Kinoamiguu
JF-Expert Member
- Nov 29, 2018
- 10,526
- 13,015
Rais wetu haishi vituko, ni mtu anayependa umaarufu rahisi (cheap popularity) tafsiri ni yangu.
Juzi bwana Diamond akiwa Kigoma kwenye tamasha lake alimpigia simu kupitia simu ya Polepole. Kupitia simu ile alisikika akisema "watanzania mna bahati sana ya kupata Rais anayewapenda, tena anapiga simu usiku" alienda mbali zaidi kwa kusema anampenda na kumfuatilia Diamond. Naye bwana Plantnumz akajibu kwamba 2020 atapata 100% ya kura zote.
Ukifuatilia sana utagundua kwamba bwana mkubwa Magufuli anahisi kutokubalika kwa watanzania walio wengi. Pia ni kama mtu anayeomba huruma ya wapiga kura
Je, ile haikuwa kampeni ya wazi kabisa tena kabla ya muda?
Polepole alienda pale kama nani wakati hakuwepo hata kwenye ratiba ya Wasafi?
Kwanini Polepole na kwanini Kigoma?
Polepole alipanga na Rais kwamba wangepigiana simu? Rais alijuaje kwamba angepigiwa simu muda ule?
Kwanini bwana Magufuli kila apatapo wasaa hujinasibisha kwamba anawapenda watanzania?
Kuvamia majukwaa ya wasanii na kufanya siasa ni aina nyingine ya siasa za kishamba na kutojiamini. Wewe unajenga reli na ndege unanunua mbona unahangaika na micro politics?