Rais Magufuli ampigia simu Diamond akiwa jukwaani, Diamond amuhakikishia ushindi 2020

Rais wetu haishi vituko, ni mtu anayependa umaarufu rahisi (cheap popularity) tafsiri ni yangu.

Juzi bwana Diamond akiwa Kigoma kwenye tamasha lake alimpigia simu kupitia simu ya Polepole. Kupitia simu ile alisikika akisema "watanzania mna bahati sana ya kupata Rais anayewapenda, tena anapiga simu usiku" alienda mbali zaidi kwa kusema anampenda na kumfuatilia Diamond. Naye bwana Plantnumz akajibu kwamba 2020 atapata 100% ya kura zote.

Ukifuatilia sana utagundua kwamba bwana mkubwa Magufuli anahisi kutokubalika kwa watanzania walio wengi. Pia ni kama mtu anayeomba huruma ya wapiga kura

Je, ile haikuwa kampeni ya wazi kabisa tena kabla ya muda?

Polepole alienda pale kama nani wakati hakuwepo hata kwenye ratiba ya Wasafi?

Kwanini Polepole na kwanini Kigoma?
Polepole alipanga na Rais kwamba wangepigiana simu? Rais alijuaje kwamba angepigiwa simu muda ule?

Kwanini bwana Magufuli kila apatapo wasaa hujinasibisha kwamba anawapenda watanzania?

Kuvamia majukwaa ya wasanii na kufanya siasa ni aina nyingine ya siasa za kishamba na kutojiamini. Wewe unajenga reli na ndege unanunua mbona unahangaika na micro politics?
 
So ulitaka ampigie mama yako ndio ungekaa kimya.
Siasa ni namna gani unatumia fursa kdg ulioipata.
Hata wewe umetumia fursa hapa JF kumuonea wivu.
Watanzania tunashida mahali.

Tofa
Ilikuwa ni burudani kama simu wangepigiana private sio public.Watu walifata show awakufata kusikiliza Simu.Labda tu kama nia ilikuwa ni ufunguzi wa kampeni kupitia show
 
Ilikuwa ni burudani kama simu wangepigiana private sio public.Watu walifata show awakufata kusikiliza Simu.Labda tu kama nia ilikuwa ni ufunguzi wa kampeni kupitia show
Kwani wewe ukipigiwa simu na mumeo hua huweki loud speaker ili na watoto wamsikilize baba yao?
 
Kinoamiguu,
Huyu rais hakubaliki kabisa, wwanaomuunga mkono ni mbumbumbu na wapumbavu, ndio maana Twaweza walipotoa Ripoti yao ya Uchunguzi na kuonesha kukubalika kwake kumepungua mpaka kufikia 56% alitamani kuwapoteza, Na huo ni ushamba kupigia simu wahuni hao wa Bongo fleva kwa kutumia Kodi zetu
 
Rais wetu haishi vituko, ni mtu anayependa umaarufu rahisi (cheap popularity) tafsiri ni yangu.

Kwa miaka mitano ambayo JPM kawa madarakani ashakuwa maarufu sana; mno, tena sana.....anazungumzwa kila kona, akitaka kupita barabarani wewe unampisha, kila chombo cha habari, nyumba za ibada anasemwa.........LABDA USEME CHEAP POPULARITY INATAFUTWAJE? AU IKOJE? na ina tofauti gani na popularity ya kawaida? alivua nguo?


Ukifuatilia sana utagundua kwamba bwana mkubwa JPM anahisi kutokubalika kwa watanzania walio wengi. Pia ni kama mtu anayeomba huruma ya wapiga kura

Kuna uongo fulani, watu fulani , mahali fulani wanawaza kama wewe kuwa JPM hakubaliki!!! this is very wrong assumption, tena sana, JPM ana nguvu mara dufu ya kikwete na ana exercise power na maamuzi magumu kama rais kuliko yeyote aliyetokea siku za karibuni!!! KOSA kuwa ambalo iunafanya ni kuweka hisia zako, akili zako kama ionekane ni WOTE ndio wanawaza hivyo. Unajua katiba ya Tanzania hata JPM akipigiwa kura na watu wawili tu anakuwa rais??? unajua??

umetumia assumptions nyingi sana; ambazo hata mama yako mzazi anaweza kukushangaa au kukukana!!!


kuwa realistic, na matatizo mengi hata ya upinzani wetu ni HATUTAKI KUWA REALISTIC MAHALI PER REALISTIC, why?
 
6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom