafuta kiki tu kama watoto wa mjini wasemavyo..lkn kwa Sie tunaomfahamu hana uCCM kabisa.kuna watu wengi wanaogombea ubunge kupitia ccm lakini ni ccm kadi tu..mfano marehemu filikunjombe nk
Unaweza kuwa sahihi maana yupo katika mailing listi TAARIFA YA SIRI: Nimetumiwa Nami Naiwasilisha Kama Ilivyo ~ Kulikoni Ughaibuni
 
TTCL ni bonge la kampuni tatitzo wanasiasa na huyo kazaura walikuwa wanairudisha nyuma makusudi kwa faida zao binafsi,kuhusu wataalam , TTCL wapo hasa wazee ambao ni watalaamu hasa ingawa hawana elimu kubwa, huyo aliyeteuliwa anafit huoni ana MBA, watalaamu wa mawasiliano ni mafundi ambao ni wazee kwenye hiyo kampuni, kwenye post ya CEO anatakiwa mtu anayejua biashara , leo nilikuwa na jamaa anafanya kazi TTCL ,anakwambia wafanyakazi wa TTCL wamefurah saana baada ya kamugisha kupigwa chini, binafsi amenieleza mambo mengi ambayo siwezi kuyaandika hapa

Well said Tracy, kama mambo yenyewe ndiyo hayo mimi hapo sitii neno naunga mkono hatua za Rais - ndiyo maana nasema kama kuna mambo alikuwa anafanya ya ndiyo sivyo hapo ujilahumu mwenyewe na akiwa amevunja ethics za kiuhadisi/Engineer alizo take an oath kuzisimamia na kuzilinda ndio basi tena - from now on atakuwa ame-learn his resson the hardway kama kuna ukweli katika shutuma levered against him.

Tracy binafsi bado na insist kwamba kutokana na on going Mega Project za kiufundi katika Shirika hilo, msimamizi i.e CEO atafutwe mwenye background ya Uandisi Mawasiliano no siyo Human Resources Management, Marketing au mambo ya Biashara watu wa design ya namna hiyo wataitajika baadae kabisa baada ya kukamilisha ufungaji wa mitambo na network nchi nzima.

Binafsi uwa sielewi kwa nini watu wengi wanakuwa carried away na watu wenye shahada za MBA, wanawachukulia kama cure all like an analgesics medicine - principles za Markov ndiyo iwe nongwa!!

Mimi sina shaka na wahandisi wa TTCL wa muda mrefu kwenye Shirika wao bado ni treasure trove and they can do wonders wakiwezeshwa na kupewa motisha.

All in all bado nalitakia kheri Shirika letu la UMMA lijitahidi kuleta changa moto na ushindani wa kweli usiyo kuwa na traces za u- cartel kwenye sekta ya mawasiliano - hicho ndicho nakipigania mimi.
 
Ubunifu unatakiwa.. Hao wahandisi hawajui marketing na Branding.. Je huyo Kindamba ni mjuvi wa hayo mambo? Ana experience Kwenye Telecom? Binafsi MBA za Bongo siziamini

Ova.
 
Mkuu, umeshawahi kuona Meneja wa Mkoa Tanroads asiye Mhandisi wa Ujenzi/Barabara? Unahisi ni kwa nini?
Kuna kazi lazima boss awe na taaluma inayoendana na kazi husika.
Kadri ya resume iliyoko humu JF,huyo CEO mpya wa TTCL inaonekana yuko vizuri kwenye mambo ya Banking, Mambo ya fedha na Uchumi.
Alitosha sana kuwa sehemu kama BOT, TRA, nk.
We jamaa unajua sana. CEO sio mtu mdogo. Anatakiwa awe mbobezi kitaalam na kiuzoefu.. Hapo wameongeza Kada tu
 
Hata sielewi ameangalia kigezo gani huyu!

Kazaura mbona amesomea kabisa hayo maswala ya mawasiliano? Sasa unamleta mfanyabiashara ili iweje? Ataweza kweli kuchanganua maswala ya ki-injinia huyu? Au ndo yale yale ya kutegemea kumezeshwa simbi tu? Haya bwana "KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI"
Unataka kutuambia pale hakuna wataalam kabisa. Shirika linatakiwa liendeshwe sasa kibiashara. Kazi ya utaalam wapo wataalam wengi pale. huyu bwana naona amebobea kwenye biashara na ataweza nadhani
 
Hata sielewi ameangalia kigezo gani huyu!

Kazaura mbona amesomea kabisa hayo maswala ya mawasiliano? Sasa unamleta mfanyabiashara ili iweje? Ataweza kweli kuchanganua maswala ya ki-injinia huyu? Au ndo yale yale ya kutegemea kumezeshwa simbi tu? Haya bwana "KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI"
Amen
 
Hata kama CEO sio lazima awe engineer lakini anatakiwa awe mtu ambaye amewahi kufanya kazi kwenye telecom industry.

