Rais Magufuli ampandisha cheo Jaji Zephrine Galeba aliyetoa hukumu kwa lugha ya Kiswahili kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufaa

Hayo mawigi umeona ktk sinema za kinaijeria au mahakama za Tanzania? Una picha yeyote inayoonyesha Jaji au wakili wa kitanzania kavaa hilo wigi!!! Kila taaluma ina mfumo wake na kuazima vya nje si vibaya. Hata uniform nyota za wanajeshi tumerithi kwa wazungu hata mifumo ya jeshi tumerithi kwa wazungu waambie wanajeshi wavae migolole kama Mkwawa basi
Punguza hasira soma vitabu upate elimu sio mihemko,yupo binadamu ambaye yoote haya na mifumo yoote ya kidunia aliya buni na kuyatekeleza mpaka wa leo tumeiga huko babel na mbabe wao anaitwa nebchadneza,na baadae nimrod ukipata kitabu cha historia yake hutolaumu mfumo wowoote uliopo duniani
 
Comte humu usitegemee michango ya maana kwa post nzuri kama hii. Chagua wa kuwajibu, yatakuja matakataka mengi hapa

Kumbe majaji wetu na mahakimu wanabanwa na sheria kutoa hukumu zao kwa kiingereza. Ukaidi umemfanya Jaji Galeba kutoa hukumu yake kwa kiswahili na kuwa amevunja sheria hiyo. Hata hivyo ukaidi wakati mwingine ni muhimu ili kulazimisha mfumo ubadirike. Kwa ukaidi wake Jaji Galeba kapata cheo na huenda mfumo ukabadirika hivyo kufaidika mara mbili. HONGERA JAJI GALEBA
devience ni nini? Yale yale ya Jiwe na Kiingereza!
 
"... kulazimisha mfumo 'ubadirike"'.

Mtoa mada unapenda Kiswahili lakini hukijui.
 
devience ni nini? Yale yale ya Jiwe na Kiingereza!
Mkuu kwanza nifanye masahihisho- neno sahihi ni DEVIANCE
Hii ni dhana ambayo katika sosiolojia inaelezea vitendo vya mtu kukiuka utaratibu uliokubalika na kufanya tofauti- unaacha utaratibu na unatunga utaratibu wako na kufanya kwa kutumia utaratibu wako huo mpya.

Deviance, in sociology, violation of social rules and conventions.

ukipata mda soma kuhusu hiyo dhana utaona na kufaidika.

JPM katika utendaji wake amekuwa deviant sana
 
Angetumbuliwa kwa kukaidi tungesema "mwana kuyatafuta ...mwanakuyapata"
Ila kwa sababu amewin battle.....wooote tunamsifu.
Hawa ndo binadamu
 
Mkuu kwanza nifanye masahihisho- neno sahihi ni DEVIANCE
Hii ni dhana ambayo katika sosiolojia inaelezea vitendo vya mtu kukiuka utaratibu uliokubalika na kufanya tofauti- unaacha utaratibu na unatunga utaratibu wako na kufanya kwa kutumia utaratibu wako huo mpya.

Deviance, in sociology, violation of social rules and conventions.

ukipata mda soma kuhusu hiyo dhana utaona na kufaidika.

JPM katika utendaji wake amekuwa deviant sana
Noted, nitakuja kwako later, ngoja nifanya kazi kidogo
 
Kutambua mchango wake kukuza kiswahili ni sawa, lkn sidhani kama ni miongoni mwa vigezo vya promotion ya majaji. Angeweza kupewa nishani ya kiswahili tu. Hapa ndipo tunapokosa independency of judiciary.
 
Mkuu hajakuza yu kiswahili- kuna hoja nzito na nyingi sana za kisheria kazielezea vizuri
PATA MDA USOME HIYO HUKUMU
 
Attachments

  • Galeba.pdf
    595.8 KB · Views: 4
Huyo hata hajakaidi sheria na kanuni za kazi zinaruhusu kuandika hukumu kwa Kiswahili au kingereza mhe jaji kaonesha uthubutu nakuondoa mazoea View attachment 1692739
Naona hata heading ya post imebadilishwa baada ya hii post yako kuonyesha sheria inaruhusu Labour Court kuandika hukumu ya kiswahili tofauti na vitengo vingine.
 
Siyo Jaji wa kwanza kutoa hukumu kwa Kiswahili. Tangu enzi za kina Jaji Mwipopo Labour Court wanatoa hukumu za kiswahili kwa kuwa sheria inaruhusu kwa kitengo hicho cha mahakama kuu
 
Back
Top Bottom