ii ndio aina ya hoja za kuunga mkono uamuzi huo .....
watu wengi wanaojuwa mambo ya nchi na misingi yake aidha wameshikwa na bumbuwazi au wanatazama tu .....wale ambao siku zote mambo ya uzalendo kwao hayana maana ndio wamekuwa wakishangilia ....aina ya watu ambao hata ikitokea vita hawawezi kuipigania nchi yao kama hata misingi yake hawaiheshimu...
wanangojea kushangilia Mwenge kufutwa ...na pengine hata mashujaa tuache kuwakumbuka...ni gharama sana ....tutakuwa tunafanya tukipata pesa .....
wakati nchi ikiwa kati kati ya vita kali ya iddi amin ....maisha yakiwa magumu ..watu wamefunga mkanda haikuweza kuingia akilini kuacha au kuahirisha chochote cha kitaifa
Mimi nawaza mapumziko tu..Lakini mapumziko yapo palepale
View attachment 334770
Sisi tulitaka mabadiliko kuelekea kwenye Tanzania ya kipato cha kati wewe bado unatueletea hadithi ya uhuru.Tangu tupate uhuru tumeshawahi kubadili namna ya kukumbuka uhuru wetu?? wewe hilo gwaride unaona ni kitu kidogo sana eeh!...kwani wale wananchi wanaokusanyika makao makuu ya wilaya,mikoa,au taifa pale wanafuata chakula eeh...,Tusichukulie mambo kirahisi namna hiyo ..au watu kama nyie ambao wanamshauri bosi kile anachotaka kusikia ....mshauri mzuri lazima atofautiane na wewe ..ukiona una mshauri ambaye kila unachosema ..anaunga mkono ...ujuwe ni tatizo ...ni lazima mara nyingine awe na mawazo tofauti na yako na ayatete mradi awe genuine.....most ya ushauri ninaouona kwenye thread hii uko so genuine ...wala sio ligi.
Huhitaji hata dictionery hata kumjuwa DC aliyeandaliwa kwa ngazi yake kuwa kiongozi .....kama alivyowahi kusema Mwalimu.....rais akitaka anaweza kujeuka kuwa "Mungu" , anapokea mambo mengi mazito ambayo katika ubinadamu wa kawaida unaweza hata kupiga mtu ......lakini lazima awe na shock absorber ...watu wanaomzunguka ambao wanayachuja yale anayofikishiwa naye akiyapata anayachuja kwa utulivu
Sisi tulitaka mabadiliko kuelekea kwenye Tanzania ya kipato cha kati wewe bado unatueletea hadithi ya uhuru.
Tanzania kwa sasa tuko kwenye vita vya kiuchumi wewe bado unatuletea hadithi za vita vya kisiasa.
Tanzania ya sasa na ijayo inafanya maamuzi ya kitaifa kwa kutumia mzani wa kiuchumi na siyo kisiasa.
Kuna faida gani ya kufanya gwaride la kisiasa na kutumia mabilioni ya pesa za watanzania wote wakati watoto wetu hawana hata madarasa, madawati, vitabu na chaki.
Kuna faida gani ya kufanya sherehe kwa gwaride la kisiasa na kuteketeza mabilioni wakati hakuna hata vitanda na madawa kwenye hospitali.
Kuna faida gani ya kufanya sherehe kwa gwaride la kisiasa wakati wananchi vijijini wanatembelea makumi kama siyo mamia ya kilometre kwenda kwenye kituo cha afya au zahanati.
Kuna faida gani ya kufanya sherehe kwa gwaride na kutumia mabilioni ya pesa wakati wananchi hawana hata barabara zinazowarahisishia mawasiliano kiuchumi.
Hivi unadhani Rais Magufuli hafahamu umuhimu wa Muungano?
Wewe endelea kuishi jana na hadithi za uhuru!
Unashangaza kweli
Hoja yako ni ipi hasa. Rais wa Muungano ni nani? Na pesa ya Muungano unayo isema wewe ulitaka ikatupwe katikati ya Bahari ya Hindi? Hivi hujui hata Mwanza ni Jamhuri ya Muungano ? Mi huwa naona kuna watu hamuna haja ya kuchangia ila mnapoteza mda labda kwa vile Mb zina-expire.Swali zuri sana ulilouliza.
Nami niongezee hivi, huyo Magufuli siyo alitwambia kuwa masuala ya Zanzibar hawezi kuyaingilia kwa kuwa Zenji ni nchi kamili yenye mamlaka yake.
