Rais Magufuli amteua Ndg. Waziri Kindamba kuwa Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCL

Mashinji kapewa ukatibu mkuu katika Chama ambacho kinamatumaini ya kupata dola.. Hana experience yoyote ya Uongozi
Naona umeamua kujitoa ufahamu hapa. Katibu wa chama umeambiwa anatakiwa kuwa wa fani gani? Huyo kindamba hakuna hata aliposoma certificate ya mawasiliano yeye ni fedha tu, halafu unampa shirika la mawasiliano. Labda amekuja kukusanya fedha zaidi huenda kulikuwa na shida eneo hilo.
 
Umesahau kumwambia kuwa kwa miaka mingi kabla ya makampuni binafsi kuanza kufanya biashara za mawasiliano,TTCL mlikuwa mungu watu,wazembe,wala rushwa,kubambikia madeni ya simu ya watu wengine. Niliomba land line iliokuwa na maungio tiyari kwa miaka minane sikuipata,hadi walipokuja washindani wenu Mobile phone companies ndio mkaja na upole kuliko wa kanisani nami nikawatosa kwa hasira.Kibaya zaidi bado mliombwa na wadau wa simu kuwa badirisha au ongeza huduma ya mobile service mkayaponda wacha mshike adabu.TTCL hawana ubunifu na kamwe hatakuwa na ubinifu ni mzigo labda iendeshwe na wananchi watakaonunua hisa za TTCL.
enzi unazoongelea uzembe ulikuwa kila mahali tanzania hii sasa kuna dalili za watanzania kuzinduka na kutaka kwenda uchumi wa kati usipende kukumbatia maovu yaliyopita na kutaka kuyafanya yawe facts za kupinga ukweli.
 
Bukyanagandi, nimekuelewa lakini hujanishawishi hasa kwa kujaribu kuonyesha kuwa TTCL ni ufundi pekee- yeye ni fundi je suala la masoko analifanyaje, ambako kwa maoni yangu ndiko TTCL imeshindwa kabisa bado wako kwenye enzi zile za kale. TTCL wanazidiwa hata na polisi ambao wamepiga hatua moja mble kwa kuwaita wote wanaofika mbele yao kuwa ni wateja hata kama ni majambazi sugu. Uhandisi siyo WHOLENESS
jaribu kiifuatilia TTCL, hivi ni kampuni gani duniani linaweza kufanya vizuri kama mhusika serikali inachukua miaka 10 haijawekeza chochote katiaka miundombinu tukubali tulijikwaa sasa ni wakati wa kuinuka na kusonga mbele, Dr. kazaula kama binadamu alifanya anachoweza na akashindwa asichoweza tunamshukuru na kumtakia maisha mema huko aendako, lakini Mheshimiwa Kindamba naye anakalibishwa aje ajaribu kufanya anachoamini kitatusongesha mbele na tunamtakia mafanikio mema
 
Ni nchi za kiafrika pekee ndizo ziliamuwa kutowekeza ktk sector ya mawasiliano na kuwaavhia wawekezaji,tena kampuni nyeti kama TTCL haikutakiwa kutupwa kiasi maana ndio moja ya nguzo za usalama Wa nchi na kitega uchumi bora zaidi,ngoja tuone naimani kubwa na awamu hii ya tano naona kuna mazuri mbele yanakuja

Sent from my TECNO-M3 using JamiiForums mobile app
 
enzi unazoongelea uzembe ulikuwa kila mahali tanzania hii sasa kuna dalili za watanzania kuzinduka na kutaka kwenda uchumi wa kati usipende kukumbatia maovu yaliyopita na kutaka kuyafanya yawe facts za kupinga ukweli.
Onyesha Key Performancee Indicator (KPI) ya sasa kama TTCL ya leo ni tofauti na ile ya zamani,kama umefaulu hilo hukutakiwa kutulamba miguu kutafuta ruzuku ya walipa kodi,unatulamba miguu kwa sababu TTCL haina vision,hana utashi,haina financial plan halisi. Wakati wa majaribio umeishapita ni kitanzi ukishindwa au ni medali ya dhahabu orign ukiweza.
 
ok ngoja nisiongee na wewe na nikupe ushindi umeshinda kwahelii mkuu.
 
Kumbe ni kada wetu
Ukada ni tatizo kubwa. Branch manager wa benki anakuwa CEO wa shirika kubwa kama TTCL . Wafanyakazi ndani ya shirika hawamtaki kabisa huyu bwana. Wanadai hajui namna ya kuendesha shirika. Zaidi anavuruga
 
Bwana mkubwa ndiyo anapenda hivyo, Bashite, Gumbo, Mwakyembe, Happy, Mnyeti n.k
 
kwani kindamba bado ypo TTCL au

kama yupo je utendaji wake vipi

vip shirika bado limpaaa au

vipi wafanyakazi wameongezewa chochote
 
Back
Top Bottom