Huwezi kumtoa junior manager wa tawi la bank eti unampa kuwa CEO wa kampuni kama TTCL.

Hao mnaosema kuna engineers atawategemea ndio hao hao wamelifikisha shirika hapo.

Inatakiwa CEO mwenye vision mpya kuhusu TTCL. Huwezi kuwa na hiyo vision kama hujui current trends kwenye hiyo sekta.

Ila ni kaimu labda kaenda kuchunguza vitu baadaye atakuja mwingine.
 
Niwashukuru sana Kimweri na Bukyanagandi kwa hoja zao.

Nilichokipata kutokana na maelezo yao ni kueleza hoja na si kueleza mtu. Nichangie senti sumuni

1. Kimweri anasema ipo haja ya kumpunguzia Rais madaraka. Nakubaliana nalo na rasimu waliokataa ilikuwa imeliona hili.

Wakakataa kwasababu wanataka kutumia fursa hizo ki CCM badala ya umma

Tatizo si kwa shirika , kila taasisi kiasi kwamba jukumu la kuongoza limekuwa la mtu na si timu

Bila kubadili mfumo wetu wa sasa haya yataendelea na teuzi zisizo na 'vetting' bali choice zitaendelea

2. Bukyanagandi ameeleza kuhusu umuhimu wa sekta ya mawasiliano.

TTCL kama shirika la umma linabeba sehemu muhimu sana ya uchumi.

Sekta ya mawasiliano duniani na hata hapa nchini ni eneo muhimu la uchumi wa taifa.

Kwa muda mfupi tu wa miongo miwili sekta hiyo imechangia sana katika pato la taifa na pato la wananchi licha ya ukweli kuwa kuna 'hujuma' kutoka private sector

Pamoja na uchumi, TTCL ni sehemu ya usalama wa Taifa. Tutakapoacha private sector itawale katika nchi changa kama yetu , tutakuwa na tatizo kubwa mbele ya safari

Kwasasa mashirika ya binafsi yanashirikiana kuhakikisha hakuna ''competition'' Zaidi yao wenyewe

Hilo ni kwa hasara ya waumiaji. TTCL ingeweza kuweka mizani kwasababu , kwanaza, ingekuwa mshindani, na pili ina advantage kwa monopoly yenye ni njema

Wachangiaji waanamzungumzia mtu, tumesahau kubinafsishwa kwa TTC kulikuwa na matatizo.

Kwanza, wakauziwa waholanzi, kisha mwingine mwisho serikali ikachukua shea zote. Katika mlolongo huo watu wamechota mipesa na kuishia zao

Nakumbuka mwekezaji wa kwanza alipewa shea na kisha kukopa kutoka serikali

Kwamba, hakuja na mtaji bali alitumia pesa zetu kununua chetu na kuwekeza kwetu

Kama tumerudisha 100% ya shea, ni sababu gani zilizotufanya tuuze na kisha kununua mali yetu?

Tukija kwa hawa wanaoongelewa, sekta ya mawasiliano inahitaji watu waliobobea.

Tuna wataalam wa kutosha ndani na nje. Sina uhakika uteuzi wa meneja kuongoza taasisi nyeti na yenye ushindani kama TTCL ni jambo la kuchukulia kirahisi

Kiongozi wa shirika kama TTCL alitakiwa apatikane kwa 'vetting' ya hali ya juu sana ikihusisha wataalamu. Hata kama tutatumia consulting firm kama PWC ni bora

Tusimalumu kiongozi aliyekuwepo, mfumo wetu wenye bodi za kuteuliwa na mtu, mawaziri na makatibu wakuu wakuteuliwa na mtu ni tatizo linguine.

Pengine alikuwa na nia njema, lakini je angeweza kupambana na nguvu za siasa? Yes nguvu za siasa kwasababu teuzi zinazingantia siasa Zaidi kama tunavyoona siku za nyuma na kuendelea

Yote haya yanatokana na jambo moja, kuweka mayai katika kikapu kimoja alichobeba mtu

Sijui nikushukuru vipi ndugu Nguruvi3 na Kimweri

- asanteni sana na Mungu awalinde kwa kujali ustawi wa Taifa letu kwa kujitolea kusema ukweli na kutumia taaluma na uzoefu kuonyesha udhaifu na loop holes zinazo tumiwa na watu wachache kukwamisha TTCL hawataki istawi ni hii ndiyo Modus Operandi ya makampuni yanayo fanya shughuli zake kama cartel hata siku moja hawatakubali kampuni iliyo chini ya Serikali ione the light of the day - Dk.Magufuli hilo anapaswa kuliwekea maanani sana linapo kuja suala la TTCL, makampuni ya simu yana misuli ya kufanya lolote ku compromise yeyote kuwajengea watu mizengwe ili mradi wao wabaki bila mshindani wa kweli - been there, be warned.
 
Back
Top Bottom