Sasa swali liko hivi, kama Muungano ni wa nchi 2 za Tanganyika na Zanzibar, sasa swala la kuamua kutumia pesa ya Muungano kwa matumizi ya Tanganyika peke yake, je hiyo siyo ubabe na kuingilia mambo ya Zanzibar?
Kuna baadhi ya watu ambao wao kazi yao ni kupinga kila kitu. Kuna wengine ambao hawajui wanachokipinga na kundi la mwisho ni wanafiki.Binafsi hii ndo vita yangu na hizi mambo za mapokeo!! Lazima tujue vipaumbele vyetu kama nchi ni nini, na tuchague kipi tufanye kipi tuache, development expenditure na recurrent expenditure?! Tujenge barabara au zahanati au tutumie tu kwa matumizi ambayo hayatokuja kutulipa in any way whasoever!!
Jamani, tukiambiwa kuthink out of the box ndio huku, ebu tuwe na guts za kujaribu mambo, ebu tuskip hizo sherehe za muungano for one year tu afu tuone pesa za pale tunaweza kuzidirect wapi kwingine, na tuone je ina tija au lah?! Kama itakuwa na tija, wale waliofaidika basi sikukuu ya muungano kwao itakuwa na maana tofauti kwao na wataanza kuienzi vizuri zaidi. TUBADIRIKE JAMANI
Yaani gwaride, vyakula na vinywaji ndio havifuti historia ya nchi? Ninatumaini unatania!Me naona hii inafuta historia za nchi .... Iv ina maana nchi zote zilizoendelea sherehe za kihistoria kama hizi wamezifuta pia?? Then muungano ni wa nchi mbili vipi iweje hiyo hela itumike bara tu visiwani isitumike tuseme ndio hamna matatizo mengi sana,,,,, ni bora iyo bil 1 itumike tanzania bara na nyingine visiwani
Soma yanayojiri nchi zilizoendelea, punguza kukariri. Patriotism haiji kwa kukusanyika national stadium, kupiga gwaride na kunywa soda;Misingi ya nchi huwa kwenye katiba ...bila hivyo hukika siku vikaja vizazi vikaanza kuona baadhi ya mambo ni ya kipuuzi kadiri ya umri wao....Misingi ya nchi haina mbadala ...na haiwezi tu kufutwa kwa sababu za kishabiki...tuacheni mihemko ..tunakoenda siko...lazima watu waende kwa sheria ..mila na taratibu ..huwezi tu kuamka na kusema ondoa hili ..peleka kule ../leo limekuwa zuri kesho limekuwa baya ...tunatabirika ?
kuna ambao bado wanaongelea juu ya kujitegeemea ...kila mtu anapenda tujitegemea ...tunamuunga mkono kiongozi wetu ..lakini ni wazi na dhahiri kuwa nchi ambayo inategemea wafadhili kwa asiloimia zaidi ya 40% haiamki tu asubuhi na kujitegemea ....tuambiane ukweli kuwa hatuwezi tu kukurupuka kujitegemea .....na kuanza kupayuka ...nendeni tunajitegemea tunajitegemea !!! bado tunahitaji wabia wa maendeleo kwa miaka kadhaa ijayo kabla ya kusimama wenyewe ..
hata kijaana huwa na hamu ya kujitegemea anapokuwa ...ila huwa hatua ..kuazia kujinunulia jozi yake ya viatu ...kumudu seehemu kubwa ya mahitaji..kuhama nyumbani na baadaye kumudu kuwa na familia na mwisho hadi kuweza kusaidia ndugu au wazazi au wahitaji baada ya kupata ziada ....wapo ambao huzeeka bila kufikia ndoto ya kujitegemea..
Unajuaje kuna hela ilitoka Zanzibar katika bilioni 2 zilizotengwa awali kwa maandalizi?Mkuu respect Mimi ningemshauri magu hiyo bil 2 moja ingekwenda zenji na iliyobaki ndio ingekwenda mwanza. Huu ni muungano sio 9 Dec.
Km ingekuwa wewe?Hili ni jambo jema na zuri sana.
Sioni kabisa tatizo lililopo hapo na kama ingekuwa mimi ningechukua uamuzi huo huo kama wa Magufuli.
Kuahirishwa siyo kuhairishwa.Huu muungano si wa nchi mbili? Hao upande wa zanzibar nao wamenufaika vipi kwa kuhairishwa hizo sherehe?
Kwanini asifanye hivi hata kwenye mbio za mwenge?Lakini mapumziko yapo palepale
View attachment 334770